Riddles

957. KALAGU – KIZE. DINA MAYU DUGANISHAGA ALIYO ADIGUTAGA – SI.

Ikalagu yiniyo, ilolile Si. Isi yiniyo, igabhabhuchaga abhanhu ulu bhabyalwa umusi munumu, na igabhamilaga ulu bhagaya bho gujikwa. Abhanhu bhagachaga bhuli makanza bhajikwa aliyo idigutaga. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “dina mayu duganishaga aliyo adigutaga – Si.”

Ikalagu yiniyo, igatumilagwa kuli munhu uyo agitilagwa ya wiza na nina aliyo uweyi adayimanile, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adabhumagana uwiza bho gubyalwa nu mayu okwe ng’wunuyo, kunguno ya gwiganiga giki weng’hwa gupandika makoye duhu umusi munumu. Uweyi olalaga mumagulu ga ng’wa mayu okwe na gub’uchiwa kungungo, aliyo agalilaga duhu ulu omisha kunguno ya guduma ugubhudebha uwiza ubho agang’witilaga, umayu okwe ng’wunyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oyidukaga Isi giki igamilaga bhanhu aliyo bhagayipandagilaga iyo igafunyaga na wasa bho gubhabhika ulu bhalijikwa, kunguno nuweyi adabhumanile uwiza bho ng’wa nina uyo omyala na gunkuja, umukikalile kakwe. Hunagwene aganhalamikilaga bho guyomba giki, “dina mayu duganishaga aliyo adigutaga – Si.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kubhudebha uwiza ubho bhitilwa na bhabyaji bhobho, ubho bhulikihamo nubho gubhenha kuwelelo na kubhalanhana mpaga bhugakula chiniko, kugiki bhadule gubhalumba abhabyaji bhenabho bho gubhakuja na gulanghana chiza, umuwikaji bhobho.

Luka 12:15.

Kumbukumbu la Torati 30:15.

Marko 16:1-8.

1Wakorintho 15:20-22.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

TUNA MAMA TUNAMLISHA LAKINI HASHIBI – ARDHI.

Kitendawili hicho, huangalia Ardhi. Ardhi hiyo, huwabeba watu wanapozaliwa duniani humu, na wanapofariki huwameza kwa njia ya kuzikwa. Wanaokufa na kuzikwa ni wengi lakini yenyewe haishibi. Ndiyo maana watu husema kwamba, “tuna mama tunamlisha lakini hashibi – Ardhi.”

Kitendawili hicho, hutumiwa kwa mtu yule ambaye hutemdewa wema na mama yake mzazi lakini hautaumbui wema huo, katika maisha yake. Mtu huyo, hautambui wema wa mama yake ambao ni pamoja na ule wa kumzaa na kumkuza, kwa kumlaumu kwamba, alimleta duniani kuteseka tu. Yeye alilala kwenye magoti ya mama na kubebwa mgongoni ng’wa mama yake, bila kusahau kumlaza aliposinzia, lakini yeye aliamuka na kulia, kwa sababu ya kushindwa kuutambua wema huo wa mama yake huyo mzazi, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeilaumu Ardhi akidai kwamba inameza watu wakati kuwazika, kwa kutokufahamu kuwa hilo ni tendo la upendo, kwa sababu naye hautambui wema wa mama yake mzazi aliyemzaa na kumkuza, katika maisha yake. Ndiyo maana humlaumu kwa kusema kwamba, “tuna mama tunamlisha lakini hashibi – Ardhi.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuutambua wema waliotendewa na wazazi wao, ambao ni pamoja na ule wa kuwaleta duniani, na kuwatunza mpaga wakawa watu wazima, ili waweze kuwashukuru kwa kuwaheshimu na kuwatunza vizuri, maishani mwao.

Luka 12:15.

Kumbukumbu la Torati 30:15.

Marko 16:1-8.

1Wakorintho 15:20-22.

cemetery-

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE- LET IT COME.

I HAVE A MOTHER WHOM WE FEED BUT SHE IS NEVER SATISFIED – LAND.

