63. Nzala Ya Kundami

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale igiza nzala yitanagwa ya kundami. Nzala iyi igamala myaka idatu na nusu. Bhanhu bhagashila no, pye bhuli ndimu jashilaga. Bhanhu bhagahabhiha, abhangi bhagalekelelwa ng’holo duhu.

Waliho Ntemi witanagwa Ng’wana Nkuba osengelema. Ng’wana Nkuba wali na jisa jitale no uko bhanhu. Lushiku lumo agiza ngikulu ojinilamba gufuma Singida, ilina lyakwe wali Kabula, mbula nulu Kudema. Amina genaya alina giki ngemi wa mbula.

Ngikulu ng’wenuyo agazunilijiwa nu Ntemi kwigasha ho gupila nzala. Ngikulu ng’wene wali ngemi wa mbula. Aho wegela ugushiga ing’wa Ntemi ujibhisa ijibhiga gasegeno hado, kiya mdusaga. Ngikulu uhaya giki, “Aliyo Ntemi aliho na ng’wichane inuma nanekaga mdusaga, bihi fai.

Ngikulu ng’wene agayudima ng’holo ja Ntemi. Wadimilaga nuko wabhisila ijibhiga jakwe. Wasosejaga ijibhiga yatula mbula gabala gadoo nako kagadimilaga, ulu yatula imbula japandika bhung’welo wa minzi ing’holo jene.

Gagabhita makanza maguhi nulu shigu mpungati giki gunilila mafa kabala gadoo nako kagadimilaga duhu. Mshiku jene ng’ehu ing’holo jugaluka nu loya.

Ng’wana Nkuba ubhuja, “Hali mayu ugang’wisijaga he?” Ngikulu uhaya, “Hii! Nagang’wisijaga bho gukoya no niyo.” “Hali bhuli nadagubhonaga uko mongo?” Kaliho kalambo guko nagadimilaga.

Ng’wana Nkuba untuma munhu gugakungila bhagabhone nuko kagang’wishijaga. Ng’wambilija umo uwilwa agafade lushiku lumo nulu gachilula duhu.

Aho kachilula ubhuka nang’hwe agafadile, oja bho kwibhanda bhanda mpaga nuko kagadimilaga. Aho kegela jupela nhambo ing’holo jijile aho kabala gene.

Ng’wambilija aho oshiga ho ubhona mafa madoto, wibhanda bihi haho. Aho gashiga makanza ga gung’wisha kuja aho jibhiga gugajisoseja mbula yandya gutula, alolile duhu. Ng’holo jung’wa aminzi mpaga jutosha. Igantula pye nu ng’wei haho ibhandile.

Ng’wambilija ubhuka ajile kaya uganomela untemi. Aho ong’wila untemi ukumya no, iki chu giki gafumaga he amafa amadoto? Na gwene jigwibyalaga ing’holo jane gashi jigulyaga jashisha.

Ngikulu ng’wene utuja. Ng’wana Nkuba ubhuja, “hali mayu uli na mbula uko ugadimilaga,” Ngikulu ulema, “Nduhui unene imbula.” Ng’wana Nkuba umana kaduyomba, ugagulila ng`wenda gopi giki gadimi noi. “Jaga lulu mayu ugang’wenhe nu ng’wiyo ize kaya, obhipilile no uko masaga.”

Ngikulu uzunya nahene, kuja kugajenha ijibhiga jene mpaga hakaya. Ijibhiga nulu imbula yene yitanagwa, kabula, mbula, nulu kudema. Ng’wana Nkuba nang’hwe wandya gulangwa akabhegeje gahajibhiga, mpaga umana gete.

Ngikulu ng’wene usada ugaya, mbula yene yubhiza ya ng’wana nkuba. Ng’wana nkuba agakumuka mabala matale no na gupandika ilumbi litale no uko bhanhu.

Swahili: Njaa Ya Kundami

Hapo kale ilitokea njaa iitwayo ya kundami. Njaa hiyo ilichukua miaka mitatu na nusu. Watu walikwisha sana, na hata wanyama wa porini walikwisha. Watu walikuwa maskini, wengine walibaki na kondoo tu.

