sayings

26. Ntemi Bhudoshi na Manyanda

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho ngosha umo lina lyakwe Manyanda. Agading’wa bhusese ugagulwa hikulu, hali Ntemi Bhudoshi. Umu milimo yakwe wali nkomezu no.

Ntemi nang’hwe akantogwa no ung’winha na cheo (bhutale), nose ubhiza ntale o bhasese. Uitanwa nkujiwa wa ntale nsese manyanda (mheshimiwa wa mkuu, mtumwa manyanda).

Kushika nose bhiza bhabyaji bhakwe kunkomola (kung`winja mu bhusese). Aliyo iki cheyo jakwe ijo winhwa akalema. Ubhawila bhabyaji bhakwe giki. “Bhabyaji bhane nalina bhulumbi bhutale no iki ng`wizaga kunikomola, aliyo natajile, na manila no ukunu.” (kulemela mu shibhi)

Huna lulu bhabyaji bhakwe bhandya kulila, nu Nina ung’wila giki ulu walemaga tutibhona nu bhebhe hangi (izumo. Kumb 30:19) Kuhayimanila Ntemi Bhudoshi uzumalika. Mu shiku jene kaliho kajile, ulu ucha Ntemi akujikwa na nganji wakwe (mpaga kuja na nsago).

Lushiku lwene lwa kucha Ntemi, bhanamhala bhakang’witana Manyanda nang’hwe akayega no uhaya, “Lelo nagubhiza Ntemi.” Aho washika bhanamhala bhung’wila, “Lelo ugujikwa uli mpanga, iki kajile kise kali chene, uyo bhitogilwe nu Ntemi akujikwa nang’hwe mpanga.”

Aho Manyanda wigwa agasunduhala no, ugema na kupela aliyo uding’wa utungwa utulwa ng’wichongo.

Ntemi Bhudoshi nang’hwe utulwa higulya, bhandya gufugila, ukunu Manyanda akulilaga mugati. “Ulu ninazunije ya bhabyaji bhane,

ninatapandikile makoye.”

Kiswahili: Mtemi/Mfalme Bhudoshi Na Manyanda

Alikuwepo mwanaume mmoja jina lake Manyanda. Alikamatwa na kupelekwa utumwani akanunuliwa kwenye ikulu, kwa mfalme/mtemi Bhudoshi. Katika kazi zake alikuwa hodari yaani, alikuwa mchapa kazi mno.

Naye Mfalme alimpenda mno, akampa cheo cha ukubwa, mwishowe akawa mkubwa wa watumwa. Akawa anaitwa mheshimiwa wa mkuu mtumwa Manyanda.

Kufika mwishowe wakaja wazazi wake kumkomboa, (kumuondoa kwenye utumwa). Lakini alikataa kwa sababu ya cheo chake alichopewa. Aliwaambia wazazi wake, kwamba,  “Wazazi wangu nina shukrani kubwa mno kwa vile mmekuja kunikomboa, lakini siendi, nimezoea mno huku.” (Alikatalia kwenye dhambi).

Ndipo wazazi wake wakaanza kulia, na mama yake alimwambia kwamba, kama umekataa hatutaonana na wewe tena (laana. Kumb. 30:19).

Kushitukia, Mfalme Bhudoshi alifariki. Kulikuwepo na desturi katika siku hizo, ya kwamba, kama akifa mfalme, atazikwa na mto wa kulalia kichwani (mpaka aende na mto wake).

Siku hiyo ya kufa mfalme, wazee walimwita Manyanda naye alifurahi mno akisema, “Leo nitakuwa mfalme.” Alipofika wazee walimwambia, “Leo utazikwa ukiwa mzima, kwa vile desturi yetu iko hivyo, yule anayependana na mfalme atazikwa naye mzima.”

Manyanda aliposikia hivyo, alihudhunika mno, akajaribu na kukimbia, akashikwa akafungwa na kuwekwa shimoni.

