19. Kaya Imo Yalina Bhana Bhadatu: Bhayanda na Nkima

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Yaliho kaya imo yalina bhana bhadatu bhayanda na nkima okanne, bhuwilwa ubhujiku aho jikome, nkima ubhawila, bhing’we bhayanda gashigaga malima, dujagi dugahambe mbiyu jise dugalime. Aho jazwa bhandya guhamba. Aho bhamala uguhamba bhigasha.

Umumpunga gupya, aho gopya, bhiwila ubujiku aho jikome ubhebhe nzuna wise intondo udime indama unyanda ohagati uwilwa gudima ng’ombe, unkulu obho uja kumpunga gujulola ulu jidulyaga inoni.

Usanga jigulyaga wandya gulinda gufuma saa imo. Aho yashiga saa inne lyushiga inoni ilo ligalyaga lyita kwa kwa. Aho olibhona itale no ogoha no na gupela uyomba unene nadulinda hangi. Uja kaya ugabhawila bhazunaye na mayu okwe, natalalinda hangi.

Uyomba uungi, nkulu wise ummpunga gushile, unene naguja ugujulinda. Aho wela uja ugalinda, gufuma saa imo, aho yashiga saa inne lyushiga inoni ilo ligalyaga umupunga lyita kwa kwa. uyomba noni ki iyi, nadulinda hangi uja kaya ugabhawila nkulone uyomba unene naguja nagalinde.

Aho wela uja ugalinda gufuma saa imo, aho yashiga saa inne lyushiga inoni iloligalyaga umupunga lyita kwa kwa. Wima du unyanda uyomba nashoge kaya nagadose lugoye. Aho oshiga ikaya ung’wila unina na bhakuluye nalibhonaga ilinoni na lulu nadose lugoye. Aho wela uja na lugoye ugatega na gulindila na yushiga inoni yupujiwa upela guja ho.

Aho oshiga ho yuyomba udizunibhulaga nunene nalagupija. Ukumya no, noni ki iliyomba, nalilomba unilekeje nadalalya umpunga. Lyung’wila injaga uloya ulohagati ululihu, uiitaligulila winja uloya lyung’wila lujanage kaya ugalutule umupunga. Aho guma bhugesa bhakaja amabhelele, bhugaiwa aho bhagutule.

Nzuna wabho ubhawila bhakuluye agateme ngito. Mayu obho uyomba bhebhe nyanda ulindo no bhawilage bhakuluyo bhagateme. Uyomba unyanda nulu nene natoshije, bhakulu bhane bhadamanile gusuma mabhelele.

Nahene jaga, uja lokwandya limi buu, wela hangi uja limi buu, hangi wela uja hangi ugajimila mpaga shigu idatu aling’wipolu. Umona nkima umo makanza ga saa idatu, dilu alinajisabho alidaha minzi unsanga ho ungisha. Ulomba minzi winhwa, aho wang’wa umuja mayu utolilwe, nang’hwe uyomba natolilwe, nalilomba uganizugile shiiiwa, hamo ngoshi oko agudaka.

Nang’hwe uyomba ngoshi one ihaha alinduhu akizaga makanza ga saa kumi na mbili, nulu saa imo, duje kaya uganizugile, unkima uyomba ngoshi one nkali no, agunibhulaga udizuja ikaya.

Nite kinehe lulu natubhile, jaga uko kunima nukwenhela ijiliwa ugigashe ko, nkima uja ugazuga jiliwa unjanila ugalya ngosha ng’wenuyo aho olya uyomba nane nalihaya ditole nang’ho, nkima uyu ung`wila, lalaga henaha, dugubhona lushigu lungi.

Lushigu lo kabhili ujana hangi aho omala ugulya ngoshi ung`wila dujage, bhuja mpaga kaya. Aho ngosha oshiga wingila na gufuma hanze wipindilija inumba utula ajile kiya mpaga kule ugashoka uja hangi dakama mpaga kule hangi ugashoga hangi wiza wingila mkaya. Bhufuma na nkima hanze bhuja bhugifeng’ha mumakwi ushiga ungoshi, uyomba isu ngeni, ufuma hanze nagwipindilija inumba aliyomba isu ingeni, ufuata ukowandija uguja ungoshi, kiya aliyomba isu ingeni, ushoga ufuata hangi guja ng’weli aliyomba, isu igeni, ushoga hangi aliyomba isu igeni, ufuata hangi dakama aliyomba isu igeni, ushoga hangi aliyomba isu igeni ufuata hangi.

