1163. MUMO JIGANONELA MUNHU JIGALEKAGWA.

Aho kale olihoyi munhu uyo olimuchalo jilebhe ijo jali jawiza noyi. Umunhu ng’wunuyo oliomanila noyi umuchalo jinijo kunguno ya wiza bhojo.

Aliyo lulu ligashiga likanza wigung’wa sata aha kaya yakwe yiniyo mpaga usamamila muchalo jingi na gwinga umuchalo jinijo kunguno yiniyo. Uweyi agajileka ichalo jinijo na wiza bhojo. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agayomba giki, “mumo jiganonela munhu jigalekagwa.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalyaga jiliwa chiza bho nduhu ugubhimbelwa umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agalyaga ijiliwa bho gwilingila chiza numo agigutililaga duhu na goya ugulya, mumo jiganolela ijiliwa jinijo, kunguno adatogilwe ugulya mpaga ubhimbelwa. Uweyi agikalaga na majiliwa mingi aha kaya yakwe kunguno ya gujitumamila na witegeleja ijiliwa ijo agajipandikaga jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ulimuchalo jawiza usamila muchalo jingi, ujileka na wiza bhojo ichalo jinijo, kunguno nuweyi agalyaga jiliwa jinonu ulu wiguta duhu ojileka na bhunonu bhojo ijiliwa jinijo. Hunagwene agayombaga giki, “mumo jiganonela munhu jigalekagwa.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gujitumila ijikolo jabho bho witegeleja bhutale kugiki jidule gubhambilija chiza, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mwanzo 19:23-26.

Mathayo 2:13.

KISWAHILI: HATA KIKOLEE UTAMU WA CHUMVI HUACHWA.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyeishi kwenye kijiji fulani ambacho kilikuwa kizuri sana. Mtu huyo alizoea sana kuishi kwenye kijiji hicho kwa sababu ya uzuri wa makazi hayo.

Lakini basi ulifika wakati ambapo alianza kuugua magonjwa mbalimbali kwenye familia yake mpaga akahamia kwenye kijiji kingine, akakiacha kijiji hicho pamoja na uzuri wake huo. Ndiyo maana yeye alisema kwamba, “hata kikolee utamu wa chumvi huachwa.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hula chakula kwa kiasi bila kubimbiwa katika maisha yake. Mtu huyo, hula chakula kwa umakini mzuri wa kutosheka tu na kuacha kula hata kama chakula hicho kitakuwa kitamu namna gani, kwa sababu hapendi kula mpaga kuvimbiwa. Yeye huwa na chakula kingi sana kwenye familia yake hiyo kwa sababu ya kuvitumia kwa umakini vyakula anavyovipata, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeishi kwenye kijiji kizuri, akahamia kwenye kijiji kingine, akakiacha hicho na uzuri wake, kwa sababu naye hula chakula kizuri na kukiacha na uzuri wake kila anapotosheka kula. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “hata kikolee utamu wa chumvi huachwa.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuvitumia vitu vyao kwa umakini mkubwa ili viweze kuwasaidia vizuri, maishani mwao.

Mwanzo 19:23-26.

Mathayo 2:13.

child-3893216__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.