Naye mfalme Bhudoshi akawekwa juu yake, wakaanza kufukia, huku Manyanda akilia ndani. “Kama ningekubali ya wazazi wangu, nisingepata matatizo haya.”

ENGLISH: EMPEROR/KING BHUDOSHI AND MANYANDA

There was a man named Manyanda. He was arrested and sent to slavery purchased at the palace, of the king / governor Bhudoshi. In his work he was brave ie, he was a hard worker.egyptian-slaves

And the king loved him so much, and gave him a great position. He finally became the greatest of the slaves. He was called the master of slaves honorable Manyanda.

At last his parents came to redeem him, (to get rid of slavery). But he refused because of his assigned position. He told his parents, that, “My parents I am very thankful that you came to redeem me, but I do not go, I am very familiar here.” (He remained in sin).

Then his parents began to weep, and his mother told him that, “if you have refused, we would never see you again” (curse Deutronomy 30:19).

Suddenly, King Bhudoshi died. There was a custom in those days that, as the king died, he would be buried by the pillar of the head (until he went with his pillar).

At that time the king died, the elders called Manyanda. He was very happy, saying, “Today I will be the king.” When he came to the elders, they said to him, “Today you are going to be buried alive, as our custom is, the one who was loved by the king will be buried with him.”

When Manyanda heard of it, he was so overwhelmed. He tried and to escape, without succeeding. He was arrested and they restrained him.king

The King Bhugoshi was put on him, and they began to put soils covering the tomb, while Manyanda went in crying. “If I had agreed with my parents, I would have not got these problems.”

25. Ndikumaja Ng`wana Geni

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho ngosha wali wogoha mihayo ya muchalo. Hamo na gupandika mihayo mitale. Ubhabhona bhanhu bhalicha. Huna lulu usamila ng’wipolu. Wigasha shiku ningi moyi. Myenda yushila, nzwili juliha no.

Lushiku lumo bhayanda, bhakaja gujuyela ung’wipolu bhugamona, bhuhaya isaji. Bhogoha na bhandya gupela. Umo wabho ugwa lyunchima linti ucha. Bhangi bhupela mpaga kaya. Bhugabhawila bhabyaji. “Dabhonaga isaji, bhiza bhunsanga ng’wipolu. Bhumona uhaya, “Lufu ludapelagwa.”

Kiswahili: Ntakumalizia Mtoto Wa Geni

Alikuwepo mwanaume aliyeogopa maneno ya kijijini kwake. “Labda nitapata shida kubwa. Akawaona watu wanakufa. Ndipo sasa alihamia porini. Alikaa humo siku nyingi.  Nguo zake zikaisha, nywere zake zilirefuka mno.

Siku moja vijana walienda kutembea porini wakamuona, wakadhani ni kichaa. Waliogopa na wakaanza kukimbia. Mmoja wao alianguka akachomwa na mti akafa.

Wengine walikimbia mpaka nyumbani. Wakaenda kuwaambia wazazi. “Tumeona kichaa, walikuja wakamkuta porini.” Wakamuona wakasema, “Kifo huwa hakikimbiwi.”

ENGLISH: I WILL FINISH YOU SON OF GENI

There was a man who was afraid of words of people in his village. He said, “May be I will get a lot of trouble.” He saw people dying. He moved to the wild. He stayed there many days. His clothes were gone, and his hairs were too long.depression-man

One day the youngsters went to the wild and saw him.  They thought he was crazy. They were afraid of him to the point of beginning to run away. One of them fell and was chopped by a tree to death.

Others ran home. They went to tell their parents. “We have seen a crazy person, they came and found him in the wild.” They saw him  and said, “One cannot run away from Death.”

24. Bhulangwa Wa ng`wa Shetani: Nduhu Wangu Wangu

Sukuma3

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey <a href=”http://www.afriprov.org/”(African proverbs,Sayings and stories)

Bhalangwa bhadatu bhang’wa shetani ntale. Bhali na lubhanza lobhulingisilo na nimo gwabho, gwagubhahubya bhanhu bha musi.

