49. Ngoso Na Ntegi Wa Nzwabu

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Kale walaliho munhu, wali ntegi wa nzwabu. Aho alija kujulinga wakabhitila kagoso kigashije ha mahushi. Kang’wila “Ligisha,” nang’hwe walema kuzunya. Nako kang’wila giki, “Nene ndakuyangula bhebhe nu bhutegi wako”.

Huna lushiku lumo ubhita, kung’wi1a hangi, ulema, uja. Wahayushika ha lwabu lwakwe, ulisangaho lishimba lyagwashiwaho. Lyung’wila giki, “Nitaligulilage wanduhaja no no no, bhujiku wa lelo natadimile nulu ndimu imo yaya.” Ulitaligulila.

Lyung’wila giki, “Ninhage ngobho yako nalye natubhaga no.” Ulinha. Lyumala, lyulomba shilalo sha lushu, na hene lyumala. Hangi lyulomba nshipi gwa munkimbili, lyugumila nugwene.

Huna lyunomba nkono gumo alibhutileho, ulila no. Huna kiza lulu akagoso, ako wakabhitilaga. Kuhaya giki, “Ni bhuli ng’wanikungu watubha giki?” Shimba yuhaya, “Natubhiwagwa na lugoye lwa ntegi.” Leka kuhaya chene ng’wanikungu. Ali lulu gemelaga nabhone umo ukizila.

Ntegi uwilwa na ngoso, “Tegaga agemele tulole.” Ugemela nakiza giki, “Chene manyandishi, nupanda aha, chene ng’wanikungu.” Nose ugwashiwa ho hangi.

Ngoso yung’wila ntegi giki, “Dupelage lulu, wizuke nakuwilaga kinahe? Ndakuyangulaga.” Uzunya untegi giki, “Lelo waniyangula gete. Ali lulu naja kaya. Wabhizaga mpija wane mu Shimba. Ulize unigishe na bhiyo bhingi no no no. shose ukusanga nabheja shabhuhondo shingino.”

Huna ngoso yung’wila untegi, “Ali lulu, ulu ndizage mutizita shiliwa shigehu. Abhichane bhali no. uhaya giki, “Bhatudula kushimala.” Huna bhubhuka.

Ngoso ya magana shiku. Jushikila mu mahaka na ha nyango. Shiliwa shulebha, julya ni ndili shaho, nijene jushila. Nose jukalya na ntana. Huna bhusaya abhanhu, bhujitula. Ngoso kufuma henaho juzenga mu bhanhu. Kale jikalaga mu mahushi ng’wagala.

Kiswahili: Panya Na Mtegaji Wa Wanyama Pori Kwa Kamba (Nzwabu)

Zamani aliwepo mtu, aliyekuwa mtegaji wa “Nzwabu” Mwindaji wa wanyama wa porini kwa kutumia Kamba.” Alipokuwa anaenda alimpita panya amekaa kwenye miti iitwayo Magushi. Kalimwambia, “Nisalimie,” naye alikataa kukubali. Nako kalimwambia hivi, “Mimi nitakuamulia wewe na utegaji wako wa wanyama wa porini.”

Basi siku moja alipita, kakamwambia tena, akakataa, akaenda. Alipofika kwenye mtego wake, akakuta pale simba amenaswa. Akamwabia, “Nifungulie hili limenitesa mno, usiku wa leo sijashika hata mmoja wa wanyama wa porini hapa” Akamfungulia.

Simba akamwambia hivi, “Nipe shuka yako nile nina njaa mno. Akampatia. Simba akamaliza, na kumwomba kile kilalio cha kisu nacho, simba akakimaliza. Aliomba tena mshipi wa kiunoni,  simba akaumaliza nao.

Basi, akamuomba mkono mmoja amkatie hapo, alilia mno. Ndipo sasa ka Panya kakaja, kale alikokuwa anakapita bila kukasalimu. Kakasema kwamba, “Kwa nini Mwanikungu umeshikwa njaa hivi?” Simba akasema, “Ninanjaa kwa sababu ya Kamba ya Mtegaji.” Panya akasema, “acha kusema hivyo, mwanikungu, hebu jaribia tuone vile ulivyokuja.”

Mtegaji akaambiwa na Panya, “Tega ajaribie tuangalie.” Simba alijaribia, “Nilikuja hivi, Kweli Manyandishi, nikakanyaga hapa, kweli Mwanikungu.” Mwishowe akakamatwa tena hapo.

Panya akamwambia Mtegaji hivi, “Tukimbie basi, ukumbuke nilikuambiaje? Nitakuokoa.” Akakubali mtegaji kwamba, “Umeniamulia, kwa maana ya kuniokoa kabisa. Hivyo basi, naenda nyumbani. Umekuwa mkombozi wangu kutoka kwenye hali ya kuliwa na Simba. Utakuja unisalimu na wenziyo wengi mno mno mno. Vyote utakuta nimeandaa vya kufurahia vingi sana.”

Panya alimwambia mtegaji, “Basi, nikija msiandae chakula kidogo. Wenzangu wanakula mno. Akasema hivi, “Hawataweza kukimaliza chakula. Ndipo wakaanza safari.

Panya ya mamia siku. Wakafikia kwenye miti iliyoezekewa nyumba yao na mlangoni. Chakula kikapungua, wakala na ngozi zao, nazo zikaisha. Mwishowe wakala na vitu vilivyofichwa. Ndipo watu wakakasirika, wakawafukuza. Kutoka hapo Panya akajenga kwa watu. Zamani waliishi kwenye miti ya mahushi, kule Mwagala.

rat and man

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.