87. Ukulibhona Ilyamponola Bayega

Collected by: Don Sybertz,  

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale walaliho munhu umo uyo witanagwa Bayega. Agasamila ng’wipolu uko bhalibhatiho abhanhu. Hanuma yahoo, bhanhu bhangi bhagandya gusamila uko lipolu lyenilo bhunsanga alikala bho mholele.

Agandya gubhagabhila amabala na gubhatimbwa ng’holo ya gwikala ung’wipolu. Bhanhu bhenebho bhaganumba noi uMayega bhung’winha Bhutemi.

Ubhiza Ntemi o ibala linilo. Bayega agayega noi ugwinhiwa Bhutemi. Ntemi Bayega olina maarifa mingi noi. Agafunya lilagilo ku bhanasi guti ntemi.

Ulu bhugazugwa walwa ahí ibala lwake mpaga bhanindile wize untemi abhubhonje tamu uwalwa wenubho, huna abhanasi wapandike ruhusa lo gubhung’wa uwalwa.

Agabhakoya noi abhanhu umu si yake ahigulya ya gubhung’wa uwalwa bhenubho, kulwa nguno olina hali nhale ya gwimana wei du. Agalala saa nne ja bhujiku ugumisha gokwe mpaga saa tatu nulu saa nne ya dilu. Hangi ofunyaga adhabu nghali noi ulu usanga munhu oseose obhubhonjaga uwalwa bhunubho ya gutulwa manasu makumi abhili na tano, na yingi mingi.

Bhanasi bhagogoha noi, bhadagemile gubhubhonja bho nduhu ruhusa ya ntemi uwalwa bhenubho. Agigela munhu umo uyo agasamila umu si yiniyo gufuma si yingi, uyo aliadalimamile ililagilo linilo lwa ntemi ng’wenuyo.

Agandya gulomelwa na bhanasi abhenyeji amalagilo ga ntemi na mito gakwe ayo agagafunya untemi wabho. Ungeni ng’wenuyo agakumya noi ugubhona hali iniyo ya gubhaluhya abhanasi.

Lushiku lumo walwa bhugazugwa ung’wibala linilo, munhu uyu ngeni oliakajije guja gujugalihya ibala lwake lya gulima, agaja uku walwa ubhasanga abhanasi, agabhawila, “Bhabehi ninhagi uwalwa nang’we.”

Abhanasi bhagayomba, atali untemi Bayega ugwiza gubhubhonja uwalwa wenubhu. Ungeni agalindila mpaga saa tano, hanuma yaho agahaya, “Ninhagi uwalwa nang’we.” Abhangi bhuyomba, dudizung’winha, kulwa nguno untemi atali ugwiza.

Aho owilwa chene ungeni agalema na gwiyangula ng’winikili, bhasi bhagiyangula gung’winha du kulwa nguno olemaga. Aho ong’wa du ungeni ng’wenuyo, untemi nawe agiza.

Untemi Bayega agaibhona inengelo imo yalidokalile chiza, Untemi agabhuja, “nibhuli inengelo iyi idokalile?” Bhanasi bhagang’wila, “Dandahilaga ngeni du, na ong’waga na ojaga gujutumama nhimo.”

“Nibhuli ng’wang’winhaga?” “Kulwa nguno, agayomba giki agudila guja gujutumama nhimo du.”

Untemi agahaya, “Ng’witanagi wize aha.” Bhajumbe bhabhili bhagaja gujung’witana wiza, untemi umuja, “Nibhuli wiyangulilaga gung’wa walwa aho nadiniza gubhubhonja unene?”

Ungeni agashosha, “Niyangulilaga gung’wa kulwa nguno nagalindila na gubhona giki nagudila guja gujutumama nhimo du.”

Ntemi Bayega aganhadikija gung’wazibu du. Agantula ipe, ungeni nawe aditile ginhu josejose, agatulwa gangi, uwei alidohya du, agatulwa hangi mara yakadatu.

