805. KANIGO KA NG’HABHI KAGANGOYA NSABHI.

Bhalihoyi bhanhu bhabhili abho bhikalaga muchalo jilebhe, uungi ilinsabhi, alu ungi alinhabhi. Unhabhi olina kanigo ako akagatuula hasi. Unsabhi akagadalahija akanigo kenako, aliyomga, “kihendyage akanigo kako nabhite.”

Unhabi agashosha, “kabhuchage duhu ukatuule lwande.” Unsabhi ng’wunyuyo, agagema ugukabhucha akanigo kenako ukaduma nulu kugasegeja. Uweyi agacha soni noyi aho oguduma ugugubhucha unigo gunuyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “kanigo ka ng’habhi kagangoya nsabhi.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agipondaga soni bho guyidahahija imilimo ya bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adaidebhile isolobho ya milimo ya bhiye yiniyo, kunguno ya libhengwe lwakwe linilo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agipondaga soni weyi ng’winikili kunguno ya guyidalaha imilimo ya bhiye bhenabho, aliyo adabhudebhile ubhudamu bhoyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsabhi uyo agaguduma ugugubhucha unigo go nhabhi uyo oliogudalahija, kunguno nuweyi agaidalahaga imilimo ya bhiye iyo adaidulile nulu uguyitumama. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “kanigo ka ng’habhi kagangoya nsabhi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza ni kujo ukumilimo ya bhichabho, kugiki bhadule gutumama milimo yabho chiza, umuwikaji bhobho.

Mathayo 6:1-4.

KISWAHILI: KIFURUSHI CHA MASKINI KILIMUADHIRI TAJIRI.

Walikuwepo watu wawili walioishi kwenye kijiji fulani, mmoja alikuwa tajiri, na mwingine maskini. Yule maskini alikuwa na kifurushi chake ambacho alikiweka chini. Tajiri akakidharau kifurushi hicho akisema, “kipishe kifurushi chako nipite.”

Yule maskini alimjibu, “kiinue tu ukiweke pembeni.” Tajiri huyo, alijaribu kukiinua kile kifurushi akakishindwa hata kukitikisa. Yeye aliona aibu sana aliposhindwa kukiinua hicho kifurushi. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “kifurushi cha maskini kilimuadhiri tajiri.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujiaibisha mwenyewe kwa kuzidharau kazi za wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hazielewi thamani na faida za kazi za wenzake, kwa sababu ya dharau yake hiyo, maishani mwake. Yeye huendelea kujiaibisha mwenyewe kwa kuumbuka baada kushindwa kuzitekeleza kazi hizo za wenzake, alizozidharau kabla ya kuzitekeleza ili aufahamu ugumu wake.

Mtu huyo, hufanana na tajiri aliyeshindwa kukiinua kifurushi cha maskini alichokidharau, kwa sababu naye huzidharau kazi za wenzake, ambazo hata haziwezi kuzitekeleza. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kifurushi cha maskini kilimuadhiri tajiri.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na hekima ya kuthamini kazi za wenzao, katika maisha yao, ili waweze kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Mathayo 6:1-4.

kanigo

kanigo1

ENGLISH: A POOR MAN’S BAG ASHAMED THE RICH.

There were two people who lived in a certain village. One was a rich one while the other was a poor who had his own package which he put down. The rich man scoffed at the package, saying, “Pick up your package and let me pass.”

The poor man replied, “Just lift it up and put it aside.” The rich man, however, tried to lift the parcel and could not even shake it. He was very embarrassed when he failed to pick up the package. That is why people told him that “a poor man’s bag ashamed the rich.”

This proverb is likened to a man who humiliates himself by despising the work of his fellows, in his life. This man does not understand the value and benefits of the work of his colleagues, because of his contempt in his life. He continues to humiliate himself by being miserable after failing to carry tasks of his colleagues, which he despised before doing them enough to understand their difficulties.

This person is like the rich man who failed to pick up the poor man’s package, because he also despises the work of his fellows, which he cannot even perform. That is why people say to him, “a poor man’s bag ashamed the rich.”

This proverb teaches people on the wisdom of valuing the works of others in their lives, so that they can fulfill well their daily responsibilities in their societies.

Matthew 6: 1-4.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.