Author: Sukuma legacy

970. HENAHO HASONGOMAJI.

Isongomaji li lipande ilo lililyagukamaaja. Ilihoyi ndimu imo iyo ikolile na nzob’e. Indimu yiniyo, ulu yubhona ginhu igajilolelaga mpaga jugajimila kunguno ya gujikamalila bhuli jene ijo ili jibhona. Hungwene aho yabhonelaga igahayigwa giki, “henaho hasongomaji.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajimijaga ikanza lyakwe bho gukamala bhuli hene aho bhanhu bhakwilaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajaga aho bhisumbijaga abhanhu agilolela bhuli jene ijo jilitiwa hoyi, mpaka okeleja ugutumama imilimo yakwe kunguno ya bhukamazu bhokwe bhunubho. Uweyi agapandikaga makoye gagugayiwa ijiliwa aha kaya yakwe, kunguno ya kulijimija ilikanza lyakwe ilya kutumama milimo bho gukamalila ginhu ija nduhu solobho yoseyose, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ndimu iyo igajimijaga likanza lyayo bho gukamalila bhuli jene ijo ili jibhona, kunguno nuweyi agalijimijaga ili ilikanza lyakwe bho gukamalila ginhu ijo jidina solobho, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “henaho hasongomaji.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gutumila ikanza lyabho bho gutumama milimo na guleka gukamalila mihayo iyo idina solobho ubhubhoyi, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Kumbukumbu 30:15-20.

KISWAHILI: MAHALI HAPA PANASTAAJABISHA.

Mahali pa kustaajabhisha ni sehemu yile inayoshangaza watazamaji wake. Kuna mnyama poli anyefanana na punda. Mnyama huyo, akiona kitu hukiangalia kokote kiendako mpaga kinapotea kwa sababu ya mshangao wake huo. Ndiyo maana pale alipoangalia huitwa, “mahali hapa panastaajabisha.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huupoteza muda wake kwa kushangaa kila sehemu wanapokusanyika watu, katika maisha yake. Mtu huyo, huenda pale wanapokusanyikia watu hao na kuangalia kile kilichopo pale mpaka anachelewa kuyatekeleza majukumu yake, kwa sababu ya kushangaa kwake huko. Yeye hupata matatizo ya kukosa chakula katika familia yake kwa sababu ya kuupoteza bure muda wake huo wa kufanya kazi, kwa kushangalia vitu visivyo kuwa na faida, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mnyama anayepoteza muda wake kwa kungalia kila kitu anachokiona, kwa sababu naye hupoteza muda wake kwa kushangaa kitu kisicho na faida, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “mahali hapa panastaajabisha.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutumia muda wao kwa kufanya kazi badala ya kushangaa vitu visicho na faida kwao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Kumbukumbu 30:15-20.

africa-1211

mustard-

ENGLISH: THIS IS A WONDERFUL PLACE.

A place of wonder is the part that amazes its viewers. There is an animal that looks like a donkey. This animal continues looking at what it sees to the point of disappearing because of its surprise. That is why the place resembles to it people call it that, “this is a wonderful place.”

This saying is likened to a man who wastes his time by marveling at every place where people gather in his life. This man goes to where the people are gathering and looks at what is there until he is late in carrying out his duties, because of his wondering at whatever he sees. He suffers from famine in his family because of wasting his free time of working by cheering for worthless things instead of working seriously in his family.

This man resembles the creature that wastes its time by looking at everything which it sees, because he also wastes his time by marveling at something useless which sees in his life, instead of using his time for working. That is why he says that, “This is a wonderful place.”

This saying imparts in people an idea on how to spend their time by working seriously instead of wondering about things that are not useful for them, so that they can have more success in their lives.

