55. Jigano Ja Ng’wa bahati

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho nkima uyo walina ng’wana umo. Lushiku lumo ng’wana ng’wenuyo akamisha nsati. Nina akanaja ng’wana mu kaya, uja kujukobha bhugota halinzenganwa.

Guko atali kwinhwa bhugota, wahayimanila ubhona numba yakwe ilibhaka moto. Nkima ng’wenuyo upela wangu wangu kuja ko. Aho washika wingila mu kaya na kunsomba ng’wana wakwe. Umandila ha shikubha atizupya moto. Aliyo unina upya pye umili, wita malonda kufumila ku magulu kushika kuntwe.

Aho wapila usaga na malanda mili pye. Ihanga lyakwe lyubhipa no. Ng’wana ng’wenuyo witanagwa Bahati. Aho wakula uyuja kujigusha na bhana bhiye, bhalinseka na bhaling’wila giki, “Limayu lyako libhi no, lilini hanga litilyawiza. Utubhonaga bhamayu bhise umo bhali bhusheku.

Bahati aho wawilwa chene, wandya kundalaha unina. Lushigu lumo akamuja unina, “Iki bhuli mayu uti ni hanga lya wiza? Bhuli mili gwako guli na malanda pye? Kufumila kuntwe kushika kumagulu?” Nina akansombolela umo yali, “Ng’wana wane aho utali ndo, numba ikapya moto. Nu bhebhe walulalile mumo, nakingila mukaya kukusola nukubhandila ha shikubha utizupya moto. Hi chene ulinibhona nalina malanda pye umili. Iki bhebhe nakutogilwe.”

Bahati aho wigwa giko akayegano, akamana giki, mayu wane wa ng’hana. Uyubhawila na bhiye, “Lolagi mayu umo anitogelilwe, abhakilile na bhamayu bhing’we.” Kufumila lushiku lwene, walatalekaga kunumbilija nina. Na akanela chiza no umu bhugikulu wakwe.

 Kiswahili: Hadithi Ya Mtoto Bahati

Alikuwepo mama mmoja, aliyekuwa na mtoto mmoja. Siku moja mtoto huyo aliamka mgonjwa. Mama alimlaza mtoto ndani ya nyumba. Alikwenda kutafuta dawa kwa jirani, kabla hajapewa dawa alishitukia akaona nyumba yake inawaka moto.

Mwanamke huyo akakimbia haraka haraka kwenda huko. Alipofika akaingia ndani na kumchukua mtoto wake. Alimkumbatia kifuani ili asiungue na moto.

Lakini mama yake aliungua mwili wote, alipata madonda kutoka miguuni hadi kichwani. Alipopona akabaki na makovu mwili wote. Sura yake ikaharibika mno.

Mtoto huyo alikuwa anaitwa Bahati. Alipokua alikuwa anakwenda kucheza na watoto wenzake. Huku wakimcheka na kumwambia kwamba, “Mama yako ni mbaya mno, ana sura isiyo nzuri, huwaoni mama zetu walivyo laini.”  Bahati alivyoambiwa hivyo, akaanza kumdharau mama yake.

Siku moja akamwuliza mama yake, “Kwa nini  mama huna sura nzuri? Kwa nini mwili wako una makovu wote? Kutoka kichwani hadi miguuni?”  Mama yake alimweleza jinsi ilivyokuwa. “Mtoto wangu ulipokuwa bado mdogo, nyumba iliungua moto, na wewe ulikuwa umelala humo. Niliingia ndani nikakuchukua nikakukumbatia kifuani. Ndivyo unavyoniona kuwa nina makovu mwili wote. Kwa kuwa wewe ninakupenda mno.”

Bahati aliposikia hivyo alifurahi mno akajua hivi, Mama yangu ni wa kweli akawa anawaambia na wenzake, “Angalieni  Mama anavyonipenda, anawazidi hata mama zenu.”  Tokea siku hiyo  alikuwa haachi kumshukuru mama yake.  Na alimlea vizuri mno katika uzee wake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.