Sukuma Proverbs

746. BHUTA BHINZIKA UNDEKELE LUGE LWANE.

Ulusumo lunulo lwingine kuli munhu uyo agalingaga ndimu bho gutumila bhuta na masonga. Ubhuta bhunuyo guli nti uyo gugagondagwa bho gutungilwa luge lo ndimu, ulo agaludutaga unasi bho gutumila lisonga naolasa.

Ubhuta bhunubho, bhudulile gubhinzika kunguno ya gubhugonda bho gutumila luge. Ulubhubhinzika unasi agupandika bhungi kunguno uluge osagaga nalo. Hunagwene agayombaga giki, “bhuta bhinzika undekele luge lwane.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ochilagwa na ng’wana okwe. Umunhu ng’uwunuyo agapinihalaga noyi kunguno ya kuzumalikilwa na ng’wana okwe ng’wunuyo. Abhanhu bhaganungujaga bho gung’wila giki, agubyala ng’wana ungi kunguno nuweyi alihoyi.

Ung’wana ng’wunuyo, agikolaga nu bhuta ubho bhugabhinzikaga, kunguno nu ng’wana ozumalikaga. Ulu luge, lugikolaga nu nina ong’wana, kunguno nuweyi iki osagaga adulile gubyala ng’wana ungi. Hunagwene abhanhu bhagayomgaga giki, “bhuta bhinzika undekele luge lwane.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho guchola nzila ja guginja amakoye ayo bhalinago, umukikalile kabho, na gubhalunguja bhichabho abho bhatali mumakoye, kugiki bhadule guyega kihamo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 2:18-23.

Marko 10:7.

UPINDE VUNJIKA UNIACHIE UGE(KAMBA YA MSHIPA WA MNYAMA) WANGU.

Methali hiyo ilianzia kwa mtu aliyekuwa akiwinda wanyama kwa kutumia upinde. Upinde huo ni mti ambao hukunjwa kwa kufungwa uge au mshipa wa mnyama, ambao huvutwa na mwindaji kwa kutumia mshale ndipo ana urusha mshale wake anapoachia.

Upinde huo unaweza kuvunjika kwa sababu ya kukunjwa na uge au kamba ya mshipa  wakati wa kuurusha mshale huo. Upinde huo ukivunjika mwindaji hupata mwingine kwa sababu amebaki na ile kamba ya mshipa. Ndiyo maana husema, “upinde vunjika uniachie uge au kamba yangu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye amefiwa na mtoto wake. Mtu huyo, huhudhunika sana, kwa sababu ya kuachwa na mtoto wake huyo wa pekee kwake. Watu humfariki kwa kumwambia kwamba, atazaa mtoto mwingine kwa sababu yeye yupo.

Mtoto huyo hufanana na upinde ambao huvunjika, kwa sababu naye mtoto amefariki. Uge au kamba hiyo ya mshipa hufanana na mama mzazi wa mtoto, kwa sababu naye amebaki kwa hiyo, anaweza kuzaa mtoto mwingine. Ndiyo maana watu husema kwamba, “upinde vunjika uniachie uge au kamba yangu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilifu wanapopatwa na matatizo, na kuwafariji wenzao, ambao bado wako kwenye matatizo ili waweze kuishi kwa furaha, maishani mwao.

Mwanzo 2:18-23. “BWANA Mungu akasema, ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wakumfaa.’’ Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani na wanyama wote wa porini. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake akapafunika mahali pale kwa nyama. Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.’’”

Marko 10:7. “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’”

745. DUMOGAGI JUZWA.

Ulusumo lunulo, lwingine kubhanhu abho bhimogaga nzwili jabho. Inzwili ja abhanhu bhenabho, jamanaga juzwa ulubhajimoga, golecha giki bhuli ng’wene atali na bhulamu ubho gwikala ukuwelelo. Aho bhadebha chene, bhuyilombela gubhiza na mbango ja bhulamu bhuli ng’wene kugiki bhamane bhibhona na gwilomela kihamo umukikalile kabho. Hunagwene bhagayiwila giki, “dumogaji juzwa.”

 Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhalombelaga mbango ja gwikala mhola, abhanhu abho agikalaga nabho, umubhulamu bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, adebhile ugwikala bho bhutogwa na bhiye. Uweyi ali na bhidohya bho gulomba bhulamu gwingila kuli Ng’winikili bhupanga, Uwelelo, kunguno adebhile igiki imbango jigafumilaga kuli Weyi.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhanhu abho bhimogaga na gwilombela mbango ja gwikala na bhuyeji, kunguno nuweyi agabhalombelaga mbango ja gwingila kuli Mulungu abhiye, umuwikaji bhokwe.

Uweyi hangi agabhalangaga abhanhu bhakwe higulya ya gwikala na witogwi bho gwilombela mbango kugiki bhikale mhola, umubhulamu bhobho. Hunagwene agabhawilaga abhiye giki, “dumogaji juzwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutogwa bho kubhalombela mbango ja gwikala chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwendelea gutumama milimo yabho na bhuyegi, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 45:28.

Waamuzi 19:3.

2 Wakorintho 2:13.

KISWAHILI: TUNYOENI ZIKIOTA.

Methali hiyo, ilianzia kwa watu waliokuwa wakinyoana nywele zao. Nywele za watu hao, zilikuwa zikiota wanapozinyoa, kuonesha kwamba kila mmoja bado ana uhai wa kuishi hapa duniani.

Walipoelewa hivyo, walianza kuombeana baraka za kuishi maisha marefu, ili waendelee kuonana na kuongea pamoja katika maisha yao. Ndiyo maana waliambiana kwamba, ‘tunyoeni zikiota.’

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwaombea baraka za kuishi salama watu anaoishi nao, katika uhai wake. Mtu huyo, anaelewa kuishi kwa upendo na wenzake.

Yeye ana upendo wa kuwaombea wenzake baraka za kutoka kwa Mungu, kwa sababu ya uelewa wake, kwamba, Mungu ndiye mwenye baraka hizo, ili waendelee kuishi kwa amani, maishani mwao.

Mtu huyo, hufanana na watu wale waliokuwa wakinyoana na kuombeana baraka za kuishi kwa furaha, ili waendelee kuwa na amani maishani mwao, kwa sababu naye huwaombea wenzake anaoishi nao, baraka za kutoka kwa Mungu, maishani mwake.

Yeye huwafundisha pia watu wake juu ya kuwa na upendo wa kuombeana baraka za kutoka kwa mwenyezi Mungu, ili waendelee kuishi kwa amani. Ndiyo maana huwaambia wenzake kwamba, “tunyoeni zikiota.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na upendo wa kuombeana baraka za kutoka kwa Mungu, ili waweze kuendelea kuonana na kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Mwanzo 45:28. “Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.’’”

Waamuzi 19:3. “mume wake akaenda kumsihi ili arudi. Alikwenda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.”

2 Wakorintho 2:13. “bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.”

744. DUGWIBHONA ULU DUTALI DUB´INYA MATU.

Ulusumo lunulo, lwingine kubhanhu bhabhili abho bhilomelaga umulugendo lobho. Abhanhu bhenabho, bhagab’inyaga amatu gabho ulu bhalilomela, golecha bhulamu bho bhuli ng’wene ubho alinabho.

 Uumo obho agang’wila ung’wiye, “unene nashika aha najile dugwibhona hangi.” Ung’wiye agashosha, “dugwibhona ulu dutali dub’inya matu.” Ukwene huguhaya giki, bhagwibhona hangi ulu bhatali bhalimhola, kunguno abhanhu abho bhacha bhadadulile ugugab’inya amatu gabho.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile igiki ilihoyi ingelelo ya bhulamu bho bhanhu umusi, iyo igabhisanganijaga kunguno bhadaimanile, umuwikaji bhobho. Umunhu ng’wunuyo, ali na bhidohya bho gulomba bhulamu gwingila kuli Ng’winikili bhupanga, Uwelelo. Uweyi agabhalombela bhulamu na bhiye abho agikalaga nabho, kugiki bhamane bhibhona ulu bhatali bhapanga.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhilomeji abho bhali bhadebhile igiki ubhulamu bhobho bhuli na ngelelo, kunguno nuweyi agabhalombelaga bhulamu abhiye gwingila kuli Mulungu, golecha giki adaidebhile ingeleo wa bhulamu bhobho.

