825. GUPILA GO NG’HABHI GUGAFUMILAGA NG’WA NTEMI.

Ulusumo lunulo, lulolile munhu ung’habhi uyo agapijiwa na Ntemi. Unhabhi ng’wunyo, agibhonelwa na nsabhi umo bho gutajiwa ilale lwakwe. Ijinaguchola wambilijiwa, agahoya na bhazenganwa bhakwe abho bhagang’wila, “jaga ng’wa Ntemi ugang’wila agwambilijie ugulipandike ililale lyako.” Ung’habhi agashosha, “nahene nandye lugendo lo guja kwigulu.”

Unhabhi ng’wunuyo agaja uganomela Untemi umo otagijiwa ililale lwake linilo nu nsabhi ng’wunuyo. Aho wiga chena Untemi, agang’witana unsabhi ung’wila alishoshe kuli ng’winikili ililale linilo, mpaga ulishosha ng’hana. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “gupila go ng’habhi gugafumilaga ng’wa Ntemi.”

Ulusumo lunulo, lugalenagnijiyagwa kuli munhu uyo agibhonelagwa obhuchola ubhung’hana bhokwe, mpaga obhupandika, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adagwaga ng’holo ulu wibhonelaga kunguno agahoyaga na bhanhu bhingi abho bhagantongelaga inzila ja gubhupandikila ubhung’hana. Uweyi agadulaga uguyipandika ing’hana yakwe, kunguno ya bhudiliji bho bhushauri ubho aging’hagwa nabhiye, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nhabhi uyo agaichola ing’hana mpaga ulipandika ililale lyakwe, kunguno nuweyi agaicholaga inhana yiniyo, ulu wibhonelaga mpaga oyipandika, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “gupila go ng’habhi gugafumilaga ng’wa Ntemi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija guichola ing’hana bho gubhudilila chiza ubhushauri, ulu bhibhonelagwa mpaga bhayipandika inhana yiniyo, kugiki bhadule gujilanghana chiza isabho jabho, umuwikaji bhobho.

Luka 18:1-8.

KISWAHILI: KUPONA KWA MASKINI HUTOKA KWA MTEMI.

Methali hiyo, huangalia mtu maskini aliyesaidiwa na Mtemi. Maskini huyo, alionewa na tajiri mmoja kwa kunyang’anywa shamba lake. Yeye alitafuta ushauri kwa kuongea na majirani zake ambao walimwambia, “nenda kwa Mtemi ukamwambie akusaidia kulipata shamba lako.” Yule maskini alijibu, “sawa naanza safari ya kwenda ikulu.”

Maskini huyo, alifika kwa Mtemi na kumueleza namna alivyonyang’anywa shamba lake na yule tajiri. Mtemi aliposikia hivyo, alimwita yule tajiri na kumwamuru alimrudishie mali hiyo mwenye shamba lake, mpaka akalirudisha kweli. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kupona kwa maskini hutoka kwa Mtemi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hudhurumiwa na kuitafuta haki yake mpaka anaipata, katika maisha yake. Mtu huyo, hakati tamaa ya kuitafuta haki yake anapoonewa, kwa sababu ya bidii yake ya kuomba ushauri kutoka kwa wale wanaoweza kumpatia njia za kuipata haki hiyo. Yeye hufanikiwa kuipata mali yake iliyonyang’anywa kwa sababu ya kuufanyia kazi ushauri anaopewa na wenzake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule maskini aliyeitafuta haki ya kurudishwa shamba lake mpaka akalipata, kwa sababu naye huitafuta haki yake mpaka anaipata, anapoonewa, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “kupona kwa maskini hutoka kwa Mtemi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kuzitafuta haki zao na kuzitunza kwa kuufuata ushauri uwezao kuwapatia haki hizo, ili waweze kuzilinda vizuri mali zao, maishani mwao.

Luka 18:1-8.

ENGLISH: THE HEALING OF THE POOR COMES FROM THE KING.

This proverb looks at the poor man who was helped by the Chief in getting back his land. The poor man was oppressed by a rich man who had his land confiscated. He sought advice by talking to his neighbors who told him, “Go to the Chief and tell him to help you find your farm.” The poor man replied, “Well I am starting the journey to the palace.”

The poor man went to the chief and told him how he had been robbed of his land by the rich man. Upon hearing this, the chief summoned the rich man and ordered him to return the property to his owner. The rich man returned it to the poor man. That is why people say that “the healing of the poor comes from the King.”

This proverb is likened to a man who is wronged and seeks his own righteousness until he finds it, in his life. He seeks justice when he is oppressed, because of his diligence in seeking advice from those who can give him the means to obtain it. He manages to recover his confiscated property by applying the advice given by his colleagues throughout his life.

This man is like the poor man who sought his right enough to get his land back, because he also seeks his right until he finds it, when he is oppressed in life. That is why he tells the people that “the healing of the poor comes from King.”

This proverb teaches people on how to be diligent in seeking their rights and taking care of them by following the advice which will enable them to get their rights, so that they can better protect their properties in their families.

Luke 18: 1-8.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.