Aho bhamala jigasho jabho jenijo, aha bhatali kubhuka lugendo lwabho lwa kwiza musi kubhakoya bhanhu. Ntale wa bhashetani agabhitana abhalangwa bhakwe na gubhabhuja higulya ya milimo yabho ya gubhalemba lemba bhanhu na gubhajimija umusi.

Nangwa wa kwandya agabhujiwa nilishetani ilitale, “Ee alu bhebhe wina nzila ki?” Agashosha, “Unene nina nzila ja gubhawila abhanhu uko Welelo giki, uMulungu atiho.”

Ushetani ntale ushosha, “Uko nzila yako yeniyo ugubhapandika bhanhu bhagehu duhu, kulwa nguno amaganiko gabhanhu gakubhamanyikijaga giki uMu1ungu aliho ng’hana.”

Agamuja uwa kabhili, “Alu bhebhe wina nzila ki?” Agashosha, “Nagubhawila giki, umoto gwa welelo na welelo nduhu, ili mihayo ya bhulomolomo gete.”

Untale wakwe aganshogeja. “Ku nzila iyi ugubhalemba lemba bhagehu duhu. Kulwa nguno hihi pye abhanhu umukwiganika gwabho, bhamanile giki, bhanhu bhagulamulwa gulenganila na shitwa shabho.”

Ha ng`halikijo, agabhujiwa nu nangwa wa kadatu. “Alu bhebhe ginehe?” “Unene nagubhawila abhanhu giki, Wangu wangu nduhu. Iti hadi ukulumva lelo, nulu ikanza linili, nulu ntondo bhungi, nulu ng’waka uyo guliza.

Nduhu Wangu Wangu.” Ntale wa mashetani akayejiwa no nilishosho lyakwe, uyomba, “Ijigasho jeniji jingilaga muntwe gwako ng’hana, ukunzila yeniyi ugubhapandika bhalangwa bhingi no.

Swahili: Mafundisho Ya Shetani – Hakuna haraka

Wanafunzi watatu wa shetani mkubwa. Hao walikuwa na kikao cha kupanga mikakati ya kutekeleza lengo lao, la kuwakosesha watu wa duniani.

 Walipomaliza kikao chao hicho, wakiwa bado hawajaanza safari yao ya kuja duniani kuwasumbua watu. Mkuu wa mashetani aliwaita wanafunzi wake na kuwauliza juu ya kazi yao ya kuwadanganya watu na kuwapoteza duniani.

Mwanafunzi wa kwanza aliulizwa na shetani mkubwa, “Wewe una njia ipi?” Alijibu, “Mimi nina njia ya kuwaambia watu hivi ulimwenguni, Mungu hayupo.”

Shetani mkubwa alijibu, “Kwa njia yako hiyo utawapata watu wachache tu, kwa sababu mawazo ya watu yanawajulisha hivi, Mungu yupo kweli.”

Akamuuliza wa pili, “Na wewe una njia ipi?” Alijibu, “Nitawaambia kwamba, moto wa milele haupo, ni maneno ya uongo kabisa.”

Mkubwa wake alimjibu, “Kwa njia hii utawadanganya wachache tu. Kwa sababu karibu watu wote katika kufikiri kwao, wanajua hivi, watu watahukumiwa kulingana na matendo yao.”

Mwishoni, alimuuliza na yule wa tatu, “Na wewe una njia ipi?” Alijibu, “Mimi nitawaambia watu hivi, hakuna haraka. Siyo lazima kuungama leo, au muda huu, au kesho kutwa, au mwaka ujao. Hakuna haraka.”

Mkuu wa mashetani alifurahishwa mno na jibu lake, alisema, “Kikao hiki kimeingia kichwani mwako kweli, kwa njia hii, utawapata wanafunzi wengi mno.”

THE ENGLISH TITLE OF THIS SUKUMA STORY IS “THE HEAD DEVIL TEACHES HIS DISCIPLES”

Nduhu wangu wangu. (Sukuma)
Hakuna haraka. (Swahili)
Pas besoin de courir, prens-le modément. (French)
There is no rush. Take it easy. (English)

There is a Sukuma story called The Head Devil Teaches His Disciples. The original Sukuma is Bulang’wa wa Ng’wa Shetani and can be found on their teachings.