Uweyi hangi agabhalangaga abhanhu bhakwe ahigulya ya gwikala na widohya bho gwilombela bhulamu kugiki bhamane bhibhona ulu bhalibhanga. Hunagwene agabhawilaga abhiye giki, “dugwibhona ulu dutali dub’inya matu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na widohya bho gunsendamila Welelo, na gwilombela bhulamu bho gwingila kuli Weyi, kugiki bhadule gwendelea gwibhona na gutumama milimo yabho chiza, umubhulamu bhobho.

Mwanzo 45:28.

Waamuzi 19:3.

2 Wakorintho 2:13.

KISWAHILI: TUTAONANA TUKIWA BADO TUNACHEZESHA MASIKIO.

Methali hiyo, ilianzia kwa watu wawili waliokuwa wakiongea katika safari yao. Watu hao, walioyaona masikio yao yakicheza walipokuwa wakiongea, kuonesha uwepo wa uhai wa kila mmoja wao alio nao.

Mmoja wao alimwambia mwenzake, “mimi nimefika ninapoenda tutaonana tena.” Mwenzake alijibu, “tutaonana tukiwa bado tunachezesha masikio.” Ndiyo kusema kwamba, wataonana tena kama watakuwa hai, kwa sababu watu waliokufa hawawezi kuyachezesha masikio yao.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa kwamba, uhai wa wanadamu una mwisho hapa duniani ambao wao hawauhafamu, maishani mwao. Mtu huyo, ana unyenyekevu wa kuomba uhai kutoka kwa mwenye uhai ambaye ni Mungu. Kutokana na unyenyekevu huo, yeye huwaombea wenzake uhai ili waendelee kuonana kama bado wako hai.

Mtu huyo, hufanana na wale watu waliokuwa wakiongea katika safari yao, ambao walielewa kwamba, uhai wao una mwisho, kwa sababu naye huwaombea uhai wenzake anaoishi nao ili waendele kupata nafasi ya kuonana maishani mwao, kuonesha kwamba haufamu mwisho wa uhai wao.

Yeye huwafundisha pia watu wake juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuombeana uhai kutoka kwa mwenyezi Mungu, ili wapate nafasi ya kuonana kama bado wako hai. Ndiyo maana huwaambia wenzake kwamba, “tutaonana tukiwa bado tunachezesha masikio.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kumtegemea Mungu, na kuombeana uhai utokao kwake, ili waweze kuendelea kuonana na  kuyatekeleza vizuri majukumu yao, katika siku za uhai wao.

Mwanzo 45:28. “Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.’’”

Waamuzi 19:3. “mume wake akaenda kumsihi ili arudi. Alikwenda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha.”

2 Wakorintho 2:13. “bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.”

743. OBHUKIJAGA MULI PUNDUKILE.

Olihoyi munhu uyo oliabhuchije jiliwa ja guchala hanhu. Aliyo lulu, ijiliwa jinijo jamanaga jugeha duhu, umu lugendo lokwe. Nose uibhuja bhung’wene, “ni bhuli unigo gone guli geha chiniki?”  Munhu umo uyo alihanuma yakwe ujibhona ijiliwa ijo jidikaga umunzila, ung’wila, “obhukikaja mulipundukile.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo gudina na solobho yose yose, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’winuyo agajimijaga makanza gakwe bho nduhu solobho, ukunhu alijimala sagala ni nguzu jakwe. Uweyi agamalaga nguzu jakwe bho nduhu gupandika solobho yose yose.

Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga nimo uyo gudikilile nu munhu uyo obhukijaga jiliwa jakwe muli ginhu ilo lipundukile, kunguno nuweyi agatumamaga nimo uyo gudina solobho, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga umunhu ng’wunuyo giki, “obhukikaja mulipundukile.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gutumama milimo iyo idina solobho yose yose, kunguno munho bhagujimija makanza gabho sagala. Gashinaga lulu, igelelilwe bhaisolanye imilimo iyo idulile gubhenhela solobho ningi, hunabhayitumame lulu iyiniyo, umuwikaji bhobho.

Hagai 1:6.

