88. Jigano Ja Ntemi

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale oliho Ntemi nkumuku noi. Uyo olintongeji o wiza noi na makujo mingi. Aho lwabhita ikanza itale lwa bhutongeji bhokwe, igigela nzala umu si yakwe na lwande lo bhuzenganwa na si yakwe.

Nzala yiniyo igasola ikanza lwa miaka idatu na nusu. Bhanhu bhagayanga na gukoya noi ung’wibala lwakwe, bhangi bhagacha na nzala. Untemi agakoiwa noi na bhanhu, giki adubhakoyakoyelaga abhanhu ku lwande lo nzala na gubhenhela mbula. Ikale yalibhizile untemi lazima weng’nhe mbula.

Bhanhu bhagayomba giki, Untemi ulu adabhingije umu makoye ga nzala na gubhenhela mbula, bhaguntula mpaga ache. Untemi aho wigwa ubhulalamiki bhingi bho bhanhu, agiyangula gutoloka guja ng’wibolu, gugapela makoye mingi umu si yakwe.

Ugonghana agatoroka uja ng’wipolu uko bhanhu bhatiho, ugibhanda mumi milima. Agikala kunuko miaka idatu na nusu. Wikala agulwaga matunda ga ng’wipolu. Mbula igatula aho yabhita miaka idatu na nusu.

Aho otoroka bhanhu bhagapandika noi ijiliwa na bhagayega noi, mpaga bhita npango gogunchola untemi obho, aliyo bhadampandikile gete.

Yubhiza abhanasi umu si yakwe, bhuja ng’wipolu kubhulingi bho ndimu. Bhaginga chalo jinane guja ng’wipolu. Kwikanza lya shigu mpungati, ukwene guhaya, nyuma imo.

Bhagalinga ukunuko kwipolu mpaga lushigu lo gatandatu dilu saa nne. Aho bhashiga ukunima nhihu uko oliwibhisa untemi obho, bhagagunyamanija unima, untemi nanghwe oliwiyanikija mulimi ku nguno ya mbeho.

Itukio la gafula (Nhanga) jigasalambana munima, na abhalingi bhusalambana, mpaga nsumba umo ufuada nhanga na mbwa jakwe ibhili.

Bhogafula umona untemi, wimila, alina hali ya nyahabhi, nzwili jakwe jabhiza ndihu, na hangi obhipa mako na mywenda ya mako noi.

Unsumba ugubhona hali yiniyo agiganika giki obhona ng’wengeleji. Unsumba agapela nhambo noi, agikindika uching’wa linti munda, ubhula bhufuma.

Unsumba agalila na gulija ng’wano. Aho bhigwa abhiye bhagiganika giki odimagwa na shimba.  Nanghwe Untemi agashiga agakumya na guhaya, “Napelaga makoye nu kunu ganipandika hangi.”

Bhagamuja na adamile ugogwita. Bhanhu bhagashiga na gumuja unsumba ng’wenuyu witaga kii? Untemi agahaya, “Nu nene onibhonaga ogoha ku gafula ku nguno ya hali yane umo nalibhizila o mako, nzwili na mpaga mywenda yane yabhipa mako.

Bhanhu bhagamuja, “Ntemi wizaga nanali ukunu?” Untemi ushosha ku bhupina, “Niza kale, nina miaka idatu na nusu.” Bhagamuja hangi, “Wizaga gwita kiyi?” Untemi uhaya, “Nagatoroka aho gigela makoye uko kaya niza gwibhisa kunu mapolu.”

Kiswahili: Hadithi Ya Mtemi (Mfalme)

Hapo zamani kulikuwako na mtemi maarufu sana. Ambaye alikuwa kiongozi safi sana na hekima nyingi. Baada ya muda mrefu wa uongozi wake, ilitokea njaa katika nchi yake na pande za jirani mwa nchi yake.

Njaa hii ilichukua muda wa miaka mitatu na nusu. Watu waliyumba sana katika eneo lake, wengine walikufa na njaa. Mtemi alisumbuliwa sana na watu, kwamba hawashughulikii watu hao kwa upande wa njaa na kuwaletea mvua. Zamani ilikuwa Mtemi lazima awe mleta mvua.

Watu walisema Mtemi asipowashughulikia kwenye tatizo la njaa na kuwaletea mvua, watampiga mpaka kufa. Mtemi aliposikia malalamiko mengi ya watu, aliamua kutoroka kwenda porini, kuyakimbia matatizo mengi katika nchi yake.