The teaching of this Sukuma story is that there are three different ways by which a false teacher can deceive and confuse people regarding the urgency of salvation. The first way is to say that there is no God. The second way is to say that there is no hell.

The third way, and most effective, is the advice that includes the saying Nduhu wangu wangu (There is no rush. Take it easy). This is the devil’s way of deceiving us into delaying to make necessary changes in our lives, to put off repentance, not to take care of our spiritual life and to forget about God.

This saying is stated in the negative – an example of the elusiveness and paradox of African proverbs and sayings that often teach through opposites.

23. Ng`wana Nkuba Na Padri

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Lushiku lumo ng’wana Nkuba bhali na Padri bhakwihalalijaga giki, ‘Ubhebhe ng’wana Nkuba iki ugenhaga mbula gemaga ulu igunipandika mu nzila.”

Ng’wana Nkuba uhaya igugupandika ni Ngudu utali ugushiga. Padri uhaya, “Nagugwinha shilingi jihumbi jimo, ulu mbula yunipandika mu nzila.

Ng’wana Nkuba uhaya nang’hwe, “Ugusola ng’ombe ulu idugupandika.” Padri ubacha gali yakwe ulaga na guja. Ng’wana Nkuba ugasoseja ijibhiga jakwe nang’hwe, ikanza idololo mbula yandya kutula nu padri adinashiga ni Ngudu.

Igali yukwama mutembe. Ulomba bhanhu bhakungwambilija ifunyiwe. Aho yafuma padri ushoga kuli Ng`wana Nkuba gung’winha ishilingi jihumbi jimo. Padri na kumala kuzunya, ng`hana idulile.

Kiswahili: Mwana Wa Nkuba Na Padri

Siku moja Mtoto wa Nkuba, au mwana wa Nkuba, walikuwa na Padri wakibishana kwamba, “Wewe Mwana wa Nkuba, si unaleta mvua jaribu kama itanikuta njiani.”

Mwana wa Nkuba, alisema, “itakukuta hata kabla ya kufika Ngudu.” Padri alisema, “Nitakupa shilingi elfu moja, kama mvua itanikuta njiani.”

Mwana wa Nkuba, alisema naye, “utachukua Ng’ombe kama haitakukuta njiani.” Padri aliwasha gari yake, akakimbia kwa kasi. Mwana wa Nkuba, alichochea kijungu chake, muda mfupi ikaanza kunyesha mvua kabla hata Padri hajafika Ngudu.

Gali ikakwama kwenye matope. Akaomba watu wa kumsaidia aiondoe. Ilipotoka padri alirudi kwa mwana wa Nkuba, kumpa shilingi elfu moja. Padri alikubali kweli inawezekana.

ENGLISH: SON OF NKUBA AND PRIEST

One day the son of Nkuba, or Nkuba’s son, had a priest arguing that, “You Son of Nkuba, if you can bring rain try if it catch me along the way.”statue priest one

The Son of Nkuba said, “It will find you even before you reach Ngudu.” Priest said, “I will give you one thousand shillings, if the rain finds me along the way.”

Nkuba’s son said to him, “if it does not find you on the way you will take a cow.” Priest started his car, and ran away faster. The Son of Nkuba, stirred up fire in his pot, shortly it began to rainy before even the priest reaching Ngudu.male-2101801__340

The car fell into the mud. He asked the people to help him in getting rid of it. When he came out of the mud the priest returned to Nkuba’s son, giving him a thousand shillings. The priest accepted the truth.