Alikuwepo Mtemi  aliyeitwa Ng’wana Nkuba wa Sengelema. Alikuwa na huruma kubwa sana kwa watu. Siku moja alikuja bibi kizee wa kinyilamba kutoka Singida, jina lake lilikuwa Kabula, mvua au kujaribu mvua. Majina hayo yalimaanisha mtu wa kujaribu kuleta mvua.

Bibi kizee huyo alikubaliwa na Mtemi kukaa hapo kwa ajili ya kupona njaa. Kwa vile alikuwa mtu wa kujaribu kuleta mvua, alipokaribia kufika kwa Mtemi, alificha kijungu mbali kidogo, mashariki kwenye vichaka. Bibi kizee alisema, “Lakini Mtemi yupo na mwenzangu nyuma nimemwacha kwenye vichaka, karibu kidogo.

Bibi kizee huyo alianza kuchunga kondoo wa Mtemi. Alikuwa akichungia kule alikofichia kile kijungu chake. Alikuwa akichochea moto mvua inanyesha kwenye sehemu ndogo aliyochungia. Iliponyesha mvua kondoo wanapata sehemu ya kunywea maji.

Ulipita muda mfupi kama siku saba hivi, sehemu hiyo majani yakawa ya kijani kwenye kisehemu kicho kidogo alichokuwa akichungia. Katika siku chache, kondoo wakawa na afya njema.

Ng’wana Nkuba aliuliza, “Hivi mama unanyweshea wapi?” Bibi kizee alisema, “Hii! Nanyweshea kwa kuhangaika mno lakini.” Mtemi akauliza, “Kwa nini sikuoni mtoni?” Bibi kizee, alijibu, “Kuna kadimbwi huko ninakochungia.”

Ng’wana Nkuba alimtuma mtu kwenda kunyemelea ili akaone huko anakonyweshea yule bibi kizee. Msaidizi mmoja aliambiwa amfuate bibi yule kuanzia pale anapotoa wale kondoo kwenda kuchunga.

Alipotoa mifugo nje naye akaanza safari ya kumfuata.  Alienda kwa kujificha ficha mpaka kule anakochungia. Alipokaribia kondoo walikimbia mbio kwenda kwenye sehemu hiyo.

Yule msaidizi alipofika hapo akaona nyasi mbichi, akajificha karibu. Ulipofika muda wa kunywesha yule Bibi alienda kuchochea kwenye kijungu hicho, mara mvua ikaanza kunyesha, naye akiwa anaona tu. Kondoo walikunywa maji mpaka kutosha. Ile mvua ilimnyeshea hata yeyé pale alipokuwa amejificha.

Yule msaidizi alianza safari kwenda nyumbani akamsilimlia Mtemi. Alipomwambia Mtemi alishangaa mno. Kiangazi hiki majani mabichi yametoka wapi? Ndiyo maana kondoo wangu huzaliana kumbe huwa wanakula mpaka wanashiba.

Yule Bibi kizee akawapeleka kondoo nyumbani. Ng’wana Nkuba, aliuliza, “hivi mama una mvua huko unakochungia?” Bibi kizee alikataa, “Mimi sina mvua.”  Ng’wana Nkuba, akafahamu kuwa hatasema, akamnunulia nguo nyeusi kwa vile ni mchungaji sana. “Nenda basi mama ukamlete na mwenzio aje nyumbani, amechakaa mno huko maporini.”

Bibi alikubali, ‘sawa’, kakaenda kukichukua kile kijungu mpaka nyumbani. Kijungu au mvua yenyewe iliitwa, kamvua, au “kudema” kujaribu.  Ng’wana Nkuba naye alianza kufundishwa namna ya kutengeneza hapo kwenye kijungu mpaka akaelewa kabisa.

Yule Bibi kizee aliugua akafariki, mvua hiyo ikawa ya Ng’wana Nkuba.  Ng’wana Nkuba alisifika kwenye sehemu kubwa na kupewe shukrani mno kutoka kwa watu.

English: The Famine Of Kundami

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.