Deuteronomy 30: 15-20.

festival-

969. KALAGU – KIZE. AMASUMBI PYE AGOSE GAGIGASIJIYAGWA LELO LILIHO LIMO LIDIGASIJIYAGWA – LIMOTO.

Ikalagu yiniyo, ilolile bhukali bho moto. Ilimoto linilo lilijitumamilo ilo lidigasijiyagwa kunguno ligikalaga liseb’u noyi. Uyo ugema uguligasija agupya noyi. Ilyoyi liliheke na masumbi pye agose ayo gagigasijiyagwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “amasumbi pye agose gagigasijiyagwa lelo liliho limo lidigasijiyagwa – limoto.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali nkali gubhilitija, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adakumiyagwa na oseose umubhutumami bho milimo yakwe, kunguno ya bhukali bhokwe bhunubho. Uweyi agabhogohyagwa abhanhu abho agikalaga nabho, kunguno ya kugumana ubhakalihila sagala duhu, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikikolaga nili moto ilikali ilo lidigasijiyagwa, kunguno nuweyi alinkali uyo adakumiyagwa umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “amasumbi pye agose gagigasijiyagwa lelo liliho limo lidigasijiyagwa – limoto.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kuleka gubhiza na bhukali bho gubhitilija umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala na bhanhu chiza, bho nduhu ugubhogohya sagala abhichabho bhenabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 10:26-31.

Luka 12:2-7.

KISWAHILI: KITENDAWI – TEGA.

VITI VYOTE HUKALIWA LAKINI KIPO KIMOJA KISICHOKALIWA – MOTO.

Kitendawili hicho, huangalia ukali wa moto. Moto huo, ni kitendea kazi kisichokaliwa kwa sababu ya kuunguza kwake. Yule ajaribuye kuukalia moto huo humuunguza sana. Wenyewe uko tofauti na viti vyote vikaliwavyo, kwa sababu ya ukali wake huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “viti vyote hukaliwa lakini kipo kimoja kisichokaliwa – moto.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkali wa kupitiliza, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa haguswi na yeyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Yeye huwaogofya sana watu anaoishi nao, kwa sababu ya kuendelea kwake kuwakalipia hovyo watu wake hao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule moto mkali usiokaliwa, kwa sababu naye huwa mkali kupita kiasi anayewakalipia watu wake hovyo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “viti vyote hukaliwa lakini kipo kimoja kisichokaliwa – moto.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwa na ukali wa kuwakalipia hovyo watu wao, katika maisha yao, ili waweze kuishi nao vizuri bila ya kuwaogofya, maishani mwao.

Mathayo 10:26-31.

Luka 12:2-7.

blaze-

fire-1

charcoal-

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

ALL CHAIRS ARE USED TO SIT IN EXCEPT ONE WHICH IS NEVER USED TO SIT IN – FIRE.

The above riddle looks at the intensity of the fire. It is an uninhabited instrument because of its burning situation. The one who tries to sit in it ablaze. It is different from all the seats which people people sit in, because of its severity. That is why people say that, “All chairs are used to sit in except one which is never used to sit in – fire.”

This riddle is equated to the person who is extremely violent in his life. This person is not advised by anyone in fulfilling his or her duties. He/she threatens the people who stay in that family because of his/her harshness.

This person is like a fiery unrelenting fire, because he/she is also a fierce person who treats others harshly in the family. That is why people say to him/her that, “all chairs are used to sit in except one which is never used to sit in – fire.”

This puzzle teaches people about stopping the habit of harshly reprimanding their people, so that they can live harmoniously with them without intimidating anyone of them in their societies.

Matthew 10: 26-31.

Luke 12: 2-7.

 

968. UMUNHU NG’WENUYU ADINIKUJO UKUBHANHU NULU ATINILANGE.

Ilikujo kalikikalile ka gubhitilaga ya wiza abhanhu bho gubhambilija chiza umumakoye gabho. Ilikujo linilo ligang’winhaga widohya bho gutumama milimo chiza uyo alinalyo.