 

22. SAYAYI, NYAMHAWA, MHALA NI MBITI

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Lushiku lumo muna Lung’wando ubhawila bhiye giki, “Nishindikilagi kubhukwingwa, aliyo tuje na sunge, bhuli ng’wene bhubhucha. Muna Mbiti atabhukije. Aho bhashika mu mapolu muna Mbiti ubhawila bhatongele nang’hwe ushoka kaya ya ng’wa Lung’wando na kaya ya ng’wa Jidivi na ya ng’wa Sala, ukasola bhana bhabili bhabhili bhuli kaya. Utunga ifulushi sunge wiza ubhawila ku bhucha isunge yeniyo bhumanhya na bhanhu ugishiwa muna Mbiti. “Ng’wadila muna juchu, madilo ng’wana juchu, madilo miza bhanga na bhagubhuchaga nigo na kumana yaya.rabbit

Muna Lung’wando wiganika gete, ung’wila muna mbiti atongele bhifule iki atina nigo uwei. Utongela muna Mbiti, aho bhasula umu nigo bhubhabhona bhana bhabho. Ubhashosha ukabhenha bhana bha mbiti.

Lung’wando utunga ifulushi muna jidivi wimila ha jifulu, unola muna mbiti ulu washika bhuja bhukampandika. Bhumanhya na bhanhu, ugisha muna Mbiti, madilo juchu, madilo na bhimila bhakubhuchaga unigo na kumana yaya. Ugishiwa lung’wando, madilo muna juchu madilo nakatunga nu shashanija umo watungile uwe.

Ugishiwa muna Sala, madilo muna juchu madilo nakimanikila nushisha bhane ugishi

wa muna Jidivi madilo muna juchu, madilo nakima na jigulu nilolekeja iki nali nyagokolo ubhuja muna mbiti, nigwa ng’wana juchu, yaya masemba duhu. Bhushika ng`hana gubhukwiye ya Lung`wando bhusung’anhwa na bhakwelaye bhandya kulya, muna mbiti ugwa ng’hana ng’wana juchu yaya masemba duhu.

Bhulagwa kuja kaya muna mbiti usanga bhana bhakwe bhalinduhu, bhatandatu. Umana giki bhabhalile uko bhugeni ukamuja muna Lung’wando bhana bhane wabhachalile ku bhukwiyo, ukagema sunge, lelo nakukulya nu bhebhe yaya muna juchu.

Nakulipa nyama tukwisangila kwibambasi dilu. Aha wela Muna Sayayi ubhasanga bhana mhuli bhagulyaga masindi, ulipundulila lisindi limo wingila moi, ili tula mbula, Mhuli imo ulimila ilisindi linilo, wingila munda ya mhuli, muna Sayayi alina silimbi ufula, bhiwila abhana Mhuli tulekanagi tumane uyo agufulaga silimbi.

Ufula hangi Sayayi bii! Bhana Mhuli bhumulaga ung’wichabho, uwei ufuma agupelaga umuna Lung`wando, kujung’wila muna mbiti, giki, “tujagi ku nyama na bhulagaga.” Wandya gulya umuna mbiti gushila na mhayo.

 Kiswahili: Sungura, Mbweha, Paa na Fisi

Siku moja Sungura aliwaambia wenzake hivi, “Nisindikizeni kwa wakwe zangu, lakini tuende na mzigo,” wengine wakabeba, lakini Fisi hakubeba. Walipofika porini Fisi aliwaambia watangulie naye akarudi nyumbani kwa Sungura na kwa mbweha na Paa au Swala, akachukua watoto wawili wawili kwenye kila familia.

Alifunga fulushi la kupeleka kama mzigo wake akawaambia wabebe mzigo huo. Akakutana na watu akasalimiwa Fisi. “Habari za jioni bwana, habari za jioni bwana, habari ni nzuri, wamebeba mzigo bila kujua.

Sungura alifikiri kabisa, akamwambia Fisi, atangulie wapumzike kwa vile yeye hakuwa na mzigo. Fisi akatangulia, wakachungulia kwenye mzigo wakawaona watoto wao. Wakawarudisha na badala yake, wakawaleta watoto wa Fisi.