Kweli alitoroka akaenda porini kusiko na watu,  akajificha kwenye milima. Alikaa huko miaka mitatu na nusu. Alikuwa  anakula matunda ya porini. Mvua ilinyesha baada ya kupita miaka mitatu na nusu. Alipotoroka watu walipata sana chakula na kufurahi sana, hata wakafanya mpango wa kumtafuta  Mtemi wao na wasimpate kabisa.

Ikawa wananchi katika nchi yake,  walikwenda porini kwa mawindo ya wanyama. Waliondoka vijiji vinane kwenda porini. Kwa muda wa siku saba, yaani wiki moja.

 Waliwinda huko porini hata siku ya Jumamosi asubuhi kama saa nne. Walifika kwenye mlima mrefu, alikojificha Mtemi wao. Waliuzingira mlima, Mtemi naye alikuwa amejianika kwenye jua kwa ajili ya baridi.

Tukio la ghafula (Kanga) walisambaa kwenye mlima, na wawindaji walisambaa, hata kijana mmoja alifuata kanga na mbwa wake wawili. Ghafula akamwona Mtemi, akasimama, akiwa na hali duni, nywele zake zimekuwa ndefu, na tena chafu na nguo chafu sana.

 Kijana kuona hali hiyo alidhani ameona kivuli. Kijana akakimbia mbio sana, akaruka akachomwa mti tumboni na utumbo ukatoka. Kijana akalia na kupiga yowe. Waliposikia wenzake walidhani ameshikwa na Simba.  Na mtemi alifika akashangaa na kusema, “Nimekimbia matatizo na huku yamenikuta tena.”

Wakamwuliza na asijue la kufanya. Watu walifika wakamwuliza huyu kijana amefanya nini? Mtemi  akasema,  “Ni mimi ameniona  ghafula akaogopa kwa sababu ya hali yangu nilivyokuwa mchafu, nywele na hata nguo zangu na hali ya uchafu.

Watu walimwuliza,  “Mtemi umekuja lini huku?”  Mtemi akajibu kwa huzuni,  “Nimekuja zamani, nina miaka mitatu na nusu.” Waliuliza tena, “Umekuja kufanya nini? Mtemi alisema, “Nilitoroka  baada ya kutokea matatizo huko nyumbani na kujificha huku maporini.”

african-chief

ENGLISH: THE STORY OF THE CHIEF.

Once upon a time, there was a very famous chief who was a very good leader with a lot of wisdom. After a long time of his leadership, there was famine outbreak in his country and the surrounding neighbouring countries.

This famine took about three and a half years. People suffered from it very much in that area.Many died of famine. The chief was very troubled by the people.They complained that he did not deal with the people on matters of famine.They looked at him as a person who had failed to bring rain. Formerly, the chief was considered to be the one who brings rain.

The people said that if the chief could not deal with the problem of famine and bring rain, they would kill him. When the chief heard people’s complaints, he decided to escape and went to the wilderness, running away the problems in his country.

He went to settle in the wilderness where there were no people.He hid himself in the mountains. He stayed there for three and a half years. He was eating only wild fruits. Finally, back in the village, it rained heavily. One day, the people of his land went to the wilderness to hunt preys. They passed eight villages and as they moved to the wilderness. They spent seven days on the way.

 They were hunting in the wilderness one Saturday morning at around ten o’clock. They came to a high mountain where their chief himself was hiding. As they hunted, they encircled the mountain.Meanwhile,the chief was enjoying  the sun for it was winter.

All of a sudden,Guinea fowls spread in different parts of the mountain.The hunters also scattered.Among the hunters, a young man was running after guinea fowls. This young man had his two hunting dogs. Suddenly he saw the chief, standing.He was in a poor condition.His hair was long and dirty.The clothes were also dirty.

As the young man saw the situation, he thought he was seeing a shadow. The young man ran very fast, trying to save his life. As he ran,a dry tree branch hit him in the stomach. He was badly injured. In fact, intestines came out. The young man screamed madly. When other hunters heard,they  thought he was being attackedby a lion. As hunters were looking at their fellow hunter who was in agony, the chief also came to the scene. Hewas surprised and he said, “I have run  away from trouble and I now have found it again.”

They asked him not to know what to do. People came and asked what the boy had done? The Chief said, “I think after seeing me, the young man got shocked and started running. The young man may have been frightened by my dirt condition, hair and even my clothes and the general dirty condition in which I am.

The hunters asked him, “When did you come here?” The Chief replied sadly, “I have come a long time ago, I have been here for  three and a half years.” They asked again, “Why did you come here? The Chief said, “I escaped as there wasa problem in the home village which could endanger my life. So, I came to hide myself here in the forest.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.