57. Mhuli Itabhunagwa Nkondo Gwayo

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho ngosha umo walatolile, ubyala bhana bhagosha bhike ikumi na bhabhili. Huna lulu nkima kubhazugila bhana bhingi cheniki wapandikaga makoye.

Makoye kizilaga hikubhi, lyanguhaga kushila. Bhandya lulu bhana kuiimba (kutaya) nduhu ukwiguta. Likubhi lya shilaga mayu. Twamalaga ikubhi. Ngikulu ubhashogeja, “Twite ki lulu?”

Huna lushiku lumo kizaho kageni. Ngeni umuja, “Bhanhu bhako bhakumanaga bhulomba (bhutaya) ikubhi bhuli?” Uhaya, Nite kinehe?” Mhuli itabhunagwa nkondo gwayo nakwiyumilija duhu.

Natigelile kuleka kubhazugila.” Ngeni ung’wila giki, ulu ulitogwa bhana bhako bhoye kumana bhulomba makubhi, nakulange isala. Ulu wazuga ikubhi, watula fugo, walileka ikubhi lingi hishiga likale lilipogoma, kushiga kubisha bhugali moto kwikale gulibhaka ho. Gemaga nzila yeniyo hamo ikukwambilija.”

Aho wabhatwalila bhugali, ikubhi lyali isebu. Aho bhandya kulya lulu, ulu wagema kulija ikubhi lingi wapya waduma kulija ikubhi lingi. Bhose bhita chene, nabhuduma kwinja ikubhi lingi. Bhuyinenela (kwinja kakubhi kado kado. Nose bhugali bhushila ikubhi litali lilimo mu nungu.

Ngeni ung’wila, wabhona isala lyenilo tumamilaga giko shiku jose. Iki mhuli itabhunagwa nkondo gwayo. Utudula kubhapeja bhana iki kugayiwa ikubhi iyumilijage duhu.

Kiswahili: Tembo Hazidiwi Na Mkonga Wake

Hapo kale aliishi mwanamume mmoja ambaye alikuwa ameoa. Walibahatika kuwa na watoto wa kiume kumi na wawili. Kwa hiyo, mama alipata shida sana kuwapikia chakula watoto wengi hivi. Shida kubwa ilikuwa kuhusu upatikanaji wa mboga. Daima mboga katika familia hiyo ilimalizika haraka  haraka.

Watoto wale wakianza kulalamika, ulikuwa ni wimbo wao wa kila siku, “Mboga imekwisha mama! Tumemaliza mboga mama!”

“Sasa nifanye nini wanangu?”

Siku moja alifika mgeni. Mgeni yule akamuuliza yule mama.

“Kwa nini watoto wako kila siku wanalalamika kuwa hawana mboga?”

“Sasa nifanyeje?  Tembo huwa hazidiwi na mkonga wake. (Tembo hashindwi na mkonga wake). Nitajitahidi  tu kuwapikia, kamwe sitaacha.”

Mgeni akamwambia,  “Iwapo unapenda watoto wako waache tabia ya kuomba mboga, nitakufundisha mbinu.”

“Mbinu gani?” Mama aliuza.

Mgeni akajibu, “Unapopika mboga na kuiweka kando ili kupika ugali, uwe unaiacha mboga nyingi figani.  Ikae pale ikichemka hadi unapokuwa umesonga ugali. Moto uwe pale ukiendelea kuwaka.

Alipowapelekea ugali mboga ilikuwa bado ina moto. Na yeyote atakayeanza kuchota mboga nyingi, itamchoma na kumwunguza kooni. Mazoea yana taabu.

Siku hiyo, mama yao akawaandalia mboga kama alivyoelekezwa na yule mgeni. Wote wakanawa. Basi, wakawa wanachota mboga kidogo kidogo na hawakuathirika.

Mwishowe ugali ukaisha na huku mboga ikawa bado chunguni. Mgeni akamwambia yule mama, “Umeiona akili hiyo? Fanya hivyo kila siku.”

“Sawa kabisa! Kwa vile Tembo hazidiwi na mkonga wake. Huwezi kuwafukuza watoto kwa kuwa umekosa mboga. Vumilia tu.”

English: An Elephant is not overwhelmed by His/Her Trunker

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s