66. Jigano Ja Nyanda Na Ng’waniki Bhahayaga Kutunga Ndoa

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Kale bhaliho nyanda na ng’waniki, unyanda ilina lyakwe Fanueli, ung’waniki Joyce. Mu bhubhili wabho bhagahaya kutunga ndoa. Aho loshiga ulushiku lwa kutunga ndoa yabho huna lulu fanueli nu Joyce bhakaja ku chumba ja kuzwalila myenda ya bhukombe nabhaje kujutunga ndoa yabho mu kanisa.

Unyanda Fanueli akazwala sulubhale jakwe ja wikole. Sulubhale igwanda igodi, malole ku miso, jilatu, na saa ya mumakono umala.

Ung’waniki Joyce nang’hwe wandya kuzwala myenda yakwe ya bhukombe, igauni lyakwe, shela, dhahabu gu matu gakwe, jilatu jisoga, Saa mumakono, udimila na bhulabhu bhusoga gete mumakono gakwe.

Ahikanza bhamala pye abhose bhufuma lulu uguchumba jabho ja kuzwalilila. Bhandya lugendo lwabho lwa kuja ku kanisa bhakatunge ndoa lulu.

Ahabhali mu lugendo umunzila Fanuel akamona munhya wakwe Joyce umo wabhelelaga uyomba giki, “Yee!! Munhya wane Joyce wabhelelaga gete, idabhelelile usimize wa magulu, imaga henaha unene naje bomani nagaguchobhele loli na gugushokela nize nagusole.”

Joyce uzunya, Nahene nsumbone ugunisanga henaha nadinga gete. Fanueli uja bomani gujuchola imondoka umo wahayilaga.

Huna lulu ikanza lya kwinga u Fanueli u Joyce usangwa iguku. Inguku yeniyo aho yampandika Joyce yuyomba, “Yee!! Ng’waniki bhebhe wabhelelaga cheniki. Aliyo umanile igiki wabhelelaga?” Ujoyce uyomba, “nduhu natimanaga igiki nabhelelaga, iki nadibhonaga.”

Inguku yung’wila Joyce, “Ulu ulihaya kumana ng’hana igiki wabhelelaga ninhage imyenda yako pye iyose wibhonanikije bhebhe ng’wenekili igiki wabhelelaga ng’hana.

Joyce aho wigwa chene agikungula bho wangu wangu imyenda yakwe pye yose. Akasaga aliduhu, akalinha iliguku pye myenda yakwe. Inguku yuyizwala pye myenda ya ng’wa joyce, inguku aho yazwala myenda yumuja, “wabhona lulu umo nabhelelela?” Joyce uhaya, “ng’hana yi obhelela.” Inguku yandya kwigeta nyadoshi gete.

Huna lulu Fanuel aho wipandika imondoka akayega no, alimana giki umunhya wakwe akwenhwa na mondoka ni haha yeniyi gashinaga Nguku. Fanuel agang’winha udeleva lilagilo limo duhu, ung’wila, “jaga lulu bhitilaga ibalabala linili duhu ugunsanga ng’waniki azwalile myenda yape nu ng’unuyo duhu, nduhu ungi ho. Deleva ubhacha gali.

Kiswahili: Hadithi Ya Mvulana Na Msichana Waliotaka Kufunga Ndoa

Hapo kale, palikuwepo vijana wawili, mvulana na msichana. Mvulana aliitwa Fanuel, na msichana aliitwa Joyce. Vijana hao walikubaliana kufunga ndoa.

Siku ya kufunga ndoa yao ilifika, walikwenda kwenye chumba cha kuvalia mavazi ya harusi. Fanuel alivaa suti iliyomkaa vizuri. Pia alivaa miwani, saa ya mkono na kofia.

Naye Joyce alivaa mavazi yake. Shela aliyoivaa ilimpendeza sana, heleni na vidani vya dhahabu vyote vilimfanya apendeze sana. Mikononi alishika maua mazuri.

Baada ya kumaliza kuvaa, wote wawili walitoka nje, wakaanza safari ya kwenda kufunga ndoa Kanisani. Wakati walipokuwa wanakwenda  Kanisani, Fanuel alivutiwa sana na mwendo wa madaha wa mchumba wake. Akasema, “Naam, Mpenzi Joyce, umependeza kweli kweli, haifai sasa utembee kwa miguu, simama hapa hapa, nami niende mjini kukutafutia gari, halafu nitakuja kukuchukua.” Joyce akasema, “sawa mchumba wangu, mimi utanikuta hapa hapa tu sitaondoka kamwe.” Fanuel akaenda mjini kutafuta gari kama alivyosema.

Basi baada ya Fanuel kuondoka, Nyani alikuja alipo Joyce. Nyani huyo alipofikia kwa Joyce akasema, “lo, asi!! Binti umependeza kweli kweli. Lakini je, unafahamu kuwa umependezaje? Joyce  akasema, “mhuu, sifahamu vizuri kwa kweli, maana sijioni sawa sawa.”

Nyani akamwambia Joyce, “Kama unataka kuhakikisha kuwa umependeza, nipe sasa mavazi yako yote nijivalie ili ujionee mwenyewe kuwa kweli umependeza.  Joyce kusikia vile, akavua kwa haraka sana mavazi yake yote, akabaki bila nguo, akampa Nyani mavazi yake yote.

Naye Nyani alijivalia mavazi yote ya Joyce. Baada ya Nyani kujivalia mavazi akasema, “umeona sasa jinsi nilivyopendeza?”  Joyce akasema, “asi!! Safi kweli, Nyani anajirembua kwa madaha kweli kweli.”

Fanuel alipoipata gari alifurahi mno, akijua kuwa mchumba wake ataletwa kwa gari mara  Kumbe Nyani. Fanuel alimpa dreva sharti moja tu, alisema, “nenda sasa, pitia barabara hili tu utamkuta msichana mwenye mavazi meupe, ni huyo huyo tu, umchukue siyo mtu mwingine.” Dreva akawasha gari tayari kwenda kumchukua Joyce.

Gari alipoliona Joyce kuwa tayari linakuja kumchukua limepambwa kwa matawi na maua safi, lo! Ikawa mkiki mkiki sasa kwa Joyce. Joyce anadai sasa mavazi yake kwa Nyani, “Nipe bwana mavazi yangu nivae mimi, gari limefika  ni hilo.”  Lo! Wapi, Nyani anajidai vizuri mno kwa kuwa amependeza, hajali ombi la mwenye mavazi ya arusi.

Dreva akafika vuu! Tayari kumchukua mwenye mavazi meupe. Nyani akaitwa kuingia ndani ya gari bila Joyce. Joyce kuona vile, akamwambia dreva,  “Ni mimi hapa siyo huyo.”  Dreva akasema, “Mimi nimeambiwa nimchukua mtu mwenye mavazi meupe tu na sio wewe.”

Joyce akaachwa pale pale analia ovyo. Fanuel alipomwona Nyani amejivalia mavazi ya arusi, bila Joyce mchumba wake, alikasirika sana, akamvua mavazi ya arusi. Akagoma kufunga ndoa na Joyce, akarudi nyumbani. Arusi haikufungwa.

boy-and bride

English: The Story Of A Boy And A Girl Who Wanted To Marry Each Other

monkey-3

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.