Aho wegela hamakwi uyomba isu igeni, nang’ho odunoja iyoka yalinamitwe mpungati aho oyomba isu igeni, lyumona na gunuma ngoshi ucha. Haho na haho iza noni yung’wanhila upila ulitema untwe.

Aho obhuka inzoka iliyomba isu igeni lyunuma hangi ucha. Iza hangi inoni yung’wanhila upila agalitema pye mitwe ulinyola iliyoka. Inoni yung’wila dujage kaya nkima na ngosha bhulina hanoni lyubhajana ukolizengile ilinoni bhubhiza bhageni ubhawila unyanda uyu aganipija olohaya gunibhulaga lyumuja umanile ikaya uyomba natamanile dujage lulu nagujane.

Lyunjana uko malambo ga mpunga lyumuja omana lulu ikaya uyomba namana lyunjana mpaga kaya. Aho bhashiga bhuyomba oshiga unyanda, unina uyomba mlinilemba ng’wanone ojimila shigu ningi. Aho bhashiga inoni yubhawila, mayu unene namalaga umpunga gwing’we. Mayu ng’wene utogwa no inoni yuyomba nafuate nang’winga oko, ng’winga ufuatwa. Aho yang’wenha inoni yuyomba ninhagi uloya lone, inoni inhwa yushoga kaya.

Na Sophia Kahabi

Kiswahili: Familia Moja Ilikuwa Na Watoto Watatu: Wavulana Na Mwanamke

Kuliwepo na familiya mojo iliyokuwa na watoto watatu wavulana na mwanamke wanne. Waliambiwa usiku kwenye kikao cha jadi wakiwa wamezunguka moto, mwanamke aliwaambia, “nyie wavulana, kipindi cha kilimo kimefika. Twendeni tukapande mbegu zetu tukalime. Zilipoota walianza kupanda. Walipomaliza kupanda wakakaa.

Mazao ya mpunga yalikubali. Baada ya hapo, wakaambiana usiku kwenye kikao cha jadi wakati wakiota moto, “wewe mdogo wetu kesho uchunge ndama”. Mvulana wa katikati aliambiwa kuchunga ng’ombe, mama yao alienda kwenye mpunga kwenda kuangalia kama ndege hawali.

Alipoenda alikuta ndege wanakula akaanza kulinda kutoka saa moja. Ilipofika saa nne likafika lindege amabalo huwa linakula huku likifanya “kwa kwa.” Kwa vile lilikuwa kubwa mno, alipoliona aliogopa mno na kukimbia, akasema, “mimi silindi tena.” Akaenda nyumbani kuwaambia, wadogo zake na mama yake, “Sitalinda tena.”

Mwingine akasema, “kaka yetu, mpunga uishe! Mimi nitaenda kulinda. Kulipokucha, alienda kulinda, kuanzia saa moja, ilipofika saa nne, likafika lile lindege ambalo huwa linakula mpunga huku likifanya ‘kwa, kwa.’ Akasema, “ndege gani huyu, sitalinda tena,” akaenda nyumbani kuwaambia, “kaka yangu, mimi nitaenda kulinda.”

Kulipokucha alienda kulinda kuanzia saa moja. Ilipofika saa nne, lile lindege likafika linalokula mpunga huku likifanya ‘kwa kwa.’ Akasimama tu, mvulana, akasema, nirudi nyumbani nikatengeneze kamba. Alipofika nyumbani, alimwambia mama yake, na kaka zake, nimemuona ndege kwa hiyo, nitengeneze kamba. Kulipokucha, alienda na kamba akaenda kutega na kusubiria, yule ndege alifika akaja kukamatwa, akakimbia kwenda pale.

Alipofika pale, ndege yule mkubwa akasema, “usiniue nami nitakuja kukuponyesha. Alishangaa mno, “ndege gani huyu anaongea,” “naomba unisamehe sitakula mpumga. Ondoa unyoya wa katikati ule mrefu.” Akalifungulia akaondoa unyoya ule mrefu, likamwambia, “upeleke nyumbani ukauweke kwenye mpunga.” Ulipokauka, wakavuna, na kuujaza kwenye maghala yao yote, mpaka wakakosa mahali pa kuuweka.