This riddle looks at the Land. This land carries people when they are born on this earth, and when they die it swallows up them during their burial. The people who die and be buried are many but it does get satisfied. That is why people say that, “I have a mother whom we feed but she is never satisfied – land.”

This riddle is applied to the person who is treated kindly by his or her mother but he does not realize that kindness in his or her life. This person does not recognize the goodness of his mother which includes the birth and rearing of his/her. He/she lay on her mother’s knees and was carried on her mother’s back. This mother made this person sleep well who fails to recognize the goodness of his/her mother, in life.

This man is like the one who blamed the Earth by claiming that it swallows people when they are buried, not realizing that it is an act of love, because he also does not recognize the goodness of his biological mother, in his life. That is why he/she blames her by saying that, “I have a mother whom we feed but she is never satisfied – land.”

This riddle imparts in people a clue on how to recognize the good deeds which were done by their parents, which include bringing them into the world, and caring for them as adults, so that they can thank them by respecting and taking good care of them, in their lives.

Luke 12:15.

Deuteronomy 30:15.

Mark 16: 1-8.

1 Corinthians 15: 20-22.

953. KALAGU – KIZE. ISONGA LYANE ULU LYINGA LIDALASHOGA – LINO.

Ikalagu yiniyo ihoyilile lino. Ilino ilya ng’wa munhu untale ulu lyinga didalashoka, kunguno ligadubukaga pye ni mizwi yalyo. Ilyoyi ulu lyinga mumho ogayiyagwa duhu ung’winikili olyo. Hunagwene agayombaga giki, “isanga lyane ulu lyinga lidalashoga – lino.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalitumila chiza ilikanza lyakwe, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunyo, agipunaga dilu oja kumilimo yakwe, ogigulambija guitumama chiza, kunguno ya gudebha isolobho ya likanza lyakwe linilo, umukikalile kakwe. Uweyi agaponaga majiliwa mingi noyi, kunguno ya bhukamu bhokwe ubho gulitumila chiza ilikanza lyakwe linilo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo adadulile ugulishosha ilino lyakwe ilolyingaga, kunguno nuweyi, adadulile ugulishosha numa ilikanza lyakwe ilo agalitumilaga bho gwigulambija gutumama milimo yakwe yiniyo, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “isonga lyane ulu lyinga lidalashoga – lino.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanza lyabho bho gwigulambija gutumama milimo, kugiki bhadule gupandika sabho ningi, umuwikaji bhobho.

2Wakorintho 4:16-18.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MSHALE WANGU UKITOKA HAURUDI – JINO.

Kitendawili hicho, huongelea juu ya jino. Jino la mtu mzima liking’oka huwa halirudi, kwa sababu huwa linang’oka na mizizi yake. Lenyewe liking’oka ndiyo kusema, mwenye jino hilo amekosa. Ndiyo maana husema kwamba, “mshale wangu ukitoka haurudi – jino.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huutumia vizuri muda wake, katika maisha yake. Mtu huyo, hujilawa asubuhi kwenda kwenye kazi zake, na kuzitekeleza kwa bidii kubwa, kwa sababu ya uelewa wa faida ya muda wake huo, katika kujiletea maendeleo. Yeye hufanikiwa kupata mafanikio mengi zaidi katika kazi zake, kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kuutumia vizuri muda wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule alisiyeweza kulirudisha jino lakwe lililo ng’oka, kwa sababu naye hawezi kuurudisha nyuma muda wake anaoutumia kwa kujiletea maendeleo, katika maisha yake. Ndiyo maana husema kwamba, “mshale wangu ukitoka haurudi – jino.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuutumia vizuri muda wao kwa kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi, maishani mwao.

2Wakorintho 4:16-18.

fisherman

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE- LET IT COME.

MY ARROW WHEN GOES OUT IT NEVER COMES BACK – A TOOTH.

This riddle talks about an uprooted tooth. When an adult’s tooth is taken out, it does not return, because it is always rooted. The very thing that can be said is that the owner of the tooth has missed it. That is why the owner says that, “If my arrow goes out it does not come back – tooth.”

