834. UJIDUBHUMBA NGUMI KIHAMO NIWE.

Ulusumo lunulo, lulemejije bhubhumbi bho ngumi kihamo niwe. Ubhubhumbi bho ngumi bhunubho, bhuli bho gudimilila liwe na guhadikija kulikumbanija bho nkono gumo uyo gugasadyaga, kunguno ya bhudamu bho liwe linilo.

Kuyiniyo lulu, unkono gunuyo gugadumaga uponya ingumi yiniyo, kunguno ya guminyiwa ni liwe linilo na gugwinha nimo goguliluta iliwe linilo. Ung’winikili nkono gunuyo, agahuganyiwaga ni milimo iyo ilibhili yiniyo, gwandija ugoguponya iliwe nu goguponya ingumi yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ujidubhumba ngumi kihamo niwe.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agadimaga milimo ibhili iyo idikolile ku likanza limo, iyo agayihadikijaga ikole bho nguzu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agasanjasanjaga mihayo ibhili iyo idikolile bho guyihadikija ikole, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga ugupandika amatwajo amingi, kunguno  ya gutumama milimo ibhili iyo idajilanijije, ku likanza limo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ubhumbaga ngumi kihamo niwe, kunguno nuweyi agadimaga milimo, nulu mihayo ibhili iyo idikolile ku likanza limo, iyo agayihadikijaga ikole bho nguzu, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ujidubhumba ngumi kihamo niwe.”

Ulusumo lunulo, lolemeja bhanhu higulya ya kutumama milimo ibhili iyo idikole kuli kanza limo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhobho.

Mathayo 6:24.

Luka 16:13.

KISWAHILI: USIFUMBATE NGUMI PAMOJA NA JIWE.

Methali hiyo, hukataza ufumbataji wa ngumi pamoja na jiwe. Ufumbataji huo wa ngumi, ni wa kushikilia jiwe na kulazimisha kulikumbatia kwa mkono mmoja, ambao huuma kwa sababu ya ugumu wa hilo jiwe.

Kwa hiyo basi, mkono huo hushindwa kutupa ngumi hiyo, kwa sababu ya kuumizwa na jiwe hilo, na hushindwa kufanya kazi ya kulitupa jiwe hilo. Mwenye mkono huo, huchanganywa na kazi hizo mbili ambazo ni kutupa ngumi na kutupa jiwe kwa wakati mmoja. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “usifumbate ngumi pamoja na jiwe.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hushiga kazi mbili zisizofanana kwa wakati mmoja, ambazo huzilazimisha zifanane kwa nguvu, katika maisha yake. Mtu huyo, huchanganya maneno mawili ambayo hayafanani kwa kuyalazimisha yafanane, katika maisha yake. Yeye hushindwa kupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukumu yake, kwa sababu ya kushika mambo mawili yasiyofanana kwa wakati mmoja, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyefumbata ngumi pamoja na jiwe kwa wakati mmoja, kwa sababu naye hushika kazi mbili zisizofanana kwa wakati mmoja, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “usifumbate ngumi pamoja na jiwe.”

Methali hiyo, hukataza watu juu ya kushika mambo mawili yasiyofanana kwa wakati mmoja, katika maisha yao, ili waweze kupata maendelea mengi, katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mathayo 6:24.

fist-

boxer-

stone-age-

ENGLISH: DO NOT MAKE A FIST TOGETHER WHEN YOU HAVE A STONE IN YOUR PALM.

This proverb forbids clenching a fist with a stone in it. Otherwise the grip of the fist will have to hold the stone by force which hurts the fingers of the one who does so, because of the hardness of the stone.

Therefore, the hand fails to throw the fist, because it is hurt by the stone, and it fails to work to throw the stone. Such hand is caught between by the two tasks of throwing a fist and a stone at the same time. That is why people say, “do not make a fist together when you have  a  stone in  your  palm.”

This proverb is likened to a man who pursues two different tasks at the same time, forcing them to be very similar in life. Such person mixes two works that are not the same by forcing them to be the same in his life. He fails to achieve much success in carrying out his daily responsibilities, because of holding on two different things at the same time in life.

This man is like the one who holds his fist with a stone at the same time, because he also performs two different tasks at the same time in his life. That is why people tell him that, “do not make a fist together when you have a  stone in  your  palm.”

This proverb forbids people from holding on two different things at the same time in their lives, so that they can make more progress in fulfilling their daily duties.

Matthew 6:24.

         

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.