Mdogo wao aliwaambia kaka zake, akakate miti ya kutengenezea ghala. Mama yao alisema, “wewe mvulana ni mdogo mno waambie kaka zako wakakate.” Mvulana akasema, “hata mimi natosha, kaka zangu hawajui kushona maghala.”

“Sawa nenda.” Akaenda siku ya kwanza, kutwa nzima, kesho yake akaenda tena kutwa nzima, na siku iliyofuata akaenda tena akaenda kupotea mpaka siku tatu yuko porini. Akamuona mwanamke mmoja wakati wa saa tatu asubuhi, akiwa na kibuyu akichota maji akamkuta pale akamsalimu. Aliomba maji akapewa. Alipokunywa alimuuliza, “Mama umeolewa?” Naye alijibu, “nimeolewa.” Naomba ukanipikie chakula, labla mme wako atakasilika.

Naye aliseama, “Mme wangu kwa sasa hayupo, huwa anakuja wakati wa saa kumi na mbili jioni, au saa kumi na moja,” “Twende nyumbani ukanipikie,” mwanamke alisema, mme wangu ni mkali mno, ataniua usiende nyumbani.

“Nifanya nini basi, nina njaa?” Mwanamke akajibu, “nenda mlimani, nitakuletea chakula huko.” Mwanamke akaenda kupika chakula akampelekea akala mwanaume huyo. Alipokula, alisema, “nataka tuoane nawe.” Mwanamke huyu alimwambia, “lala hapa, tutaona siku nyingine.”

Siku ya pili, alipeleka tena chakula, alipomaliza kula, mme wake alimwambia, “Twende.” Alienda mpaka nyumbani. Mwanamume alipofika aliingia ndani akatoka nje akaizunguka nyumba, akaelekea mashariki mpaka mbali, akarudi na kwenda tena kusini mpaka mbali, tena akarudi na akaja kuingia ndani nyumbani.

Wakatoka na mwanamke nje, wakaenda kujificha kwenye kuni. Mme wake akafika, akasema, “harufu ngeni,” akatoka nje akaizunguka nyumba akisema, “harufu ngeni, alifuata alikoanzia kwenda mmewe, mashariki akisema, harufu ngeni, akarudi akafuata tena magharibi, alikisema, “harufu ngeni.” Akarudi tena akisema, “harufu ngeni.”  Akafuata tena kusini, akisema, “harufu ngeni.” Akarudi tena akisema, “harufu ngeni.” Akafuata tena.

Alipokaribia kwenye kuni, akisema, “harufu ngeni.” Nawe umetuchosha, joka lenye vichwa saba, aliposema, “harufu ngeni,” likamuona na kumuuma mme wake akafa. Hapo hapo akaja ndege akamzomea, akapona akalikata kichwa.

Aliposimama, joka likasema, “harufu ngeni,” likamuuma tena akafa. Akaja tena yule ndege akamzomea akapona, akamkata vichwa vyote akalishinda lile joka.

Ndege alimwambia, “twende nyumbani, mwanamke na mwanaume wakapanda mgongoni mwa ndege huyo, akawapeleka kule anakokaa yule ndege, wakawa wageni wa yule ndege. Akawaambia “mvulana huyu aliniokoa alitaka kuniua. Akamuuliza, “unafahamu nyumbani?” Akasema, “sifahamu.” Yule ndege akasema, “twende basi nikupeleke.”

Yule ndege mkubwa, alimpeleka kwenye majaruba ya mpunga, akamuuliza, “umefahamu sasa nyumbani?” Akasema, “nimefahamu,” Akampeleka mpaka nyumbani.

Walipofika wakasema, “mvulana amefika,” mama akasema, “mnanidanganya mtoto wangu amepotea siku nyingi.”

Walipofika yule ndege mkubwa, aliwaambia, “mama mimi nilikuwa namaliza mpunga wenu.” Mama yule alifurahi mno. Yule ndege akasema, “nifuate na mkaa mwana wako.” Mkaa mwana akafuatwa. Yule ndege alipomleta alisema, “nipeni unyoya wangu.” Ndege yule akapewa unyoya wake akarudi nyumbani.

Na Sophia Kahabi.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.