18. Ngosha Nseni wa Ng`hwi

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Oliho bhabha umo oli nseni ong’hwi. Nalulu nang’hwe goli nimo go bhuli lushiku, ubhabha ng’wenuyo olishaga bhana bhakwe gulogusena ng’hwi.

Onoga nose bhabha ng’wenuyo ayibhuja, nibhuli shi unene nagalyaga ja gukoyela shiniki, nibhuli abhangi bhagalyaga nulu bhadajile gung’hwi. Bhing’we bhabehi nalabheja ahene unene.

Bhabha ng’wenuyo umugwibhuja gokwe agibhuja nose wiwila hambu hambu ulu gwibhulaga na ng’hana agabhuka kuja kujuyela ng`wipolu, munumo ubhona ahasoga wiwila ahanaha yafayaga ugwibhulagila.

Bhasi agandya gwitungila lugoye lokwe. Aho naho agawilwa na munhu, bhuli nkoyi ulihaya gwibhulaga aliyo utali shiku ningi giki ahawelelo na lulu utali na miaka makumiane iyagwikala umusi.

Munhu ng’wenuyo akanemeja nkoyi lekaga gete ugwibhulaga ulabheja duhu imyaka yagubhutongi. Na hangi naguwile giki ihaha senaga ng’hwi duhu uje kaya, ulu ushika ikaya imhindi ugayele hasokoni ugubhona nkima aguyelaga, nkima ng’wenuyo ng’wilage gwitola.

Ngosha ng’wenuyo ogashika ikaya agibhona imhindi yadilaga aje ugusokoni. Nose yushika imhindi okabhilaga aliwila unkima ng’wenuyo hamo nalinajo ijikolo nagusabha.

Agaja gusokoni ng’hana ugamona unkima ng’wenuyo aguyelayelaga agang’wila goguntola. Nang’hwe adalemile uzunya ng’hana unsola lulu ubhiza na bhakima bhabhili, gukula hangi lulu unigo ubhiza ongeja likoye hangi lingi wendelea duhu ichene ugujisena ing’hwi bhiza bhalya.

Imanila hangi lushiku goshika ugokwe, uiwila bhabehi unene naiwilaga giki nkima ng’wenuyu agunisabya gashi yaya. Unene mumo namalila duhu, gogwibhulaga nayubhela. Bhasi wela usola hangi lugoye guja ng’wipolu gujibhulaga, agiwila naduja uko nalinaja, ihangi nalole kungi.

Agalola ipande lingi ng’hana ugashika halinti limo isoga usola lugoye lokwe ugwasija hangi. Ushika hangi umunhu okwe ung’wila, hama hangi iki nagagulemeja bhuli hangi osola lugoye?

Nang`hwe ushosha nibhulage nkoyi, nagongeja ikoye duhu nagukoyaga noyi. Ubhulingisilo bho ng`wenekili ulu bhutali ugushikila agalemejiwa nulo kabhili uwilwa giki solaga ahenaho yiyo juba yina bhugota ulu ushika ikaya ugogwandya nuguwila giki, wibhuje ning’wa nani aliho nsatu, nkoyi unene nagubhiza nang’ho bhulikanza ulu ugashika aho linsatu uguyulola bhulingisilo bhone mumakono ulugikalile kabhuli lushiku mumo agupila ulu kikalila guntwe mumo udupila ulu gikalila gumagulu ng’wenuyo agupila.

Huna ungosha ung`habhi ng’wenuyo agasena ng’hwi hangi usola na jubha uja kaya ukawila obheja nkoyi. Bhulekana ogashika ikaya wandya lulu gwiganika. Ng’wa nani aliho nsatu, uwilwa aliho ng’wa mbati.

Agabhuka gujunola unsatu ng’wenuyo, ogashika ho ubhagisha ubhabhuja ginehe akajile ka nsatu, ginehe amadilo gakwe? Nabho bhushosha yii bhabha, gadulindilile ikanza duhu. Nalulu mayu nalina bhugota bhogunagula unsatu.

Ngikulu uhaya yii, ugudula bhabha, ngosha uhaya nagudula duhu. Ngikulu uhaya nahene lulu bhabha nagulage. Haho na haho wingila umukaya ugunola unsatu. Wandya gulola ishimanyikijo jakwe ulola uguntwe ugaiwa, ulola gumagulu ugabhona amakono, umana agumpija.