Huna ungeni nawe agiyangula gwikenya. Untemi agatulwa nhang’ha gomumbazu na henaho untemi agiyangula gwikenya gete, agatulwa hangi nhang’ha go muntwe na gugwa hasi, agagwila ung’wibala limo lwa mabala ayo galinamoto.

Ahenaho haho bholibhozugilwa uwalwa; upandika luguma, na gupya moto. Bayega agakindwa na ngeni, na bhutemi bhugasolwa nu ngeni ng’wenuyo.

 Na gutangaja ku bhanasi giki ubhutemi bho Bayega bholi bhuli bhubhi. Ungeni nawe agatula sheria jingi higulwa ya gulindila bhanasi gung’wa walwa. Agabhawila abhanasi giki, makanza ayo naladile gwiza, ili lazima abhanasi bhang’we uwalwa, idi gunilindila.

Kiswahili: Utaliona Lililompiga Ngeo Bayega

Hapo zamani palikuwa na mtu mmoja aliyeitwa Bayega. Huyo alihamia porini mahali pasipo na watu. Baadaye watu wengine walianza kuhamia huko porini wakamkuta anaishi kwa amani.

Akaanza kuwagawia maeneo na kuwapa moyo wa kuishi porini. Hao watu walimshukuru sana huyu Bayega wakampa utemi, akawa mtemi wa mahali hapo. Bayega alifurahi sana kupewa ufalme. Mtemi Bayega alikuwa na maarifa mengi mno. Alitoa amri kwa wananchi kama mtawala.

Pombe ikipikwa katika eneo lake mpaka wamsubili kwanza aje Mtemi aonje kwanza hiyo pombe, ndipo wananchi watakapopata ruhusa ya kuinywa hiyo pombe.

Aliwahangaisha sana watu katika nchi yake juu ya hiyo pombe kuinywa, maana alikuwa na ubinafsi mkubwa sana. Alilala saa nne za usiku kuamka kwake mpaka saa tatu au saa nne za asubuhi. Tena alitoa adhabu kali sana akikuta mtu yeyote ameonja pombe hiyo, atapigwa viboko ishirini na tano n.k.

Wananchi waliogopa sana, hawakuthubutu kuionja pombe bila ruhusa ya Mtemi. Kulitokea mtu mmoja aliyehamia hapo kutoka katika nchi nyingine ambaye hakujua amri za mtemi huyo.

Alianza kusimliwa na wananchi wenyeji amri za mtemi na matendo yake aliyotoa mtemi wao. Mgeni huyo alishangaa sana kuona hali hiyo ya mateso kwa wananchi.

Siku moja pombe ilipikwa katika eneo hilo. Mtu huyo mgeni alikuwa na haraka ya kwenda kupanua eneo lake la kulima, alikwenda kwenye pombe akawakuta wananchi, akawaambia, “Jamani nipeni pombe ninywe.”

Wananchi wakasema bado mtemi Bayega hajaja kuionja hii pombe. Mgeni alisubiri mpaka saa tano, baadaye alisema, “Nipeni pombe ninywe.” Wengine walisema tusimpe. Maana Mtemi bado hajaja.

Baada ya kuambiwa hivyo alikataa na kujiamlia mwenyewe. Basi wakaamua kumpa tu kwa kuwa amekataa. Baada ya kunywa tu yule mgeni, Mtemi naye akaja.

Mtemi Bayega akakiona chungu kimoja hakikujaa sawa sawa, akauliza kwa nini mtungi huu haukujaa? Wananchi wakamwambia, “Tumemchotea mgeni tu, amekunywa na akaenda kufanya kazi.”

Kwa nini mmempa? Kwa sababu alisema kwamba atachelewa kwenda kufanya kazi tu. Mtemi alisema, “Mwiteni aje hapa.” Wajumbe wawili wakaenda kumwita akaja, Mtemi akamuuliza, “ Kwa nini umejiamulia kunywa pombe kabla ya kuionja mimi?” Mgeni akajibu nimeamua kunywa kwa sababu nilisubiri na kuona kwamba nitachelewa kwenda kufanya kazi tu.

