1164. UDIZIGUSHA NA NGUKU UGUBUKULA MBELELE.

Inguku ili shinu nhenaguji gete ukubhalimi iyo igajaga kumigunda yabho yagajilya ijiliwa jabho. Inguku yiniyo idulile gugamala amandege ga nimi uyo agigusha nayo bho nduhu ugukalana ijinagugulinda ungunda gokwe.

Olihoyi nimi uyo agigusha ni nguku bho guleka ugugulinda chiza ungunda gokwe uyo gali go mandege mpaga jugalya pye amandege gakwe genayo usagijiwa mbelele duhu. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “udizigusha na nguku ugubukula mbelele.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajilekanijaga sagala ijiliwa jakwe mpaga jaliwa na majilili, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adajilanhanaga chiza ijiliwa jakwe ulu japya umumigunda yakwe kunguno ya bhulekenija bhokwe bhunubho. Uweyi agasangaga jamalagwa guliwa na majilili ijiliwa jakwe jiniko haho jitali mungunda kunguno ya bhujidadilila bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agaleka ugugalanhana chiza amandege gakwe mpaga gumalwa guliwa na nguku haho gatali mumo ngunda, kunguno nuweyi agajilekanijaga mpaka jamalwa guliwa na majilili ijiliwa jakwe, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “udizigusha na nguku ugubukula mbelele.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na bhulalanhanu bho gujilanhana chiza ijiliwa jabho, kugiki bhadule kupandika jiliwa gubhambilija ujilisha chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

1Petro 5:8-9.

2 Thimotheo 4:7.

KISWAHILI: USICHEZE NA NYANI UTAVUNA MABUA.

Nyani ni mnyama mharibifu kabisa kwa wakulima ambaye huenda kula mahindi kwenye mashamba yao. Nyani huyo aweza kuyamaliza kuyala mahindi ya mkulima yule ambaye hucheza naye kwa kutokuyalinda vizuri mashamba yake hayo.

Alikuwepo mkulima yule ambaye alicheza na nyani kwa kuacha kulilinda vizuri shamba lake la mahindi mpaka nyani hao wakayala mahindi yake yote akabakishiwa mabua tu. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “usicheze na nyani utavuna mabua.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatelekeza mashamba yake ya chakula mpaka yakafikia hatua ya kuliwa na wanyama waharibifu, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hayalindi vizuri mashamba yake ya chakula yanapokamaa kwa sababu ya kutokuyajali kwake. Yeye hukuta wanyama hao wameyala mazao yake yote yangali bado shambani kwa sababu ya kutokuyalinda vizuri hivyo mazao yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule ambaye hakuyalinda vizuri mahindi yake mpaka yakaliwe na nyani yangali bado shambani, kwa sababu naye huyatelekeza mazao yake mpaka yanaisha yote kwa kuliwa na wanyama waharibifu. Ndiyo maana watu humuambia kwamba “usicheze na nyani utavuna mabua.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ujanja wa kuyalinda vizuri mazao yao ya chakula, ili waweze kuvuna mazao ya kutosha kuwasaidia katika kuzilisha vizuri familia zao, maishani mwao.

1Petro 5:8-9.

2 Thimotheo 4:7.

ENGLISH: DO NOT PLAY WITH MONKEYS; YOU WILL REAP STALKS.

Monkeys are very destructive animals to farmers because they go to eat maizes in their fields. The monkey can end up eating the maizes of the farmer who plays with him by not protecting his fields properly.

There was a farmer who played with monkeys by not protecting his field of maizes properly until the monkeys ate all the maizes and he was left with only stalks. That is why people told him that, “do not play with monkeys; you will reap stalks.”

This proverb is compared to the person who neglects his food fields until they reach the stage of being eaten by pests, in his life. Such person does not protect his food fields well when they mature because of his carelessness. He finds that pests and other destructive animals have eaten all his crops while they are still in the field because of not protecting them properly, in his life.

Such person is similar to the one who did not protect his maizes properly until they were eaten by monkeys while they were still in the field, because he also neglects his crops until they are all eaten by pests. That is why people tell him that “do not play with monkeys; you will reap stalks.”

This proverb teaches people to be smart enough to protect their food crops, so that they can harvest enough crops to help them in feeding their family members well, in their lives.

1 Peter 5:8-9.

2 Timothy 4:7.

long-tailed-macaque-4501435__480

2 comments

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.