This riddle is related to the person who spends nicely most of his time in life. Such person, in the morning, goes to work, and performs it with great diligence, because of being aware of the benefits of his time, in bringing about development. He succeeds in achieving greater success in his endeavors, because of his diligence in using well his time in life.

This person is like the one who was unable to bring back his uprooted tooth, because he also cannot regain the time he spends for development, in his life. That is why he says that, “If my arrow goes out it does not come back – tooth.”

This riddle imparts in people an idea on how to use their time well by striving to fulfill their responsibilities, so that they can have more success in their lives.

2 Corinthians 4: 16-18.

947. KALAGU – KIZE. HIGULYA IKUB’I, AHA GATI LUKWI, AHA HASI JILIWA – NH’OGO.

Ikalagu yiniyo, ilolile nh’ogo. Unh’ogo gunuyo, guli nti uyo gugatumilagwa na bhanhu gwingila gumadutu mpaga ku mizwi yago. Ugoyi guli na solobho nhale ukubhanhu kunguno amadutu gago gali makub’i, imiti yili ng’hwi, imizwi yago yili jiliwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “higulya ikub’i, aha gati lukwi, aha hasi jiliwa – nh’ogo.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ng’wiza nholo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhambiljaga chiza abho bhali na makoye bho gutumila sabho jakwe, kunguno ya welwa nholo bhokwe bhunubho. Uweyi agayegaga na bhanhu bhingi abho agabhambilijaga kunguno ya bhutogwa na wiza nholo bhokwe bhunubho ukubhoyi, umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nh’ogo uyo gugambilijaga bhanhu bhingi gwingila ku madutu gago mpaga kumi mizwi yago, kunguno nuweyhi agambilijaga bhanhu bhingi abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “higulya ikub’i, aha hagati lukwi, aha hasi jiliwa – nh’ogo.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gub’iza bhiza nholo umukikalile kabho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza, umuwikaji bhobho.

Yoshua Bin Sira 4:1-4.

Mathayo 25:31-46.

Waebrania 12:2-3.

Waebrania 13:1-3.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

JUU MBOGA, KATIKATI KUNI, CHINI CHAKULA – MUHOGO.

Kitendawili hicho, chaangalia muhogo. Muhogo ni mti unaotumiwa na watu kuangia kwenye majani hadi kwenye mizizi yake. Mti huo, una faida nyingi kwa watu kwa sababu, majani yake ni mboga, miti ya matawi yake ni kuni na mizizi yake ni chakula. Ndiyo maana watu husema kwamba, “juu mboga, katikati kuni, chini chakula – muhogo.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkarimu, katika maisha yake. Mtu huyo, husaidia watu walioko kwenye matatizo kwa kutumia mali zake, kwa sababu ya ukarimu wake huo. Yeye hufurahi na watu wengi aliowasaidia kwa sababu ya upendo na ukarimu wake huo kwao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule muhogo uliosaidia watu wengi kuanzia kwenye majani hadi kwenye mizizi yake, kwa sababu naye huwasaidia watu wengi walioko kwenye matatizo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “juu mboga, katikati kuni, chini chakula – muhogo.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwasaidia wale walioko kwenye matatizo, katika maisha yao, ili waweze kusaidiana vizuri, katika kuyatatua matatizo yao hayo, maishani mwao.

Yoshua Bin Sira 4:1-4.

Mathayo 25:31-46.

Waebrania 12:2-3.

Waebrania 13:1-3.

cassava-leaves-

 

ENGLISH:  I HAVE A RIDDLE- LET IT COME.

THE TOP PART OF IT IS VEGETABLE, THE MIDDLE PART IS FIRE WOOD AND ITS ROOT IS FOOD – CASSAVA PLANT.

This riddle looks the cassava. Cassava is a tree that people use to get to the leaves to its roots. This tree has many benefits for people because its leaves are a vegetable, its branches are fire woods and its roots are food. That is why people say that, “high vegetables, in the middle the fire wood, low food – cassava plant.”