Huna nilikanza linilo agang’wisha bhugota. Ubhawila giki nakwiza nanole makanza. Ushoka kaya ugaja gujusena ng’hwi. Ugasenha ushoka mhindi, uja hangi gujunola unsatu okwe, ugansanga ihali yakwe nsoga, odulaga naguyomba.

Ubhabha ng’wenuyo ulomba minzi ung’wisha hangi ubhugota, ubhawila giki ntondo dilu nagwiza nanole, uja kaya gujulala. Bhogela uja gujunola hangi unsanga alimila ogema nagushimiza. Kaya yayegaga no. Ung’wisha hangi ubhugota, ubhawila hangi giki, naje bhabehi nagaje gung’hwi. Agalemejiwa yaya bhabha, igishaga undegeleke unsatu.

Agandya gwibhula uhaya giki yaya bhabha nalekile shibhi no ikaya, namhala agamuja shibhi ki bhabha olekile? Nalekaga nduhu nulu shiliwa ugukaya.

Bhabha ng’wenuyo agadahilwa shiliwa magunila abhili na hela ya gutumamila bhuchalilwa ikaya. Agikala ho makanza ga shiku idatu ubhiza opila gete unsatu okwe.

Agandya guibhuja hangi, kimba ulu ng’wanani hangi. Wiganika ng’hana ing’wa ntemi aliho ng’wana okwe osata. Halushiku lo kane ubhawila abhaha kaya yiniyo, abehi nayeleyele kunu hadoo.

Nabho bhunzunilija ukubha ajile mpaga ng’wa Ntemi ugashiga upiga hodi ugihaya imihayo yakwe ahanyango. Uwilwa giki yichene bhabha ugamanile amalagilo ga ntemi?

Bhagabhulagagwa ulu uduma ugumpija ung’wana ontemi. Ngosha ng’wenuyo agahaya nahene duhu, iki ulu nadumaga, una lulu bhaganzunilija aha nyango wingila na ushika guko lintemi. Ung’wila makulu gakwe.

Aho ong`wila Ntemi uchalwa gunumba agabhitiwa gumpindo ugolekejiwa mitwe ya bhafumu abhobhanduma ‘ipindilijije pye indugu ya numba. Aho obhona uchalwa gujunola unsati, ushigila gulola ulumeng’ho ulo agalolaga ubhona giki agumpija.

Haho na haho wandya gung’winha bhugota, ung`wene shiku ibhili ubhiza opilaga gete. Ntemi agayega no agang`winha manong`ho gabhuli mbika. Nagubhejiwa ibarabara mpaga ha ng`wakwe, ugazengelwa na manumba. Welelo nhale ungosha ng´wenuyo ihaha goshika gobhusabhi agigasha ikanza lya ng’weji gumo haho.

Unsati ubhiza oshokelwa nu mili gokwe. Hanaho agabhiza opandika inong’ho hangi winhwa ng`waniki gutola ashishe bhadatu lulu. Na ubhegejiwa nu Ntemi liwinga litale no. Na bhagasamva iti hado.

Ili nong’ho ilingi utinilwa bhupande ubhiza Ntemi. Ngosha ng’wenuyo igashila imyaka yakwe wiyibhile nguno agabhiza nabhuyegi wibha nugogwinija.

Lushiku na lushiku ajile gujuyela alinudeleva okwe ubhabhona bhanhu bhalisimba jigila, ung`wila udeleva giki obhabhona abhanhu abho bhalisimba jigila?

Deleva okwe unshokeja, dujage dugukeleja, huna bhupela pela ubhona hangi bhanhu bhabhukije maiti, ung`wila hangi udeleva okwe obhabhona abhanhu bhabhuchije maiti, deleva ushosha, bhebhe nang’ho kadugukeleja.

Bhupela bhupela hangi hadoo, bhumona munhu alimicha iloli yabho, ung’wila udeleva nang’hwe uhaya bhebhe kadugudila, bhupela hadoo hangi bhubhona munhu ugubhutongi alimicha iloli yabho, ung’wila hangi udeleva imaga, nose wima ng’hana.

Umunhu ng´wenuyo umuja onimana? Nang’hwe ushosha, yaya nadugumanaga, umunhu ng’wenuyo wandya gwiyeleza, nunene uyo nagagutinila lugoye munhingo, uguhaya lulu nkoyi ishiku jako jashilaga lelo, haho na haho ucha na gucha.

