833. KANUNGU KA MINZI KAGAJAGA UKO KAFUMILE.

Oliyohi munhu uyo oliadafunyaga ijikolo jakwe ukubhiye. Umunhu ng’wunuyo, wiganikaga giki adalapandika makoye, umukikalile kakwe. Lushigu lumo, agagayiwa minzi aha kaya yakwe, ugalomba ha bhazenganwa bhakwe aliyomba, “nigunanagi minzi nagayiyagwa gete agagung’wa.”

Abhazenganwa bhakwe bhagashosha, “dudugwinha aminzi ayise kunguno ubhebhe udabhinhaga abhiyo abho bhali na makoye.” Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “kanungu ka minzi kagajaga uko kafumile.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adabhambilijaga abhiye abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agalemaga ugwikala kihamo nabhiye, kunguno ya wiming’holo bhokwe. Uweyi agalemaga ugubhambilija abhanhu abho bhagajaga gujunomba bhugunanwa bhokwe ubho bhudulile kubhingija amakoye gabho genayo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo olemaga ugufunya ijikolo jakwe kubhiye abho bhanombaga, kunguno nuweyi adabhambilijaga abhiye abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Uweyi agagayiyagwa umunhu uo gung’wambilija ulu opandikaga makoye, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “kanungu ka minzi kagajaga uko kafumile.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizang’holo bho gubhambilija abhichabho abho bhagapandikaga mayange, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 2:44-45.

KISWAHILI: CHUNGU CHA MAJI HUENDA KINAKOTOKA.

Alikuwepo mtu mmoja ambaye alikuwa hatowi vitu alivyo navyo kwa wenzake. Mtu huyo, alifikiri kwamba hatapata matatizo, katika maisha yake. Siku moja, aliishiwa maji kwenye familia yake, akaenda kuomba kwa majirani zake akisema, “nisaidieni maji ya kunywa nimeishiwa kabisa.”

Majirani zake walijibu, “hatukupi maji sisi kwa sababu wewe huwa huwapi wenzako waliokumbwa na matatizo.” Ndiyo maana watu husema kwamba, “chungu cha maji huenda kinakotoka.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa hawasaidii wenzake waliokumbwa na matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hukataa kuishi pamoja na wenzake kwa sababu ya uchoyo wake huo. Yeye hukataa hata kuwasikiliza wale wanaomuomba msaada wake uwezao kuwaondolea matatizo yao.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekataa kutoa vitu vyake kwa wenzake wanaomuomba, kwa sababu naye huwa hawasaidii wenzake walioko kwenye matatizo. Yeye hukosa watu wa kumsaidia anapopata matatizo, maishani mwake.Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “chungu cha maji huenda kinakotoka.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwasaidia wenzao waliokumbwa na matatizo, katika maisha yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Matendo ya mitume 2:44-45.

pot water

pot water1

 ENGLISH: THE WATER POT GOES WHERE IT CAME FROM.

There was one man who was not giving things which he had to his fellows. He thought that he would never get problems in his life. One day, he ran out of water in his family, and went to ask for help from his neighbors saying, “Help me get a drink of water. I am completely exhausted.”

His neighbors replied, “We do not give you water because you do not give it to your colleagues who are in trouble.” That is why people say, “the water pot goes where it came from.”

This proverb is likened to a man who does not help his troubled colleagues in his life. He refuses to live with others because of his greed. He even refuses to listen to those who call on him for help with their problems.

This person is like the one who refused to give his things to his fellow beggars, because he also does not help his colleagues who are in trouble. He misses people who can help him when he has problems in his life. That is why people tell him, “the water pot goes where it came from..”

This proverb instills in people an idea on how to be generous in helping others who are sufferings in their lives, so that they can develop well their family members in their societies.

Acts 2: 44-45.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.