959. KALAGU – KIZE. ULU NUGUDIMA NADUGULEKELA – WILEMBO.

Ikalagu yiniyo, ihoyelile linti ilo ligitanagwa, Wilembo. Ilinti linilo, ligafunyaga mingi ayo gikolile na mabhele ulu uligoma. Aminzi genayo, ulu ugabhambila nulu jinhu judamila chiza guti jadimilagwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ulu nugudima nadugulekela – wilembo.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayidimilaga imihayo iyanhana bho nduhu ugutinginyiwa na oseose, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agilangaga mihayo ya gung’winha kajile kawiza, na guyidimila chiza, kunguno ahayile ayibheje chiza ikaya yakwe. Uweyi, agapandikaga matwazo mingi umumilimo yakwe, kunguno ya kujidimila chiza inhungwa ija wiza jinijo, umuwikaji bhobho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu wilembo ubho bhugadimilaga aha ginhu, kunguno nuweyi agajidimilaga inhungwa ija wiza bho nduhu ugutinginyiwa na oseose, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “ulu nugudima nadugulekela – wilembo.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwilanga nhungwa ja wiza na kujimila chiza, umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Ufunuo 2:10.

Yohana 6:67-68.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

NIKIKUKAMATA SIKUACHII – URIMBO.

Kitendawili hicho, huongelea juu ya mti uitwao Urimbo. Mti huo, ukigongwa hutoa maji kama yanayofanana maziwa, ambayo hutumika katika kuzibia vitu kwa sababu ya kushika vizuri pale yanapowekwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “nikikukamata sikuachii – Urimbo.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujifunza tabia njema na kushikilia vizuri bila kutikiswa, katika maisha yake. Mtu huyo, hujifunza maneno yenye maadili mema na kuyaishi vizuri, kwa sababu anataka kuilea vizuri familia yake. Yeye hufanikiwa katika kuiletea maendeleo mengi familia yake, kwa sababu ya kuyaishi vizuri maadili hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule urimbo unaoshika vitu bila kuachia, kwa sababu naye huyashikilia vizuri maadili mema bila kuyaachia, katika maisha yake. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “nikikukamata sikuachii – Urimbo.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujifunza maadili mema na kuyaishi katika utekelezaji wa kazi zao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Ufunuo 2:10.

Yohana 6:67-68.

 

children-12

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.