119. NONI NA LYIMBO

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

119. NONI NA LYIMBO

Diyu imo bhanhu bha mu chalo jise bhagamisa bhogwipunha noi. Bhagandya gulima ngunda gwise. Umuchalo jise olihoi ng’wana umo uyo witanagwa, Furaha (bhuyegi). UFuraha olatogilwe gumisha dilu noi guti na bhabyaji bhakwe umo bhamisijaga. Ulushugu lunulo abhabyaji aho bhamisa nanghwe agamisha.

Aliyo uwei adajile ugujulima ukundunda, agasaga hakaya agwigushaga. Ahowela hadoo agigwa lyimbo linonu noi ilo noni jimbaga mimbo gajo. Agigwa uyega na gukumwa uguligwa ilyimbo ilinonu giko noi.

Loli lukangala lokwe lo gwandya ugwigwa giko. Agilalangija bhuli lwande, kugiki wibhone inoni yiniyo. Adibhonile wangu kulwa nguno yaliib’isa mumatambi ga linti litale.

Adanogile uguichola. Agandya gunchola ng’wana ng’wiye uyo witanagwa Amani. Nanghwe agamona uFuraha agulolaga mulinti, umuja, “Furaha ugulolaga kiyi?” UFuraha agashosha, “Nagulolaga noni imo iyo ilimba lyimbo linonu noi.” Amani umuja, “Ilihei nadibhonaga?” Furaha agashosha, “Yalinahenaha linti linili.” “Ilimba ginehe?” Agabhuja uAmani. “Ihaha yoyaga ugwimba. Hamo yadogohaga. Aliyo yalimbaga giki. ‘Mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka.’”

UAmani agatogishiwa noi ni mihayo ya lyimbo linilo. Agashika uhaya nanghwe wibhone inoni yiniyo.

Kubahati ya wiza, inoni yiniyo yalihoi umulinti linilo yahumula sele. Yamanaga yubhalola uFuraha nu Amani umobhalikoyela. Aho yabhona giki bhahaya gugwa ngholo, igandya ugwimba;

 “Mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka.”

Abhana bhenabho bhagayeka noi uguligwa ilyimbo linilo. Hangi uAmani ahaooligwa agayomba, “Lo! Gashinaga nghana ilimba lyimbo linonu noi. Ehe, lililyimbo linonu noi. Nzugu uilole umo yili. Yiliyapi, ubhoya bhoyo bhunogoleku niyo ili nisunzu lwawiza noi ukuntwe goyo.” UFuraha agayomba.

 “Ndugu one, ilelo duli na bahati ya gwigwa lyimbo linonu giti linili.” Agayomba uAmani. Oganoga umuja uFuraha “imihayo yose yiniyo iyawiza ilinabhulingisilo ki?”

UFuraha agashosha, “Ha! udamanile? Nulu hadoo, lindaga naguwile. Ubhulingisilo bho lyimbo linili ni giki:

 “Mvivu shika jembe, (Nkokolo dimaga igembe), mvivu shika jembe, (Nkokolo dimaga igembe),  mvivu shika jembe.” (Nkokolo dimaga igembe),

“Abheja noi,” Agalumbilija uAmani.

Inoni yiniyo igalala yuja kumigunda ukunu igwimbaga ilyimbo lyayo linilo.

UFuraha nu Amani bhagendelea ugwimba ilyimbo linilo kulushuku lugima. Abhabyaji bhabho aho bhashoka ugufumila ukundunda bhagawigwa abhana bhabho bhose wagwimbaga umuchalo,

“Mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka.”

Bhagakumya kulwa nguno ilyimbo linilo ligimbagwa na noni. Bhadamanile ni nani uyoobhalangaga abhana bhenabho. Ilyimbo linilo lyimbagwa na noni bhuli ng’waka. Aliyo lyimbagwa mumakanza ga malima duhu.

Abhanhu ulu bhumala ugulima, inoni yiniyo yingikaga gete, nuko yajaga, olinduhu uyo olamanile. Bhuli ikanza lya malima ulu lyashika inoni yiniyo yizaga na gwimba ilyimbo lyayo linilo.