Aliyo lulu uyo adinalyo ilikujo linilo, agashoshiyagwa kubhabyaji bhakwe kugiki aginhiwe bhupya ililange linilo, kunguno adalangilwe nzila ja gwikala chiza na bhanhu. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “umunhu ng’wenuyu adinikujo ukubhanhu nulu adinilange.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli ng’waniki uyo otolwa ugabhadunya nulu ugabhalemela ukubhutolwa bhokwe, [ukubhukwiye]. Umunhu ng’winuyo, agitaga mihayo yabhubhi ukubhiye iyo ilikihamo na gubhadosa, bho gubhabyeda sagala kunguno ya bhugokolo bhokwe ugutumama imilimo, na nhinda jakwe jinijo, umukikilalie kakwe. Uweyi agashoshiwagwa kung’wawe kunguno ya gugayiwa ililange lya gubhakuja abhanhu abho agikalaga nabho bhenabho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo adinikujo nulu ililange ilya gwikala  na abhanhu, kunguno nuweyi adalangilwe ililange linilo ilya gwikala na bhanhu chiza, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “umunhu ng’wunuyu adinikujo ukubhanhu nulu atinilange.”

Akahayile kenako, kalanga bhabyaji higulya ya kubhalanga abhana bhabho ikujo lya gwikala na bhanhu chiza, kugiki bhadule kujibheja chiza, ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Kutoka 20:12.

Mithali 9:10.

KISWAHILI: MTU HUYU HANA HESHIMA KWA WATU WALA HANA MAADILI MEMA.

Heshima ni namna ya kuishi vizuri na watu kwa kuwasaidia bila majivuno. Heshima hiyo, humpatia unyenyekevu wa kuyatekeleza majukumu yakwe vizuri yule aliye nayo.

Lakini yule asiye nayo, hiyo heshima hurudishwa kwa wazazi wake ili akafundishwe upya heshima hiyo, kwa sababu hana maadili hayo mema ya kumwezesha kuishi vizuri watu. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu hana heshima kwa watu wala hana maadili mema.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa msichana yule aliyeolewa akaenda kushindikana kule ukweni kwake. Msichana huyo, hutenda maovu ya kuwadharau watu kwa kuwafanyia kiburi na uvuvi wa kutokufanya kazi, kwa sababu ya kukosa maadili hayo mema kutoka kwa wazizi wake. Yeye hurudishwa nyumbani kwa wazazi wake ili akafundishwa upya, kwa sababu hana maadili hayo mema ya kumwezesha kuishi na watu kwa heshima, maishani mwake.

Msichana huyo hufanana na mtu yule asiyekuwa na heshima wala maadili mema kwa watu, kwa sababu naye huwadharau watu wa ukweni kwake, kutokana na kukosa maadili na heshima hiyo ya kumwezesha kuishi vizuri na watu. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu huyu hana heshima kwa watu wala hana maadili mema.”

Msemo huo, hufundisha wazazi juu ya kuwalea watoto wao kwa kuwapatia maadili mema ya kuwawezesha kuishi vizuri na watu, ili waweze kuzilea na kuziendeleza vizuri, familia zao, maishani mwao.

Kutoka 20:12.

Mithali 9:10.

model-1

ENGLISH: THIS PERSON HAS NO RESPECT FROM PEOPLE AND HAS NO MORALS.

Respect is a way of living well with people by helping them without pride. Such honor, in turn, gives a person humility for carrying out well his duties.

But the one who does not have this honor is returned to his/her parents so that he/she can be re-taught that honor, because he/she does not have the good values ​​which necessary for living well with the people. That is why people say that, “This person has no respect from people and has no morals.”

This saying is likened to a married woman who went on a rampage. This girl, on the other hand, commits atrocities by insulting people, making them proud and idle fishing, because of the lack of good values ​​from her parents. He is sent home to her parents to be re-educated, because of not having those good values ​​for living peacifly with people in his life.

This girl is like the man who has no respect for the people, because she also despises the people who belong to her, due to the lack of morals and respect that will enable her to live well with people. That is why people say to her that, “This person has no respect from people and has no morals.”

This saying teaches parents about raising well their children by giving them good values ​​enough to enable them live well with people, so that they can nurture and develop well, their families, in their lives.

Exodus 20:12.

Proverbs 9:10.

