829. NG’WIKAJI ATINA NGOFYOLO.

Akahayile kenako, kalolile wikaji bho ng’wana munhu uyo wikalaga ha kaya ya ng’wa munhu nhebhe. Umunhu ng’wunuyo otumamaga milimo ya ha kaya yiniyo bho gulipwa gitumo bhiyiigwila. Uweyi olipagwa hela ngehu duhu, kunguno olilaga hayo ijiliwa bhuli lushigu.

Kuyinyo lulu, ung’wikaji ng’wunuyo, oli adikalaga na hela ningi umukikalile kakwe, kunguno ihela ijingi ojililaga hayo ulu otengelwa ijiliwa. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ng’wikaji atina ngofyolo.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo gudadulile ugung’wambilija ahashigu ijahabhutongi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga nimo uyo gugang’wenhelaga hela ngehu duhu ijo agajigulilaga jiliwa ja gulya lushigu lumo duhu jashila. Uweyi agagayiyagwa ihela ja gung’wambilija ulu opandikaga makoye guti ga bhusatu, aha kayaya yakwe, kunguno ya gwisanga ojimala pye ihela jakwe bho gujigulila jiliwa, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mwikaji uyo opandikaga hela ngehu, kunguno nu weyi agapandika hela ngehu ijo agajigulilaga jiliwa, mpaka wisanya adina hela, ija gung’wimbilija umu makoye. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ng’wikaji atina ngofyolo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kutumama milimo yabho bho gujilang’hana chiza ihela jabho, kugiki bhadule kubhiza na hela ja gubhambilija umu makoye gabho.

Tito 3:3.

2Petro 2:19.

KISWAHILI: MKAAJI HANA KIPATO.

Msemo huo, huangalia ukaaji wa mtu aliyeishi katika familia ya mtu fulani. Mtu huyo, aliishi kwa kufanya kibarua kwenye familia hiyo ambayo ilimlipa kwa kadiri ya makubariano yao. Yeye alilipwa pesa kidogo tu kwa sababu ya pesa nyingi kukatwa kwa ajili ya chakula alichokula hapo kila siku.

Kwa hiyo basi, hali hiyo ilipelekea kwa yeye kuwa na pesa kidogo katika maisha yake, kwa sababu ya hela yake yingine kukatwa na familia hiyo kwa ajili ya kulipia chakula alichopewa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mkaaji hana kipato.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi isiyoweza kumsaidia katika siku za mbeleni, maishani mwake. Mtu huyo, huwa anafanya kazi ambayo humwingizia hela kidogo tu ambayo huimalizia kwenye mahitaji ya kununulia chakula cha siku moja. Yeye hukosa pesa za kuweza kumsaidia anapokumbwa na matatizo mbalimbali yakiwemo yale ya kuumwa, kwenye familia yake, kwa sababu ya kujikuta amezimalizia pesa zake zote kwenye mahitaji ya kununulia chakula, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mkaaji aliyekuwa akipata pesa kidogo alizozimalizia kwenye chakula, kwa sababu naye huzimalizia pesa zake kwa kununulia chakula, mpaka anafikia hatua ya kuishi bila pesa. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mkaaji hana kipato.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuyatekeleza majukumu yao, kwa kuzitunza vizuri pesa zao, ili waweze kuwa na ziada ya kuwatatulia matatizo yatakayokumba, maishani mwao.

Tito 3:3.

2Petro 2:19.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.