Abhanhu bhazunije giki, inoni yiniyo igizaga gubhokomeleja abhagokolo bhalime.

 

KISWAHILI: NDEGE NA WIMBO

Asubuhi moja watu wa kijiji chetu waliamka mapema sana. Walianza kulima shamba letu. Katika kijiji chetu palikuwa na mtoto mmoja jina lake Furaha.

Furaha alipenda kuamka asubuhi sana, kama wazazi wake walivyokuwa wakiamka. Siku hiyo wazee walipoamka, naye aliamka pia. Lakini yeye hakuenda kulima shambani, alibaki nyumbani akicheza. Kulipopambazuka kidogo alisikia wimbo mmoja mtamu sana wakati ndege walipokuwa wakiimba nyimbo zao.

Alisikia akafurahi, kisha alishangaa kuusikia wimbo mmoja mtamu sana. Ilikuwa mara yake ya kwanza kuusikia. Alitazama kila upande ili amtazame na kumwona ndege yule. Hakumwona upesi kwa sababu alijificha katika matawi ya mti mkubwa.

Hakuchoka, bali alianza kumtafuta mtoto mwenzake aliyeitwa Amani. Naye alimwona Furaha akitazama mtini, alimwuliza, “Furaha unatazama nini?” Furaha alijibu, “Natazama ndege mmoja ambaye anaimba wimbo mtamu sana.” “Yuko wapi simwoni? Aliuliza Amani. “Alikuwa kwenye mti huu.” Furaha alijibu. “Anaimba namna gani?” Amani aliuliza.  Furaha akajibu, “Sasa ameacha kuimba. Labda anatuogopa sisi,  lakini anaimba hivi,

“Mwolo kola ichaka,  mwolo kola ichaka,  mwolo kola ichaka.”

Amani alipendezwa sana na maneno ya wimbo ule. Alifika akataka naye amwone yule ndege. Kwa bahati ndege yule alikuwa yuko mtini katulia kimya. Alikuwa akiwaangalia Furaha na Amani wanavyohangaika. Halafu alipoona kwamba wanataka kukata tamaa, alianza kuimba;

“Mwolo kola ichaka,  mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka.”

Watoto wale walifurahi sana kuusikia wimbo ule. Tena amani alipousikia alisema, “Lo! Kumbe kweli anaimba wimbo mzuri sana.”

“Ndiyo  huo ni wimbo mzuri sana. Njoo umtazame alivyo. Ni mweusi, manyoya yake mororo na ana kishungi kizuri sana kichwani pake.” Furaha alisema. “Ndugu yangu leo tuna bahati ya kusikia wimbo mtamu kama huo.” Amani alisema, kisha alimwuliza Furaha maneno yote hayo matamu yana maana gani? Furaha alijibu, “Ha! Hujui? Hata kidogo, ngoja nikueleze maana ya wimbo huo ni hivi;

“Mvivu shika jembe, mvivu shika jembe, mvivu shika jembe.”

“Asante sana,” Amani alishukuru. Yule ndege aliruka akaenda shambani akiendelea kuimba wimbo wake. Furaha na Amani waliendelea kuuimba wimbo huo siku nzima.

Wazazi wao waliporudi kutoka shambani waliwasikia watoto wote wa hapo kijijini wakiimba,

“Mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka, mwolo kola ichaka.”

Walishangaa, maana wimbo ule huimbwa na ndege. Hawakujua ni nani aliyewafundisha watoto wale. Wimbo ule huimbwa na ndege kila mwaka. Lakini huimbwa wakati wa kilimo tu.

Watu wakisha kulima, basi ndege  yule hutoweka  kabisa, anakokwenda hakuna anayejua. Kila kipindi cha kilimo kinapoanza, naye huja kuimba wimbo wake huo. Watu wanaamini kwamba, ndege yule huja kuwahimiza wavivu walime.

tree bird

boys-

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.