92. Ng’wana Nchembe

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale ya kale, bhanhu bhagalazimika gwilipa bho gubhala magulu mpungati bho mpungati. Na gwiyunguja mhembe inne bho guchimika mambo.

Oliho munhu uyo witanagwa Ng’wana Nchembe uyo agaja ntuzu kugiki guhangilwa. Aho oshika ukunuko agawilwa giki agupandika bhusabhi bhutale. Agawilwa hangi, agutung’wana nabho umu nzila yiniyo duhu.

Ugonhana, agailondeja inzila yiniyo. Aho oshika bhukule bho kilomita ikumi, agaibhona mondoka ndoo iliza wangu wangu. Wihayila umu nholo, “Nibhuli imondoka yiniyi iliza bho lugendo lukali giki?”

Imondoka yiniyo aho yabhiza ilegela noi, Ng’wana Nchembe aliomala kale uguyileka inzila yiniyo nhangala idatu. Agafujafujiwa gubholwa ni limondoka linilo. Imondoka yiniyo yigabhita na gugwisha lisandiko lyokalile hela, noti pye. Ilisandiko lwenilo lyalilidakundikijiwe.

Huna u Ng’wana Nchembe, agaja gujulilola. Agajibhona noti ningi noi. Agakumya na gwiyombela ng’winikili, “Ee nite ki ni hela iji?” Agagema guliduta ilisandiko linilo guja ng’wipolu kugiki ajibhise ihela jinijo. Uduja gujibhisa bihi ni nzila.

Aho yabhita saa imo, Ng’wana Nchembe agibhona imondoka yiniyo ilishoka. Uguhaya ubhunhana, Ng’wana Nchembe agachanganyikiwa noi ahigulya ya hela iningi jinilo ijo olojikuga.

Agafuma ung’wisaka na gwimila ha lwande lo nzila, na gwandya gubhapungila nkono abhanhu abho bhali mumondoka. Agabhawila, “Nzugi, aha jiliho hela ningi noi.”

Aho bhigwa iyombo bhagayomba, “Ehe, dimiche imondoka kugiki duje dugandegeleke umunhu uyo.” Udeleva agaimicha imondoka. Bhutung’wana nu Ng’wana Nchembe alinilisandiko linilo ilo lyalilyokalile hela ningi.

Bhagamuja, “Ulihaya ginehe?” “Ilisandiko linili lyokalile hela ningi noi, na nadamanile nite ki najo!” agayomba u Ng’wana Nchembe. Ahanaho, udeleva, polisi nu ntuji o hela, bhagibhuja, “Ee, dung’witile ki umunhu uyu?” “Dumulage,” deveva agashosha.

“Yaya, dudizumulaga bhabehi. Aliyo duntule mapi na gung’winha noti ya shilingi ikumi.” Agashauri untuji o hela. Halafu, upolisi agantala mapi na gung’winha ishilingi iji kumi du na gungema nyahala, “Ulimbuli noi ubhebhe. Udalasabha bhulunga kele gete.” Mpaga leo iyi, ung’wana Nchembe alinhabhi.

 

Kiswahili:  Mtoto Wa Nchembe (Ng’wana Nchembe)

Hapo zamani za kale, watu walilazimika kulipana kwa kuhesabu  miguu sabini kwa sabini.  Na kuzungushia pembe nne kwa kupigilia vijiti (mambo). Kulikuwapo na mtu aliyeitwa Ng’wana Nchembe ambaye alikwenda Ntuzu ili kuzindika. Alipofika huko aliambiwa kuwa atapata utajiri mkubwa. Aidha, aliambiwa kuwa atakutana nao kwenye barabara hiyo hiyo tu.

Kweli, aliifuata barabara hiyo. Alipofika umbali wa kilometa kumi, aliliona gari dogo linakuja kasi mno. Akajisemea moyoni, “ Mbona gari hili linakuja kwa mwendo kasi hivi?”  Gari  lilipokuwa linakaribia zaidi, Ng’wana Nchembe tayari alikuwa amekatisha barabara mara tatu. Alikoswakoswa kugongwa na gari hilo.

Gari lilipita na kuangusha sanduku lililojaa fedha, noti tupu. Sanduku lenyewe halikuwa limefungwa. Ndipo Ng’wana Nchembe alikwenda kuliangalia. Aliziona noti nyingi sana.  Alishangaa na akajisemea mwenyewe,  “Je nifanye nini na hizi fedha?”  Alijaribu kulivuta lile sanduku kuelekea porini, ili aweze kuzificha zile fedha. Akafaulu kuzificha karibu na barabara.

Saa moja baadaye, Ng’wana Nchembe aliliona lile gari linarudi. Kusema kweli, Ng’wana Nchembe alichanganyikiwa sana kuhusu zile fedha nyingi alizookota. Akatoka kule kwenye kichaka na kusimama kando ya barabara na kuanza kuwapungia wale watu waliokuwa kwenye gari. Akawaambia, “Njooni, hapa kuna fedha nyingi sana.”

Waliposikia kelele wakasema, “Haya, tusimamishe gari ili twende kumsikiliza mtu yule.” Dereva akasimamisha gari. Wakakutana na N’gwana Nchembe akiwa na lile sanduku lililofurika fedha nyingi. Wakamuuliza, “Unasemaje?”

“Sanduku hili limejaa fedha nyingi sana, na sifahamu nifanye nazo nini!”  Ng’wana Nchembe alisema. Hapo dereva, Polisi na Bwana fedha waliulizana, “Je tumfanyie nini mtu huyu?”  “Tumuue,” dereva alijibu.

“Hapana, tusimuue jamani. Ila tumpige tu makofi na kumpa noti ya  shilingi  kumi.” Alishauri bwana fedha.

Baadae, Polisi alimzaba makofi na kumkabidhi shilingi kumi tu na kumkejeli,  “Mpumbavu sana wewe. Kamwe hutatajirika milele.” Mpaka leo hii, Ng’wana Nchembe ni maskini.

treasure-chest

English: Nchembe’s Child (It became a name ‘Ng’wana Nchembe’)

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.