Kiswahili: Mwanaume Mkata Kuni

Alikuwepo baba mmoja aliyekuwa mkata kuni. Basi, naye hiyo ilikuwa kazi yake ya kila siku. Baba huyo alikuwa akilisha watoto wake kwa kazi hiyo ya kukata kuni.

Mwishowe baba huyo alianza kujiuliza, “kwa nini mimi huwa nakula cha kuhangaikia hivi, kwa nini wengine hula hata kama hajawaenda kwenye kuni? Jamani nyie! Nitafanikiwa lakini mimi!”

Baba huyo katika kujiuliza kwake hivyo, mwishowe alifikia uamuzi wa kujiua. Kweli alienda porini kwenda kutembea, humo aliona pazuri akafikiri kuwa hapo ingefaa kujiulia.

Basi alianza kujifungia kamba yake. Hapo hapo aliambiwa na mtu, “kwa nini bwana unataka kujiua wakati bado una siku nyingi hivi za kuishi duniani, basi bado una miaka arobaini ya kuishi duniani.”

Mtu huyo alimkataza kujiua, na kumwambia kuwa, atafanikiwa kwenye miaka ya mbele. “Pia nikuambie hivi, sasa kata kuni tu uende nyumbani, ukifika nyumbani jioni ukatembee sokoni utaona mwanamke akitembea, mwanamke huyo umwambie muoane.”

Mwanaume huyo alipofika nyumbani, aliiona jioni kama imechelewa ili aende sokoni. Mwishowe jioni ikafika akiwa na hamu akifikiri kuwa mwanamke huyo labda ndiye mwenye mali, hivyo, atatajirika.

Alienda sokoni kweli, akamuona mwanamke huyo akitembea tembea, akamweleza suala la kumuoa. Naye hakutaa alikubali kweli akamchukua, akawa na wake wawili. Mzigo ukawa mkubwa tena ikawa ameongeza tatizo jingine tena. Basi aliendelea tu kuifanya kazi yake ya kukata kuni na kuuza na kupata kwa ajili ya wao kuja kula.

Akashtukia tena siku moja wazo lake likafika tena, akawa anajiuliza, “jamani mimi nilifikiri kwamba mwanamke huyu atanitajirisha kumbe hapana. Mimi nabaki na uamuzi wangu tu wa kujiua ndiyo itakuwa vizuri.” Basi kesho yake, alichukua tena kamba kwenda porini kujiua, akafikiria kutoenda kule alikoenda mara ya kwanza, alienda kwingine.

Kweli alienda upande mwingine na kuukuta mti mzuri akaifunga kamba yake tena. Akafika tena mtu wake akamwambia, “kwa nini tena hivi nilikukataza umechukua kamba?”

Naye akajibu, “nijiue bwana, naongeza tatizo tu nahangaika mno.” Lengo la mwenyewe kama halijafikia, alikatazwa na mara ya pili, akaambiwa hivi, “chukua hapo hiyo chupa ina dawa, kama ukifika nyumbani, jambo la kwanza nakuambia hivi, ujiulize kwa fulani kuna mgonjwa, bwana mimi nitakuwa nawe kila wakati ukifika kwa mgonjwa.

Utakuwa unaangalia lengo langu kwenye mikono maisha ya kila siku. Lakini kama mikono ikiwa kichwani, maana yake, mgonjwa hatapona, lakini ikiwa miguuni, mgonjwa huyo atapona.

Ndipo mwanaume huyo maskini alikata kuni tena akachukua chupa akaenda nyumbani akakaambia “asante bwana.” Wakaachana, alipofika nyumbani, alianza basi kufikiria. “Kwa nani kuna mgonjwa?” Akaambiwa “yuko kwa fulani.”

Alianza safari ya kwenda kumtazama mgonjwa huyo. Alipofika pale, aliwasalimu, akauliza, “vipi maendeleo ya mgonjwa, ameshindaje?” Nao walijibu, “hii baba, tunasubiria muda tu.” “Sasa mama, nina dawa ya kumtibu mgonjwa.”

Mama wa nyumba, alisema, “hii, utaweza baba?” Mwanaume alisema, “nitaweza tu.” Mama wa nyumba akasema, “sawa basi baba mtibu.” Hapo hapo akaingia ndani kumuona mgonjwa. Alianza kutazama vijulisho vyake, akaangalia kichwani akakosa, akaangalia miguuni akaiona mikono, akafahamu kwamba, atapona.