Mtemi Bayega akaamuru kumwadhibu tu. Akampiga kofi, mgeni  naye hakufanya jambo lolote, akapigwa tena ananyenyekea tu, akapigwa tena mara ya tatu.

Ndipo mgeni naye akaamua kupigana. Mtemi akapigwa fimbo mbavuni na hapo Mtemi akaamua kupigana sawa sawa. Akapigwa tena fimbo ya kichwani na kuanguka chini.

Akaangukia katika sehemu moja ambayo ilikuwa na moto. Mahali hapo palipopikiwa pombe akapata ngeo na kuungua moto. Bayega akashindwa na mgeni, nao utawala ukachukuliwa na huyo mgeni.

Na kutangaza kwa wananchi kwamba utawala wa Bayega ulikuwa mbaya. Mgeni naye akaweka sheria nyingine kuhusu na mpango wa kusubiri wananchi kunywa pombe. Akawaambia wananchi kwamba wakati nitakapochelewa kuja ni lazima wananchi wanywe, si kunisubiri.

fight

ENGLISH: YOU WILL SEE THE ONE THAT WOUNDED BAYEGA.

In the past, there was a man called Bayega. He decided to live alone in the wilderness where there were no people. Later, some people began to move to the wilderness and found him living in peace.

He began to givepeople some plots to make them live in the wilderness. Those people thanked him so much that they made him chief of that area. Bayega was very happy to be given the kingdom. Chief Bayega had so much wisdom. He started ordering the people as a ruler.

Whenever alcohol was cooked in his area,he was the first to come and taste it.Thereafter, other people were permitted to drink.

He was very concerned about drinking.That was because he was very selfish. He slept at around ten o’clock at night and got up  at around nine orteno’clock in the morning. He also gave the most severe punishment whenever he found anyone who had drunka lcohol before he had tasted it. He could cane that  person twenty-five strokes.

All people were afraid of him.They did not dare to drink alcohol without the permission of the chief. There was a man who had just moved to that place from another country. That man did not know the Chief’s directives.

He was just told by his hosts about the commands of the chief and his various punishments that he gave to the villagers. The newcomer was very surprised to see the state of suffering the people of that place were experiencing.

One day, alcohol had been made in the area. The newcomer was in a hurry going to his farm.He went to the place where alcohol had been made and found the people.He said, “Fellows get me a drink.”

His hosts told him that Chief Bayega has not yet come to taste thealcohol. The new comer waited for five hours.After that long waiting, he said, “Give me a drink.” Others said they should not give him, for the chief had not yet come.

After being told so, he refused and decided forced to be given alcohol. Then the hosts decided to give him just because he had refused to continue waiting. After the newcomer, had just finished drinking, the chief came.

When Chief Bayega saw that one pot was not full, he asked why the pot was not full. The hosts said to him, “We just gave alcohol to the newcomer. He drank and went to work.”

“Why did you give him?”, he asked. “Because he said he would be late to work.” The Chief said, “Bringhim here.” Two delegates went to call him, and the chief asked, “Why have you decided to drink alcohol before I drink?” The newcomer replied, “I have decided to drink because I waited and saw that I would be late  for work.”

Chief Bayega decided to punish him. He slapped him, and the new comer did nothing.He was beaten  again. He still  humbled himself.He was beaten the third time.

Then the newcomer decided to fight. The chief was beaten with a stick on his ribs.The chief decided to continue with the fight. He was struck again witha stick on the head and he fell down.

Unfortunately, the chief fell into fire. As a result the chief got wounded. That means Bayega was defeated by the newcomer.Then seat got taken by the newcomer.

After that, the newcomer made new rules about tasting alcohol. He told the people “If I am late, people should drink.They should not wait for me.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.