Mhubiri 2:11.

Isaya 49:4.

Yeremia 12:13.

Luka 17:10.

1 Wathesalonike 3:5.

Tito 3:9.

Luka 10:38-42.

Luka 16:16-20.

KISWAHILI: UMEBEBEA KWENYE CHOMBO KILICHOTOBOKA.

Alikuwepo mtu aliyebeba chakula akikipeleka sehemu fulani. Lakini, chakula hicho kilikuwa kikizidi kupungua tu katika safari yake hiyo. Mwishowe akaanza kujiuliza mwenyewe, “kwa nini mzigo wangu unazidi kupungua?” Mtu mmoja aliyekuwepo nyuma yake akakiona chakula hicho kilichokuwa kikimwagika, akamwambia, “umebebea kwenye chombo kilichotoboka.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi isiyo na faida yoyote, katika maisha yake. Mtu huyo, hupoteza wakati wake bure, huku akizimaliza hovyo nguvu zake hizo. Yeye huzimaliza nguvu zake hizo kwa kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na bila faida yoyote.

Mtu huyo, hufananishwa na yule aliyebebea chakula chake kwenye chombo kilichotoboka, kwa sababu naye hufanya kazi isiyo na faida, katika utendaji wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umebebea kwenye chombo kilichotoboka.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kupoteza muda wao katika kufanya kazi isiyo na faida yoyote, maishani mwao. Kumbe basi, wanatakiwa kuzifanyia utafiti kazi zao, ili waweze kuzichagua na kuzitekeleza zile zinazowaletea faida katika kuziendeleza familia zao, maishani mwao.

Hagai 1:6. “Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotoboka toboka.”

Mhubiri 2:11. “Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo mikono yangu ilikuwa imefanya na yale niliyotaabika kukamilisha, kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbizaupepo, hapakuwa na faida yo yote chini ya jua.”

Isaya 49:4. “Lakini nilisema, “Nimetumika bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida. Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa BWANA, nayo ijara yangu iko kwa Mungu wangu.””

Yeremia 12:13. “Watapanda ngano lakini watavuna miiba, watajitaabisha lakini hawatafaidi cho chote Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya BWANA Mungu.’’”

Luka 17:10. “Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili, tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.”

1 Wathesalonike 3:5. “Kwa sababu hii nilipokuwa siwezi kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.”

Tito 3:9. “Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi, mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu sheria, kwa sababu haya hayana faida tena ni ubatili.”

Luka 10:38-42. “Ikawa Yesu na wanafunzi Wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake. Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Maria, ambaye yeye aliketi chini miguuni mwa Yesu akisikiliza yale aliyokuwa akisema. Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Yesu na kumwuliza, “Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.” Lakini Bwana akamjibu, “Martha,Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.””

Luka 16:16-20. ‘‘Torati na manabii vilitumiwa mpaka kuja kwa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni rahisi zaidi mbingu na nchi kupita kuliko hata herufi moja kuondoka katika Sheria. “Mtu ye yote ampaye mkewe talaka na kumwoa mwanamke mwingine azini, naye mwanaume amwoaye mwanamke aliyetalikiwa azini.  ‘‘Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa, kila siku. Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima.”

742. UGUB´INAGA WISAGILILE ULU UKABHONILE UDUKALEKA.

Ulusumo lunulo, lulolile nguno ya ng’wa munhu uyo agub’inaga mbina. Inguno yakwe yiniyo igang’winhaga wisagizu bho gujipandika ijo ajihayile jinijo umubhutumami bhokwe.

Olihoyi munhu uyo ob’inaga mbina kunguno ya kuchola nyiye bhitole. Umunhu ng’wunuyo, agikomeja noyi ub’ina mbina yiniyo, mpaga nose umpandika ung’wiye bhitola, naoya lulu ugub’ina. Hungwene abhanhu bhang’wilaga giki, “ugub’inaga wisagilile ulu ukabhonile udukaleka.”

Ulusumo lununo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe na wisagizu bhutale bho gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agikomeja noyi uguitumama imilimo yakwe na bho bhukamu bhutale, kunguno amanile igiki agupandika ijo alijichola.

