830. MALIKO MINGI GAGUBEHELA ILO LYITA NG’OMBE YASINZWA LILIMO.

Iliko jili ginhu ijo jigikalaga na moto uyo gudulile gutumamila milimo mingi. Giko lulu na bhanhu abho bhagabehega shigala bhagapembaga moto gogubehela, uyo gudulile nulu guzugila nyama ya ng’ombe iyo yasinzagwa.

Aliyo lulu, ulu galihoyi maliko mingi agabhabehi bha shigala bhenabho, ligubhejiwa na gutumilwa liko limo duhu uguyizugila inyama yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “maliko mingi gagubehela ilo nyita ng’ombe yasinzwa lilimo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agihayaga giki uweyi aliyo osolobho kukila abhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumama milimo yakwe bho gwigimba kugiki abhanhu abho bhalimona bhankumilije, kunguno adaibhonaga isolobho ya bhiye umu bhutumami bho milimo yiniyo. Uweyi adabhalekelaga abhiye imilimo yakwe, kunguyo ya gubhadahaya aliyo nabho bhagatumama chiza guti nuweyi.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na maliko agagubehela shigara, aliyo ilo ligatumilwa uzugila inyama lilimo duhu, kunguno nuweyi agiiganikaga giki alio solobho gulebha abhiye, aliyo bhadikilile umubhutumami bhobho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “maliko mingi gagubehela ilo nyita ng’ombe yasinzwa lilimo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja gwibhona giki bhali bha solobho kukila abhichabho, kugiki bhadule gwiyambilija kihamo ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Warumi 12:4.

1Wakorintho 12:3-6.

KISWAHILI: MAJIKO MENGI NI YA KUVUTIA SIGARA LAKINI LILILOFANYA NG’OMBE ACHINJWE NI MOJA TU.

Jiko ni chombo kile ambacho huwa na moto unaoweza kufanyia kazi mbalimbali. Hivyo basi, wavuta sigara huweza kuutumia moto huo ambao huwa wanauwasha kwa lengo la kuvutia sigara. Moto huo pia unaweza kutumika kwa kupikia au kuchomea nyama ya ng’ombe aliyechingwa.

Lakini yakiwepo majiko mengi ya wavutia sigara, jiko litakalotumika kuipikia nyama hiyo ni lile litakalo washwa kwa ajili ya ng’ombe huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “majiko mengi ni ya kuvutia sigara lakini lilifanya ng’ombe achinjwe ni moja tu.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujidai kuwa wa maana kuliko wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huyatekeleza majukumu yake kwa kujigamba ili watu wanaomuona wamsifie, kwa sababu ya kujifikiria kwake kuwa ni wa maana kuliko wenzake anaoishi nao, katika utekelezaji wa majukumu hayo. Yeye huwa hawaamini wenzake kiasi cha kutosha kuwaachia kazi zake, kwa sababu ya tabia yake ya kuwadharau wenzake hao, wakati wanao uwezo wa kufanya kazi kama yeye.

Mtu huo hufanana na majiko ya kuvutia sigara, kwa sababu naye hujifikiria kuwa ni wa maana zaidi kuliko wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “majiko mengi ni ya kuvutia sigara, lakini lilifanya ng’ombe achinjwe ni moja tu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia za kujifikiria kuwa wao ni wa maana zaidi kuliko wenzao, katika maisha yao, ili waweze kuwa na ushirikiano wa kuyatekeleza vizuri majukumu yao, kwa ajili ya kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Warumi 12:4.

1Wakorintho 12:3-6.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.