967. UMUNHU NG’WENUYU ADACHAGULILE NULU ADAYANGULAGWA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile Welelo uyo adulile jose. UWelelo ung’wene adachagulaga nulu guyangulwa giki ansole nani, kunguno agamulaga weyi dulu. Uweyi nulu yubhiza nzala agamulaga Weyi duhu igiki mbula yize, kunguno ya bhudula bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhaganyombaga giki, “Umhunhu ng’wenuyu adachagulile nulu adayangulagwa.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo mpaga opandika sabho ja gubhambilija bhanhu bhakwe chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga gutumama milimo yakwe chiza, kunguno alina bhutogwa bho gubhambilija bhanhu bhingi bho gutumila sabho jakwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi ijo agajitumilaga bho gubhagunana abhanhu bhakwe gitumo atogelilwe weyi, kunguno ya bhutogwa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu Welelo uyo alina bhudula bho guyangula yose gitumo atogelilwe, kunguno nuweyi alina bhutogwa bho gujitumila isabho jakwe, bho gubhambilija bhanhu bhakwe gitumo atogelilwe weyi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhaganyilaga giki, “umhunhu ng’wenuyu adachagulile nulu adayangulagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza bhakamu wa kutumama milimo na bhutogwa bho gubhambilija bhichabho bhose abho bhali na makoye, kugiki bhagule kujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Luka 1:35-38.

1Wakorintho 6:14.

Waefeso 2:1, 4-6.

2Wakorintho 5:17-18.

 

KISWAHILI: MTU HUYU HACHAGUI WALA HASHAURIWI.

Methali hiyo, huongelea juu ya Mungu awezaye yote. Mungu Mwenyewe hachagui wala hashauriwi kwamba amchukue nani, kwa sababu yeye huamua lolote atakalo yeye. Yeye hata ikitokea njaa kubwa, Aweza kuamua mvua inyeshe wakati wowote, kwa sababu ya uwezo wake huo mkubwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu hachagui wala hashauriwi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi kwa bidii mpaka anapata mali za kumwezesha kuwasaidia watu wengi, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake vizuri, kwa sababu ana upendo wa kuwasaidia wengi kwa kutumia mali zake. Yeye hupata mali nyingi ambazo huzitumia katika kuwasaidia watu wake hao, kama atakavyo yeye, kwa sababu ya upendo wake huo kwao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Mungu atumiaye uwezo wake atakavyo, kwa sababu naye ana upendo wa kutumia mali zake katika kuwasaidia watu wake wote, kama atakavyo yeye, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu huyu hachagui wala hashauriwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kufanya kazi, wakiwa na upendo wa kuwasaidia wenzao wote, walioko kwenye matatizo, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Luka 1:35-38.

1Wakorintho 6:14.

Waefeso 2:1, 4-6.

2Wakorintho 5:17-18.

 

ethiopia-21

ENGLISH: THIS PERSON DOES NOT HEED TO ADVICE.

This proverb speaks of the almighty God. God Himself does not choose or need an advice from anyone about whom to take, because He decides whatever He wills. Even in the time of a severe famine, He may decide that it will rain at any time, because of His great power. That is why people say that, “This person does not heed to advice.”

This proverb is related to a man who works hard until he finds wealth that will enable him in helping many people in his life. Such person, in turn, strives to do his best, because he loves to help many people by using his resources. He finds numerous treasures that he uses for supporting his people, as he wills, because of his love to them, in life.

This person resembles to God who uses his power for doing good things, because he loves to use his wealth for supporting all his people, as he wills, in his life. That is why people say to him that, “This person does not heed to advice.”

This proverb teaches people about being hard workers enough to have wealth for supporting all their people who are in trouble, so that they can develop well their families in their lives.

Luke 1: 35-38

1 Corinthians 6:14.

Ephesians 2: 1, 4-6.