Uweyi agabhalanjaga na bhanhu bhakwe inzila ja gwikomeja uguitumama imilimo yabho na wisagizu bho gupandika matwajo mingi. Kunzila yiniyo, agapandika amatwajo mingi noyi, umuwikaji bhokwe, ayo gagenhagwa na uwisagizu bhokwe bhunubho, ubho bhugang’winaga nguzu ja gwikomeja kutumama milimo yakwe mpaka ojipandika ijo alijichola.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mini ombina uyo ob’inaga na wisagizu bhutale bho gupandika ng’wiye ogwitola nang’hwe mpaka nose umpandika, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe na wisagizu bhutale mpaka opandika matwajo mingi umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki,  “ugub’inaga wisagilile ulu ukabhonile udukaleka.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo yabho na wisagizu bho gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhobho, kugiki bhadule guitumama imilimo yabho na bhukamu bhutale mpaka bhapandika matwajo gagujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 13:45-46.

Mathayo 10:10.

Mithali 6:23.

1 Wakorintho 9:23-27.

1 Yohana 3:2-3.

Luka 18:28-29.

Sala ya gwisagila

Mathayo 19:27-29.

UNACHEZA KWA MATUMAINI KAMA UMEKAONA HUTAKAACHA.

Methali hiyo, huangalia lengo la mtu anayecheza ngoma. Lengo hilo, humpatia matumaini ya kukipata kile anachokitaka, katika utendaji wake wa kazi. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alikuwa anacheza ngoma kwa lengo la kumpata mwenzake wa kuoana naye.

Mtu huyo, alijibidisha kucheza ngoma hiyo, mpaka mwishowe akafanikiwa kumpata mwenzi huyo wa maisha, wakaoana, ndipo alipoacha kucheza ngoma hizo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “unacheza kwa matumaini kama umekaona hutakaacha.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake kwa matumaini makubwa ya kupata mafanikio mengi, katika utendaji wake. Mtu huyo, hujibidisha kuzitelekeza vizuri kazi zake hizo, na kwa bidii kubwa kwa sababu anayo matumaini makubwa ya kufanikiwa.

Yeye huwafundisha pia wenzake njia za kujibidisha katika utekelezaji wa majukumu yao, wakiwa na matumaini ya kufanikiwa zaidi. Kupitia njia hizo, yeye pia hupata mafanikio mengi katika maisha yake, yatokanayo na kuwa na matumaini makubwa ambayo humpatia nguvu za kuyatekeleza vizuri majukumu yakwe.

Mtu huyo, hufanana na mcheza ngoma aliyekuwa aliyecheza huku akiwa na matumaini makubwa ya kumpata mwenzi wake wa maisha mpaka akampata, kwa sababu naye huyatekeleza majukumu yake kwa matumaini makubwa ya kufanikiwa kuyafikia malengo yake, maishani mwake. Ndiyo maana watu, humwambia kwamba, “unacheza kwa matumaini kama umekaona hutakaacha.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao wakiwa na matumaini makubwa ya kufanikiwa katika utendaji wao, ili waweze kuongeza bidii ya kuwapatia mafanikio ya kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 13:45-46. ‘‘Tena, Ufalme wa Mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi. Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

Mathayo 10:10. “Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtenda kazi anastahili posho yake.”

Mithali 6:23. “Kwa maana maagizo haya ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,”

1 Wakorintho 9:23-27. “Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake. Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo. Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele. Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa, la, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha ili nikishawahubiria wengine, mimi nisiwe mtu wa kukataliwa.”

1 Yohana 3:2-3. “Wapenzi, sasa tu watoto wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba, Yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya katika Yeye hujitakasa, kama vile Yeye alivyo mtakatifu.”

Luka 18:28-29. “Ndipo Petro akasema, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” Yesu akajibu, “Amin nawaambia, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu”

Sala ya matumaini

Mathayo 19:27-29. “Ndipo Petro akamjibu, ‘‘Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata, tutapata nini basi?’’ Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia , wakati wa kufanywa upya vitu vyote, wakati mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake cha utukufu cha enzi, ninyi mliomfuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. Kila mmoja aliyeacha nyumba au ndugu zake wa kiume au wa kike au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili Yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo na ataurithi uzima wa milele.”