134. LEKAGA KWISHINA BHUBHABHU BHO BHEZE

Research Sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya lusumo lwenulu ihaiye giki: ikale ibheze jaliningi noi umukaya ga bhanhu. Jikalaga jiguyelaga umunumba yabho. Nose jigayubhaluma ahikanza lya bhujiku na jabalekelaga bhubhabu bhoguyikala bhagwisinaga bhuli makanza.

Nose bhagaiwila giki, bhaleke ugwishina ubhubhabhu bhunubho, nguno bholekwa na bheze duhu. Ijinaguhaya chene, lugabhiza lusumo uluhaile giki, “Lekaga kwishina bhubhabhu bho bheze.”

Lusumo lunulo, lugalinganijiyagwa na makoye ayo gabhita ukubhanhu. Ukwene huguhaya giki, idichiza umunhu ugwikala alizuka imihayo iyoyabhita.  Nulu idichiza ugwikala aligizuka amakoye ayo gabhita.

Ubhulangwa bho lusumo lwenunu, bhuli higulya ya kuleka gugwishiwa ngholo na makoye ayo gabhita, nulu mihayo imibhi iyoyabhita. Ilichiza ukulimunhu ugwandya bhupya, uluopandikaga makoye.

Ayubu 3:1-4.

KISWAHILI: ACHA KUJIKUNA MUWASHO WA MENDE

Chanzo cha methali hii husema kwamba, zamani mende walikuwa wengi mno katika familia za watu. Walikuwa wakitembea ndani ya nyumba zao.

Mwishowe wakaanza kuwa wanawauma watu hasa wakati wa usiku, na kuwaachia muwasho. Wakawa wakijikuna kila wakati.

Mwishowe wakawa wakiambiana kwamba, waache kujikuna muwasho huo, kwa sababu uliachwa na mende tu. Kwa kusema hivyo ikapatikana methali isemayo, “Acha kujikuna muwasho wa mende.”

Methali hiyo, hufananishwa na matatizo yaliyopita.  Ndiyo kusema kwamba, siyo vizuri kwa mwanadamu kuwa anayakumbuka maneno yaliyopita. Au siyo vizuri kuwa anayakumbuka matatizo yaliyopita.

Fundisho la methali hii, ni juu ya kutokuvunjwa moyo au kukatishwa tamaa na matatizo yaliyopita, au maneno mabaya yaliyopita. Ni vizuri kwa mwanadamu kuanza upya akipata tatizo badala ya kukata tamaa.

“Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.  “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’ Siku ile na iwe giza, Mungu juu na asiiangalie nayo nuru isiiangazie.” (Ayubu 3:1-4.)

ENGLISH: STOP ITCHING AN ITCH OF BUGS

The source of this proverb says that a long time ago bugs were too many in the families of the people. They were walking in their homes. Eventually they began to bite people at night. People were constantly thinking about the itch of those bugs.

Finally, they were telling each other that they would have to get rid of them because their lives were being controlled by bugs. There was no point of continuing itching an itch of the bugs. In so saying a proverb was found: “Stop itching an itch of bugs.” This proverb is likened to past problems. That is, it is not good for people to continue recalling their previous problems or bad words to the point of losing hope in their lives. It is not good to lose hope because of their past problems. The teaching of this proverb is not to be discouraged by past problems or past bad words. It is good for a person to start regaining new strength positively in his or her life.

“After this, Job opened his mouth and cursed his birthday. “My birthday and go away, and that night it was fitting, ‘The boy is born!’ Let that day be darkness, and let God not look upon it with light to shine.” (Job 3: 1-4.)

monkeys-

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.