50. Subhi Na Lung´wando

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Waliho muna Subhi walazengile hipande ilebhe, ubhona hambu hambu nasame henaha. Giko wandya kubhuta mazengo, aho waja kukindika nigo gwa mazengo. Aho winga ho, Sayayi nang’hwe utwala nigo gwa mazengo, ntondo Subi usanga miligo ibhili ukumya! Utula gwa kadatu. Aho winga ho Sayayi wenha nigo gungi yushika inne. Bhamanaga bhita giko na kwibhona yaya.

Nose lushika lushiku lwa kusimbila numba, muna Subi usimbila ipande uja. Sayayi nang’hwe wiza usimbila ipande, numba yushila. Wandya kulumba muna Subi ulumba. Sayayi nang’hwe ipande lyakwe. Nose makanza gashiga ga kuikanda inumba.

Lushiku lwa kusamila mo Sayayi utonga kuja mo mu chumba jakwe. Giko wandya kubhacha moto, muna Subi ubhuja, “Nani wapemba moto mu numba yane,” Sayayi nang’hwe, “Nani wapemba moto mu numba yane.” Bhandya lulu kwiduka, aho wasaya umuna Subi, Sayayi ung’wila nke, “Bhalijage abhana.”

Aho bhalila, Sayayi umuja nke, “Bhana bhenabha bhalilijiwa ki?” Aho bhalila, Sayayi ushosha giki, “Bhalililila matima ga Mhuli. Aho wigwa Subi giki bhalihaya kubhulaga Mhuli bhabhenhele bhana bhabho matima wogoha ufumula.

Giko bhulala, ku ntondo hanngi yandya yombo. Sayayi ung’wila nke hangi, “Bhalijage abhana,” aho bhalila, ubhuja usayayi, “Bhana bhalilijiwa ki?” Nkima ushosha, “Bhalililila matima ga Subi.” Sayayi uhaya “Gwenuyu guli nimo ndo, bhabho bhalumu ntondo nakubhabhulagila bhana bhane bhalye matima.”

Bhana Subi bhatalalile bhujiku, aho wela dilu bhusama na kusama. Aho bhalisama bhukamanhya na Nguku. Nguku, ikumujaga giki, “Uyijiwa ki? (kuyila) dilu cheniki.” Nang’hwe alihaya, “Napejiwa mu numba na Sayayi angu bhana bhakwe bhalililila matima ga mhuli, ntondo bhakulya matima ga Subi.

Nguku yung’wila muna Subi giki, “Unene amasala ga ng’wa Sayayi nagamanile. Tujage nakutwale, twilujage (twilunganyage) mikila yise.” Aho bhegela Sayayi ung’wila nke, “Bhalijage abhana,” aho bhalila, Sayayi ubhuja, bhalilila ki?” Nkima uhaya, “bhalililila matima ga Subi.” Sayayi uhaya, “Chuu!! Twalaganaga na muna nguku giki akunenhela, uyo.” Aho wigwa muna subi uhaya, “Bhebhe walunilemba lembaga nakutwale, gashinaga wamalaga kulagana.” Bhuja bhakwidutanjaga wilekela numba yubi ya ng’wa Sayayi.

Kiswahili: Chui Na Sungura

Kulikuwa na chui aliyekuwa anaishi sehemu Fulani, aliona afadhali ahame. Hivyo alianza kukata fito za kujengea. Akaenda kuweka mzigo wa fito.

Alipoondoka pale, sungura naye alipeleka mzigo wa fito pale, kesho yake Chui alikuta mizigo miwili alishangaa! Aliweka wa tatu. Alipoondoka pale Sungura akaleta mwingine ikafika mine. Walikuwa wakifanya hivyo, bila kuonana.

Mwishowe ikafika siku ya kuchimbia nyumba. Chui alichimbia upande akaenda. Sungura naye akaja kuchimbia upande, nyumba ikaisha. Wakaanza kuezeka, chui akaezeka. Sungura naye upande wake. Mwishowe ukafika wa kuziba kwa matope nyumba hiyo.

Siku ya kuhamia humo Sungura alitangulia kwenda kwenye chumba chake. Hivyo akaanza kuwasha moto, chui akauliza, “Nani amewasha moto kwenye nyumba yangu?”

Sungura naye, “Nani amewasha moto kwenye nyumba yangu?” Wakaanza sasa kutukanana, alipokasilika Chui, Sungura alimwambia mkewe, “walize watoto.”

Walipolia watoto, Sungura alimuuliza mkewe, “Watoto wanalizwa na nini?” Walipolia Sungura alijibu hivi, “Wanalilia maini ya Tembo.” Chui aliposikia kwamba wanataka kuua Tembo wawaletee watoto wao maini, aliogoka, akanyamaza.

Hivyo walilala, kesho yake tena kelele ikaanza. Sungura akamwambia mkewe “walize watoto,” walipolia, aliuliza Sungura, “Watoto wanalilia nini?” Mkewe akajibu, “Wanalilia maini ya Chui.” Sungura akasema, “Hii ni kazi ndogo, hao wapo humu, kesho nitawaulia watoto wangu wale maini.”

Chui hawakulala usiku, kulipokucha asubuhi walihama na kuhama. Walipokuwa wanahama walikutana na nyani. Nyani aliuliza hivi, “umetoka jasho kwa sababu gani asubuhi hii?”

Naye Chui alisema, “Nimefukuzwa kwenye nyumba yangu na Sungura, eti watoto wake walililia maini ya Tembo, kesho watakula maini ya Chui.

Nyani alimwambia Chui hivi, “Mimi akili za Sungura nazifahamu. Twende tufungane mikia yetu.” Walipokaribia Sungura alimwambia mkewe, “walize watoto,” walipolia, Sungura alisema, “Aaa!! Tumeagana na nyani kwamba ataniletea huyo.”

Chui aliposikia hivyo, alisema, “Wewe ulikuwa unanidanganya danganya nikupeleke, kumbe umemaliza kuagana.” Wakaenda wakivutana, wakaiacha nyumba ikawa ya Sungura.

arctic-hare-828994__340

leopard-

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.