Sungura alifunga fulushi, mbweha akasimama kwenye kichukuu, akamchungulia Fisi alikofika, wakaenda mpaka wakampata. Wakakutana na watu, akasalimia Fisi, habari za jioni bwana, habari za jioni, wakasimama wakiwa wamebeba mzigo bila kujua.

Akasalimiwa Sungura, habari za jioni bwana, nimeufunga kama alivyofunga yeye. Alisalimiwa Swala au Paa, habari za jioni bwana, habari za jioni, nilishitukia, nikafikisha watoto wangu.

Akasalimiwa na Mbweha, habari za jioni bwana, habari za jioni, nilisimama kwenye kichuguu nikajionea kwa vile ni mvivu. Akauliza Fisi, nimesikia bwana, hapana michezo tu. Wakafika kweli kwa wakwe zake Sungura, wakapokelewa na shemeji zake, wakaanza kula, Fisi alianguka kweli bwana, hapana utani.

Waliagwa kwenda nyumbani, Fisi alipofika nyumbani, hakuwakuta watoto wake sita. Akafahamu kwamba, wamewala kule ugenini, akamuuliza Sungura “watoto wangu waliwapeleka kwa wakwe zako, akajaribu mzigo wa kupeleka huko, leo nitakula wewe.”

Sungura lisema, “Hapana bwana. Nitalipa nyama tutakutana jangwani asubuhi.” Kesho yake, aliwakuta Tembo wakila mamung’unya, jamii ya tikiti maji, akatoboa na kuingia kwenye mung’unya mojawapo tembo akalimeza, wakati huo mvua ilikuwa inanyesha. Akaingia kwenye tumbo la Tembo, Sunguru akiwa na filimbi. Akapuliza, Tembo wakaelezana tuachane ili kumfahamu yule anayepuliza hiyo filimbi.

Akapuliza tena Sungura bii! Tembo wakamuua mwenzao. Akatoka humo sungura akikimbia, kwenda kumwambia Fisi kwamba, “twende kwenye nyama, nimeua.” Fisi akaanza kula, neno likaisha.

ENGLISH: RABBIT, FOX, ANTELOGY AND HYENA

One day Rabbits told his colleagues, “Escort me to my grandparents, but let us go over with loads,” some carried, but hyena did not carry it. When they came to the forest hyena told them to go ahead of him. He returned to their house and took two children in each family.

He fastened his luggage for sending and told them to carry it. He met people who greeted with Hyena. “Good evening mr, it is good, the news is good, they have carried a cargo without knowing.”

The rabbit thought absolutely, he said to the hyena, that he should go ahead of them, they rested because he did not have a burden. When the hyena left, they looked at the load and saw their children. They brought them back and instead, they brought the children of the hyena.

The rabbit scrubbed the hyena, the fox stood in the lighter, watched the hyena coming, and went on till they found him. They met the people, greeted Hyena, good evening mr, good evening, stood barely loaded with burdens without knowing.

The Rabbit was greeted, “good evening e sir,” I have closed up as he closed. The other was greeted, “good evening sir, good evening,” I was shocked, I have reached my kids here.

He was greeted by Fox, “good evening sir, good evening, and I was stood on the countryside felt discouraged. He asked Hyena, I heard the master, there was no games. He came to his grandparents at the rear, when he was received by his sisters in law.  They began to eat, hyena fell true, sir, there is no jokes.

They said goodbye on their way home, when hyena came home, did not find his six children. He knew that, when he was in control of the village, he asked the rabbit “you took my kids to your grandmother, and tried to load the truck there, today I will eat you.”

The rabbit says, “No sir. I will pay the meat we shall meet in the desert in the morning” The next day, he found an elephant feeding kind of water melon, he made on hole in it and entered into it. The elephant swallowed it. It was raining, while the rain was over. He went into the elephant’s stomach, Rabbit with a whistle. He shot, elephants split each other apart to get to know who blows the whistle.

Rabbit whistled again bii! Elephants killed their partner. Rabbit went out of there running, going to tell Hyena, “go to the meat, I have killed.” The hyena began to eat, the word disappeared.