64. Mbita Hagati Itagayaga – Shimba Na Negele

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Shimba na Negele bhali bhunwani gete. Bhalibhazengile bhuli ng’wene ha ng’wakwe. Wali bhuzenganwa wa kasegeno hado. Shimba yajaga kuhwima, ulu yakabhulaga ndimu yenha nyama ha kaya wang’witana nsumba ng’wiye, “Negele, nzugu ng’wana wa mayu tulye nyama,” Waja bhakalya. Na Negele nayo yajaga kusumila bhuki, yenha ha kaya wang’witana nsumba ng’wiye, “Nzugu bhageshi tung’we bhuki nenha,” nayo yaja bhakang’wa. Bhakikala bhusumba wa shiku ningi.

Ja lushiku lumo Sayayi ubhasanga bhalilomela, huna lulu Sayayi akabhabhuja mhayo, ubhabhuja giki, “Aliyo ng’witogilwe no,” Nabho bhuhaya, “Ng’hana.”

Sayayi ubhawila giki, “Mbita hagati itagayaga (nulu itakilanhyiagwa) mulikenya duhu, nulu bhusumba wing’we bhulacha.” Bhulema bhuhaya, “Bhutalacha.”

Sayayi ubhaleka umola ajile kaya. (Wamolaga kuja kaya) gashinaga ugabheja isala lya gubhabhulagija bhusumba wabho. Wahayugashoka ku lushiku lungi ukashikila hagati ya bhuzenganwa wabho, atashikile ha ng’wa Shimba nulu ha Negele, hagati wibhanda.

Kitumo kali akajile kabho, muna Shimba wali waja kuhwima, nu muna negele kujusumila bhuki. Shimba ikanguha kushoka kufuma kuhwima.

Sayayi wamalaga kwibhanda hagati ya bhuzenganwa wabho. Shimba wahayushika ha kaya ung’witana nsumba ng’wiye, “Negele, nzugu ng’wana wa mayu nenha nyama tulye.” Sayayi nang’hwe wigemeja kiti Negele ulema, “ii amanyama gako ganinogije galyage bhebhe ng’wenikili natizaga unene.

Kakanza katakulile muna Negele ushoka nang’hwe. Kitumo kali kajile kabho, ung’witana nsumba ng’wiye, “Bhageshi nzugu lulu nenha bhuki tung’we.”

Sayayi wigemeja kiti Shimba ushosha “Namalaga kukwitana walemaga kwidika, ng’waga mabhuki gako natizaga ko unene.”

Henaho aho Sayayi wabhona wabhabhulagija ubhusumba wabho utoloka uja kaya. Bhusumba wa Negele na Shimba bhucha.

Kiswahili: Ipitayo katikati huwa haikosekani – Simba Na Nunda.

Simba na Nunda walikuwa marafiki sana. Walikuwa wakiishi kila mmoja kwake, ingawa hapakuwa mbali sana. Kila mara Simba alikuwa anakwenda kuleta nyama nyumbani kwake.

Halafu humwita rafiki yake, Nunda. “Njoo, mtoto wa mama, tule kwani nimeleta nyama. Nunda akija, wanakula ile nyama. Naye Nunda alikwenda mwituni kurina asali.

Akisha pakua asali hiyo huileta nyumbani kwake, naye humwita rafiki yake,  Simba  “Njoo rafiki yangu turambe asali niliyoileta.”  Simba huja na wote wawili huramba asali. Waliishi kwa urafiki wa namna  hiyo kwa siku nyingi.

Siku moja, alitokea Sungura na akawakuta marafiki hao kwenye mazungumzo yao. Basi, Sungura aliwauliza, “Mbona mnapendana  hivyo?” Wao wakamkubalia, “Sisi ni  marafiki wakubwa sana!” Sungura akawaambia, “Katika urafiki wa aina hii, kipingamizi hakitakosekana. Ipo siku, mtakuja kukosana, hata urafiki wenu utavunjika tu.”

Lakini wao walimkatalia na kusema, “Hautavunjika kamwe!” Sungura aliwaacha akarudi nyumbani kwakwe. Kumbe yule Sungura alikuwa mwerevu wa kuvuruga urafiki wao. Siku nyingine,  Sungura alifunga safari na kukomea katikati ya makazi ya marafiki hao wawili na akajificha.

Kama ilivyo kawaida yao, Simba alikwenda kuwinda na Nunda alikwenda kupakua asali. Simba aliwahi kurudi kutoka kwenye mawindo yake.

Alimwita rafiki yake Nunda, “Njoo mwana wa mama, nimeleta nyama uje tule.”  Naye Sungura alijifanya kuwa ndiye Nunda akamjibu Simba kwa dharau, Simba, “Hapana, manyama yako hayo yamenichosha, kula wewe mwenyewe. Mimi siji.”

Ukapita muda mfupi, naye Nunda akafika, akamwita rafiki yake Simba, “Rafiki, sasa nimeleta asali, njoo tunywe.”

Sungura  akajifanya kuwa ni Simba akajibu, “Mbona mimi nilipokuita, ulikataa kuitika. Kunywa mwenyewe maasali yako. Mimi siji!”

Sungura alipoona amefaulu kuusambaratisha urafiki wao, akatoroka na kwenda masikani kwake. Urafiki kati ya Simba na Nunda ukavunjika kabisa.

the-rabbit-the-lions

English: The Middle Passer Cannot Be Absent- Lion And  badger (Animal Drinketh Honey).

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.