1155. KALAGU – KIZE. NTOLWA ALILAB’AGILA MUNGUNDA – LIZETI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola lizeti. Ilizeti yiniyo, lilinti ilo ulu giki lyuhola ligafunyaga wilab’u b’ulab’agizu guti ntolwa uyo alifumanija kunguno nang’hwe agazwalaga jizwalo jilab’agizu chiza. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ntolwa alilab’agila mungunda –  lizeti.”

Ikalagu yiniyo, igalenganiyagwa kuli ntolwa uyo agayilelaga chiza ikaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agatumamaga milimo yakwe chiza na gubhalanga bhanhu bhakwe nzila ja gwika chiza na bhanhu kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho. Uweyi abhalumanyaga chiza abhanhu abho bhidumaga bho guhoya nabho chiza kunguno ya nhungwa jakwe ijawiza jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga ni lizeti iyo igalab’agilaga mungunda, kunguno nuweyi alina nhungwa niza ijo jigang’wambilijaga ugubhalela chiza abhanhu bhakwe, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ntolwa alilab’agila mungunda –  lizeti.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhitoji higulya ya gubhiza na nhungwa ja gubhalela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwikala chiza, umu kaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Wimbo ulio bora 3:11.

Wimbo ulio bora 4:1.

Wimbo ulio bora 5:1’

Isaya 61:10-11.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI –  TEGA.

BIBI HARUSI ANAMEREMETA SHAMBANI – ALIZETI.

Chanzo cha kitendawili hicho kinaangalia alizeti. Alizeti hiyo, ni mti ule ambao ukichanua hutoa maua ya kumeremereta kama bibi harusi anayeolewa kwa sababu naye huvaa mavazi ya kumetameta vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, “bibi harusi anameremeta shambani – alizeti.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa bibi harusi yule ambaye huilea vizuri familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake vizuri na kuwafundisha watu wake njia za kuishi vizuri na watu, kwa sababu ya uaminifu wake huo. Yeye huwapatanisha watu waliokosana kwa kuongea nao vizuri, kwa sababu ya tabia hiyo njema aliyo nayo, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na ile alizeti iliyokuwa ikimeremeta shambani, kwa sababu naye ana tabia njema ambayo humsaidia katika kuwalea vizuri watu wake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “bibi harusi anameremeta shambani – alizeti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuwalea vizuri watu wao, ili waweze kuishi vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Wimbo ulio bora 3:11.

Wimbo ulio bora 4:1.

Wimbo ulio bora 5:1’

Isaya 61:10-11.

sunflower-1627179__480

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.