791. ISABHO JIDOKAJIYAGWA.

Aliyoyi munhu umo uyo oli nsuluja omajikolo mingi. Umunhu ng’wunuyo, ohayaga ajikwije ihela mpaga jokale. Kuyiniyo lulu, lushigu lumo aja munhu gujulomba bhugunanhwa kuli weyi aliyomba, “naliomba unigunane hela nagagulile jiliwe ja gulya aha kaya yane.” Unsuluja ng’wunuyo, ashosha, “nadudula ugugwinha kunguno natali ugujikwija ihela jinijo.”

Aho ntondo yaho, unombi o wambilijiwa ng’wunuyo agalomba hangi, “naliomba unigunanage lulu ilelo ulu ojikwijaga ihela jinijo.” Unsuluja ng’wunuyo, agalema hangi aliyomba, “natali ugujikwija, ulu nujokaja nagugugunana.”

Oganoga nose uhabhipa unsuluja ng’wunuyo, adangunanile umunhu uyo olombaga bhugunanhwa. Ahikanza linilo, agandya gushoga gwizuka giki, ninga niongunana umunhu uyo alina makoye ng’wunuyo, aho oli najo ningi isabho. Hunagwene abhanhu bhang’wila giki, “isabho jidokajiyagwa.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adabhagunaga abhiye abho bhagajaga gujunomba kuli weyi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajidalahijaga isabho ijo alinajo bhuli ikanza. Uweyi ahayile ajikuminge isabho mpaka jikwile hunawandye ugubhambilija abhiye, kunguno adadebhile igiki, adulile gucha, nulu guhabhipa ahashigu ijahabhutongi.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsuluja uyo agalema ugungunana umunhu uyo olina makoye, kunguno nuweyi adabhagunanaga abhanhu abho bhagajaga gujunomba abhambilije, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “isabho jidokajiyagwa.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guzunya gubhagunana abho bhagalombaga wambilijiwa ubho bhalibhuduja, kugiki bhadule, kupandika mbango ja kubhiza na matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

2Wakorintho 8:12-13.

Luka 21:1-4.

KISWAHILI: MALI HAZIJAZWI.

Alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa mfanya biashara wa vitu vingi. Mtu huyo, alitaka kukusanya pesa mpaka zijae. Kwa hiyo basi, siku moja maskini alienda kuomba msaada kwake akisema, “naomba unisaidie pesa nikanunulie chakula ili niweze kula nyumbani kwangu.” Mfanya biashara huyo alijibu, “siwezi kukusaidia kwa sababu pesa hazijawa nyingi.”

Kesho yake, yule maskini alimuomba tena, akisema, “naomba unisaidie basi kwa siku ya leo kama hizo pesa zimekuwa nyingi.” Yule mfanya biashara alikataa tena akisema, “pesa hazijawa nyingi, nikizijaza nitakusaidia.” Mwishowe, yule mfanya biashara alifilisika, mpaka akaanza kukumbuka kwamba, angemsaidia yule maskini alipokuwa na mali. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “mali hazijazwi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukataa kuwasaidia wahitaji wale wanaomumba msaada wake, katika maisha yake. Mtu huyo, huendelea kuidharau mali anayoipata maishani mwake. Yeye hutaka akusanye mali nyingi zaidi ndipo akubali kuwasaidia maskini, kwa sababu ya kutokuelewa mwisho wa maisha yake, na kile kitakachompata kwenye siku mbeleni.

Mtu huyo, hufanana na yule mfanya biashara aliyemnyima yule maskini msaada alioumba kwake, kwa sababu naye, huwanyima wale wanaomwendea wakiomba msaada wake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mali hazijazwi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kukubali kuwasaidia wahitaji wanaoomba msaada kutoka kwao kwa kile wanachoweza kuwasadidia, ili waweze kupata Baraka za kufanikiwa zaidi, maishani mwao.

2Wakorintho 8:12-13.

Luka 21:1-4.

cattle

sheep3

goats3

ENGLISH: WEALTH IS NOT FILLED (MONEY IS ALWAYS NOT ENOUGH).

There was one man who was a merchant of various things. He wanted to raise money until it was full. So one day a poor man went to him asking for help, saying, “Please help me to buy food so that I can eat at home.” The businessman replied, “I cannot help you because there is not much money.”

The next day, the poor man begged him again, saying, “Please help me some for today if that money is full.” The businessman again refused, saying, “I don’t have much money, if I fill it up I will help you.” Eventually, the businessman went bankrupt, until he began to realize that he could help the poor man when he was rich. That is why people said to him, “wealth is not filled (Money is always not enough).”

This saying is likened to a person who refuses to support the needy who seek his assistance in his life. Such person continues to despise the possessions he acquires in his life. He wants to accumulate more wealth and then he will start helping the poor, because he does not understand the end of his life, and what will happen to him in the future.

This person is like the businessman who refused to help the poor person who asked help from him, because he too denies those who approach him seeking help in his life. That is why people say to him, “wealth is not filled (Money is always not enough).”

This saying instills in people an idea of helping the needy who need help from them in what they can support them with, so that they can receive blessings of greater success in their lives.

2 Corinthians 8: 12-13.

Luke 21: 1-4

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.