This riddle is related to the person who is generous to others in life. This person helps people who are in need by using his or her resources, because of his or her generosity. He/she rejoices with a good number of people whom he/she has helped because of his/her love and generosity toward them, in life.

This person is like the cassava that helped many people from the leaves to the roots, because he/she also helps many people who are in trouble, in life. That is why people tell him/her that, “high vegetables, in the middle the fire wood, low food – cassava plant.”

This riddle imparts in people an idea on how to be generous in helping those who are in great need, so that they can help each other enough to easily solve their problems, in their lives.

Joshua Bin Sirach 4: 1-4.

Matthew 25: 31-46.

Hebrews 12: 2-3.

Hebrews 13: 1-3.

941. KALAGU – KIZE. UNTEMI AHEB’ILWE NA B’IKAJI BHAKWE – NG’WI O WALWA.

Ikalagu yiniyo, ilolile ng’wi o walwa. Ung’wi o walwa ng’wunuyo, ali munhu uyo agang’waga walwa mpaga gab’ipa amasala gakwe. Uweyi agahewagwa nu walwa bhunubho kunguno gagagaluchaga amasala gakwe bho wandya kuchola likenya nulu guyugwa sagala, mpaga wiminya, ulu ubhung’wa. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki “untemi aheb’ilwe na b’ikaji b’akwe – ng’wi o walwa.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajitumilaga nyalaku ijikolo jakwe mpaga jang’wenhela makoye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agapangikaga sabho nulu hela, ojikenagaula sagala mpaga jantuula mu makoye kunguno ya bhulaku na jilangu jakwe jinijo. Uweyi agakoyiyagwa na makoye bho likanza lilihu ayo gagenhagwa na bhukenjai bho jikolo jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wi o walwa uyo agang’waga walwa mpaga gab’ipa amasala gakwe, kunguno nu weyi agajikenagulaga sagala ijikolo jakwe mpaga jang’wenhela makoye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “untemi aheb’ilwe na b’ikaji bhokwe – ng’wi o walwa.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya kuleka bhulaku bho bhung’wi bho walwa, na bhukenaguji sagala bho sabho jabho, kugiki bhadule gujilang’hala chiza isabho jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 9:18-23.

I Wakorintho 10: 4 – 7.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MFALME WANAMSHINDA WAKAZI WAKE – MLEVI WA POMBE.

Kitendawili hicho, chaangalia mlevi wa pombe. Mlevi huyo wa pombe ni mtu anayekunywa pombe mpaga akili yake inaharibika. Yeye hulemewa na pombe hiyo kwa sababu akili yake hubadilika na kuwa mbaya akiinywa. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mfalme wanamshinda wakazi wake – mlevi wa pombe.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvitumia kwa ulafi mali zake mpaga zinamletea matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hupata mali na hela na kuziharibu hovyo mpaga zinamuingiza kwenye matatizo mengi kwa sababu ya ulafi wake huo. Yeye husumbuliwa kwa muda mlefu na matatizo hayo yaliyoletwa na utumiaji wake huo mbaya wa mali hizo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mlevi wa pombe aliyekunywa mpaka akili yake ikawa mbaya, kwa sababu naye huvitumia hovyo mali zake, mpaka zinamuletea matatizo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mfalme wanamshinda wakazi wake – mlevi wa pombe.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya ulafi wa kung’wa pombe, na utumiaji hovyo wa mali zao, ili waweze kuzitunza vizuri mali zao hizo, maishani mwao.

Mwanzo 9:18-23.

I Wakorintho 10: 4 – 7.

alcohol-1

alcohol-gel-1

model-eyes

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

THE KING IS OVERCOME BY HIS RESIDENTS – AN ALCOHOL DRINKER.

This riddle looks at an alcoholic person. This alcoholic is a person who drinks alcohol to the point of mental retardation. This person becomes addicted to alcohol because his/her mind changes as he/she drinks it. That is why people say to him that, “the king is overcome by his residents –an alcohol drinker.”

This riddle is likened to a man who overindulges in his possessions in life. This man acquires property and money and squanders them, to the point of getting into a lot of trouble because of his greed. He suffers for a long time from these problems which have been caused by his misuse of these properties in his life.