Ndipo wakati huo akamunywesha dawa. Akawaambia kwamba, “nitakuja kumuona wakati Fulani. Akarudi nyumbani na kwenda kukata kuni. Alienda kukata hizo kuni na kurudi jioni. Alienda kumwangalia mjonjwa wake tena na kukuta kuwa hali yake imekuwa nzuri mpaka ameweza kuongea.

Baba huyo aliomba maji akamnywesha tena dawa. Akawaambia kwamba, “kesho asubuhi nitakuja nimuone,” akaenda nyumbani kwenda kulala. Kulipokucha alienda kwenda kumuona tena akamkuta anasimimama na kujaribu kutembea. Familia hiyo aliikuta imefurahi mno. Akamnywesha tena ile dawa, akawaambia tena hivi, “niende jamani nikaende kwenye kuni.” Alikatazwa, “hapana baba, kaa umsikilize mgonjwa.”

Alianza kuwaelezea akisema hivi, “hapana baba nimeacha hali mbaya mno nyumbani.” Mzee alimuuliza “hali mbaya ipi baba uliyoacha?” “Nimeacha hakuna hata chakula nyumbani.”

Baba huyo alichotewa chakula magunia mawili na hela ya kutumia walipelekewa nyumbani. Alikaa pale kwa muda wa siku tatu, akawa amepona kabisa yule mgonjwa wake.

Alianza kujiuliza tena, “sijue ni kwa nani tena?” Akafikiri kuwa kwa mfalme kuna mtoto wake aliyeugua. Siku ya nne, aliwaambia, wa kwenye nyumba hiyo, “jamani nitembee tembee huku kidogo.”

Nao walimkubalia akaanza safari ya kwenda mpaka kwa Mfalme, akafika na kubisha hodi, akayasema maneno hayo mlangoni. Akaambiwa kwamba, “hivyo baba unayafahamu lakini masharti ya Mfalme?”

“Huwa wanauliwa kama ukishindwa kumponyesha mtoto wa mfalme.” Mwanaume huyo, alisema, “sawa tu, si ni kama nimeshindwa.” Basi walimkubalia mlangoni akaingia na akafika huko kwa mfalme. Akamwambia malengo yake.

Alipomwambia mfalme, alipelekwa kwenye nyumba akapitishwa kwa nyuma akiizunguka nyumba, akaoneshwa vichwa vya waganga walioshindwa kumponyesha imezungushwa kuta zote za nyumba. Alipoona alipelekwa kumuona mgonjwa, akafikia kuangalia alama yake anayoitumia na kuona kwamba atamponyesha.

Hapo hapo alianza kumpa dawa, mgonjwa huyo siku mbili, akawa amepona kabisa. Mfalme alifurahi mno akampa zawadi za kila aina. Ikatengenezwa barabara ya kutoka pale mpaka kwake, akajengewa na nyumba. Mungu ni mkubwa, mwanaume huyo, sasa umefika wakati wa utajiri, alikaa muda wa mwezi mmoja hapo.

Mgonjwa akawa mzima na afya ya mwili wake ikamrudia. Hapo akapata zawadi tena, akapewa msichana wa kuoa, basi akawa na wanawake watatu. Alifanyia arusi kubwa mno na mfalme.  Wakazawadiwa si kidogo.

Zawadi nyingine alikatiwa sehemu akawa mfalme. Mwanaume huyo iliisha miaka yake akiwa amejisahau kwa sababu ya kuwa na furaha, akasahau na wazo lake la kujinyonga.

Siku moja akiwa katika safari ya kwenda kutembea na dereva wake, aliwaona watu wanachimba kaburi, akamwambia dreva wake hivi, “umewaona watu hao wanaochimba kaburi?”

Dereva wake alimjibu, “twende tutachelewa.” Ndipo wakakimbia kidogo akaona tena watu wamebeba maiti, akamwambia tena dereva wake, “umewaona watu hao waliobeba maiti?” Dereva alijibu, “wewe nawe, tutachelewa.”

Alikimbia kidogo tena, wakamuona mtu akisimamisha gari yao. Akamwambia dereva, naye akasema, “wewe tutachelewa.” Wakakimbia kidogo tena, wakamuona mtu mbele akisimamisha gari yao, akamwambia tena dereva “simama.” Mwishowe, akasimama kweli.

Mtu huyo alimuliza, “umenifahamu?” Naye alijibu, “hapana sikufahamu.” Mtu huyo alianza kujieleza, “ni mimi yule niliyekukatia kamba shingoni, basi ndiyo kusema bwana, siku zako zimeisha leo, hapo hapo alifariki.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.