188. NAGUKOYELAGA IGEMBE

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo ugubhejaga igembe lya kulimila, bho gulikomela chiza aha npini golyo, kugiki lidule gudama. Iligembe linilo ulu lyudama chiza ligung’wambilija unimi o ngunda, nulu unimiji ongese, umugutumama nimo ntale mulikanza liguhi. Gashinaga iligembe ilikomezu lidulile gutumama nimo ntale mulikanza liguhi.

Aliyo iligembe ulu lyunega, ligakolokagaga na gufuma umunpini golyo. Hunagwene abhanhu bhagakomelaga amagembe gabho, kugiki gadame chiza ijinagugalimila umumigunda yabho. Umunhu uyo alilikomela iligembe linilo, ulu ubhujiwa giki ‘ulitaki?’ Agashoshaga giki, ‘nagukomelaga igembe.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agunangaga ng’wana okwe higulya ya gutumama milimo, kugiki amane uguitumama chiza. Ugunanga milimo chiniko ng’wana ng’wunuyo, ilenganilile na gulikomela iligembe lidame aha npini golyo, mpaga lyoye ugunega.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kubhalanga gumana kutumama milimo chiza abhana bhabho, pye na bhose abho b’agikalaga aha kaya yabho, kugiki bhadule gubhiza bhatumami bhakamu wa milimo.

Yigelelilwe abhabhyaji, bhang’walimu, na bhatongeji bha bhanhu, bhabhalange abhanhu bhab’o mpaga bhadebhe uguitumama chiza imilimo ya bhuli lushigu, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi aga jikolo ja gudula gutumila kumakanza malihu umukaya jabho.

Luka 2:41-51.

KISWAHILI: NAKOMELEA JEMBE

Chanzo cha msemo huo chaangalia mtu atengenezaye jembe lake kwa kulikomelea kwenye mpini ili lishikane vizuri na mpini huo, kiasi cha kutosha kulilimia bila kulegea kwa muda mrefu.

Jembe hilo likishikana vizuri na mpini wake, litamsaidia mkulima wa shamba na mpaliliaji wa palizi, kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi. Kumbe jembe lililokomelewa vizuri laweza kutumika shambani kwa kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi.

Lakini jembe likilegea, hukongoloka na kutoka kwenye mpini wake. Ndiyo maana watu hukomelea mapembe kwa kuyatengeneza vizuri ili yashikane vizuri na mpini kiasi cha kutosha kuyalimia kwa muda mrefu kwenye mashamba mbalimbali, bila kulegea. Mtu atengenezaye jembe hilo akiulizwa kwamba ‘unafanya nini?’ Yeye hujibu ‘nakomelea jembe.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu afundishaye mtoto wake juu ya kufanya kazi kwa bidii ili afahamu vizuri. Lengo lake ni kumwezesha mtoto huyo, kuwa mfanyakazi mwenye bidii katika maisha yake, kwa ajili ya kujiletea maendeleo makubwa katika familia na maishani mwake.

Kumfundisha mtoto namna hiyo, hulingana na kukomelea jembe kwenye mpini wake kwa kulitengeneza vizuri kutosha kulifanyia kazi shambani ili lisilegee, bali liwe imara.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwapa malezi ya kufanya kazi kwa bidii, watoto wao, na wote waishio kwenye familia zao, ili waweze kuwa wafanyakazi wenye bidii maishani mwao.

Yafaa wazazi, walimu, na viongozi wote wawalee watu wao vyema kwa kuwafundisha namna ya kuwa wafanyakazi hodari maishani mwao, ili waweze kujipatia mapato ya kutosha kuziendeleza familia zao.

Luka 2:41-51.

girl-with mother

ENGLISH: I’M FIXING THE HOE

The overhead saying focuses on the act of fastening a hoe in its handle to make it firm enough for effective cultivation, and to prevent it from becoming loose easily.

If the hoe is tightened well in its handle, the farmer is able to accomplish a great job in a relatively shorter time.back-pain

But if the hoe is loose in its grip, it turns round the handle and easily comes off. That is why people are always fixing their hoes to make them sturdy enough to cope with the long weeding periods in the fields. Asked what he/she is doing, the maker of the hoe would respond by saying, ‘I’m fixing the hoe.”

That saying is comparable to a person who teaches his/her child on how to work hard in life, with the aim of instilling in him/her the virtue of hard work for self and family development.

Teaching a child that way is akin to fixing a hoe in its handle to make it strong enough to do the fields without falling off.

The adage is used to encourage sound upbringing of children, making them appreciate and practice hard work in their lives and in their families.

It is important for parents, teachers and all leaders in general to teach people to embrace hard work. This would enable them earn enough income to sustain their families.

Luke 2: 41-51.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.