2 Corinthians 5: 17-18.

966. B’UDIMU B’O LIGEMBE GULINDILA GU NGESE.

Iligembe jili jitumamilo ja gulimila ukuli nimi. Iligembe linilo, ligamanyikaga ubhudamu bholyo ahikanza ilya gulilimila ingese, kunguno ilidimu lidakolokaga. Aliyo lulu, iligembe ilinegu ligakokolokaga nulu wandya duhu unimi ugulilimila ingese yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “b’udimu b’o ligembe gulindila gu ngese.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyitilaga bhukengeji bhutale imilimo na mihayo hayo atali uguyandya nulu uguitumamila, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agitakaga bhukengeji bho kujilola chiza, inhungwa ja bhanhu abho bhali nhomela, kunguno ya gutogwa gubhudebha chiza ubhumhana bho milimo nulu imihayo yiniyo. Uweyi agayombaga mihayo ya nhana na kupatandika matwajo mingi umumilimo yakwe, kunguno ya gutumama milimo iyo wiyitilaga bhukengeji bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ligembe ili ligikalaga na bhudamu ahikanza ilya gulilimila ingese, kunguno nuweyi agapandikaga matwajo mingi umumilimo yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhakwe inzila ja guyidebha chiza imilimo yabho, haho bhatali uguyandya uguitumama. Hunagwene agabhawilaga giki, “b’udimu b’o ligembe gulindila gu ngese.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guyitila bhukengeji bhutale imilimo yabho haho bhatali uguyandya uguyitumama, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhobho.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 12:33-37.

KISWAHILLI: UGUMU WA JEMBE KUSUBIRI KWENYE PALIZI.

Jembe ni kitendea kazi cha kulimia kwa mkulima. Jembe hilo, hujulikana ugumu wake wa kulilimia wakati huo wa kulifanyia kazi, kwa sababu lile lililo gumu huwa halikongoloki. Lakini lile lililolegea hukongoloka pale mkulima anapoanza tu kulilimia. Ndiyo maana watu husema kwamba, “ugumu wa jembe kusubiri kwenye palizi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzifanyia utafiti mkubwa kazi zote kabla hajaanza kuzifanya, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya utafiti wa kufahamu tabia za wale anaoongea nao kabla ya kuyapokea maneno yao, kwa sababu ya kutaka kuufahamu ukweli wa kazi hizo na maneno hayo. Yeye huongea ukweli na hupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukumu yake, kwa sababu ya kufanya kazi njema alizozifanyia utafiki wa kina, kabla ya kuzianza, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na lile jembe lililoendelea kuwa gumu hata wakati wa kulilimia, kwa sababu naye hupata mafanikio mengi katika kazi zake, maishani mwake. Yeye huwafundisha pia watu wake namna ya kuzifanyia utafiti wa kina kazi zao, kabla ya hawajaanza kuzitekeleza. Ndiyo maana huwaambia watu hao kwamba, “ugumu wa jembe kusubiri kwenye palizi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzifanyia utafiti wa kina kazi zao, kabla ya kuanza kuzitekeleza, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika utekelezaji wa majukumu yao, maishani mwao.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 12:33-37.

africa-121

black-12

ENGLISH: THE DIFFICULTY OF THE HOE IS TO WAIT FOR WEEDING TIME.

A hoe is a farming tool for the farmer. It is known to have a hard time in cultivating at the time of working, because the hard one does not bend. But the loose ends when the farmer begins to week. That is why people say that, “The difficulty of the hoe is to wait for weeding time.”

This proverb is likened to a man who conducts a thorough study of all the works before he begins to do them, in his life. This person, in turn, conducts research that is good enough to understand the behavior the people to whom he is speaking before accepting their words, out of an aim of understanding the truth of their works and words. He speaks the truth and finds great success in the discharge of his duties, because of the good works that he has done in-depth research, before starting to work them out, in his life.

This person is like the hoe that continues to be difficult even when it is weeding, because he also finds great success in his work, in his life. He also teaches his people on how to do their research thoroughly, before they start doing their works. That is why he tells them that, “The difficulty of the hoe is to wait for weeding time.”

This proverb imparts in people a clue on how to do a thorough research on their works, before they start implementing them, so that they can be more successful in fulfilling their responsibilities, in their societies.

Matthew 7: 15-20.

Matthew 12: 33-37.