This man resembles the alcoholic person who drank until his mind became bad, because he also wastes his resources, until they cause him problems, in his life. That is why people say to him that, “the king is overcome by his residents – an alcohol drinker.”

This riddle instills in people an idea of having abstinence from alcohol abuse and the misuse of their possessions, so that they can nicely manage their possessions in their lives.

Genesis 9: 18-23.

I Corinthians 10: 4-7.

 

940. KALAGU – KIZE. NG’WISHIGU ALIYO ADIOGUSEJIWA – LIJIGANGA.

Ikalagu yiniyo ihoyelile lijipanga. Ilijiganga liniyo, lili liwe litale ilo lidasegejiyagwa na mhunhu oseose kunguno lyasumva chene. Ilyoyi lili lidito ilo lidilyagushingisha nulu hado nu nshindiki olyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “ng’wishigu aliyo adiogusegejiwa – lijiganga.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agadimilaga nhungwa ja wiza bho nduhu ugutinginyiwa na munhu ose ose, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alemile ugugaleka amiito gakwe agawiza mumo bhagang’witila abhanishi bhakwe, kunguno agapandikaga mbango ja gufumila kuli Mulungu uyo ang’wisanije, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’winuyo, agikolaga ni liwe ilo lidasegejiyagwa na oseose, kunguno nuweyi alemile uguyileka imihayo iya nhana, umukikalile kakwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhakwe guyidimila imihayo ya ng’wa Mulungu bho kikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ng’wishigu aliyo adiogusegejiwa – lijiganga.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gudimilaga chiza inhungwa ja wiza bho gunzunya na gung’wisanya Mulungu shigu jose, kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala chiza na bhichabho, umuwikaji bhokwe.

Waefeso 6:10 – 17.

Wagalatia 5:1.

Tito 2:1-2.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

YU IMARA LAKINI HASOGEZWI – MWAMBA.

Kitendawi hicho huongelea Mwamba. Mwamba huyo, ni jiwe kubwa ambalo halisogezwi na mtu kwa sababu limeumbwa hivyo. Lenyewe ni zito lisilo tigiswa hata kidogo na msukumaji wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “yu imara lakini hasogezwi – mwamba.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huishikiria tabia njema bila kutikishwa na mtu, katika maisha yake. Mtu huyo, hataki kuyacha matendo yake mema hata maadui zake wamtigise kiasi gani, kwa sababu hupata Baraka kutoka kwa Mungu amwaminiye ambazo humsaidia kuyashikiria mema hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na lile jiwe lisilosogezwa na yeyote, kwa sababu naye hataki kuiacha tabia yake hiyo njema yimwezeshayo kuishi maisha mema, maishani mwake. Yeye huwafundisha watu wake namna ya kuyaishi maneno ya Mungu kwa njia a maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “yu imara lakini hasogezwi – mwamba.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuyaishi maadili mema kwa kumwamini Mungu siku zote, ili waweze kupata Baraka za kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao.

Waefeso 6:10 – 17.

Wagalatia 5:1.

Tito 2:1-2.

 

stone-11

stone-12

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

HE IS STRONG BUT NOT MOVED – A ROCK.

This riddle speaks of the Rock. This rock is a huge stone that cannot be moved by any one because it was created in that way. It is heavy to the point of not being moved by its pushers. That is why people say that, “He is strong but not moved – a rock.”

This riddle is compared to a person who adheres to good manners without being shaken by anyone in life. Such person does not want to give up his/her good works no matter how much his/her enemies may scare him/her, because he/she receives blessings from a God who helps him/her enough to hold on to live that good life.

This person is like a stone that no one can move, because he also does not want to give up his good character that enables him to live a good life with others. He teaches his people on how to live the word of God through his life. That is why people say to him that, “He is strong but not moved – a rock.”

This riddle imparts in people an idea on how to live morally by trusting in God at all times, so that they may receive blessings of living well with one another in their lives.

Ephesians 6:10 – 17.

Galatians 5: 1.

Titus 2: 1-2.

coast-rock