82. Ntale Osi Nyerere Na Nzala

Collected by: Don Sybertz,
With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Ng´waka 1974 Itanzania igabhiza ni yanga lwa nzala. Bhanasi bhagayisaila iSelekari kulwa nguno ya kugaiwa ginhiwa jiliwa. Iki jiliwa ja nzala jalijahujumiwa na bhanhu abho bhagimana bhoi duhu.

Ku iniyo, abhanasi bhagapandika iyange itale. Jililo ja abho abhatina nguvu, jiganshigila úntale o si, ung´walimu Julius Nyerere.

Aho owigwa ubhulalamiki bhobho, wamua gugayelela ama mabhelele gose ayo gatumikaka umugujitula ijiliwa ja gubhagabhila bhule ung´wishirika lya si lwa bhushisha (NMC).

Lushiku lumo aho ali kunjini go Shinyanga, Ung´walimu agita jito ja gubhashesha abhanhu, ja guzwala majitambalala makulukulu na ngofila ubhi giti munhu ung´wilombeleja.

Aho oshika aha nyango go NMC, nduhu munhu nulu umo uyo agamhana. Wishebeleja lumo na lumo mpaga mu ofisi ya ng´wa meneja, bho nduhu guzunulijiwa tamu.

Agapiga hodi aha nyango na guhamuka aliyomba, “Aying´we bhanhu umugati umo!” “Nambilijagi, natina jiliwa ukukaya yane!” Meneja unshokeja, “Lekaga gudukoya namhala ebhe! Ingaga ahenaha! Jaga jako uko isoko ugigulile ijiliwa. Kihamo ni iniyo, Nyerere agendelea gubhikumbilija, “Bhabehi, nambilijaji! Nagucha na nzala.”

Aliyo bhadandegelekile, umeneja na bhambilija bhakwe, bhagendelea kujinja mubei ya higulwa na bhasuluja abha bhagashika ho gugula ijiliwa jenijo ja nzala, ijo jalijidakililwa kugabhanyiwa bhule ku bhanasi abho bhalibhadinajo.

Gashinaga ili nghana igiki,
Uo lwiguto adanmanile uo nzala.

Inghalikilo yaho, Unyerere agagufungula unyango na gwingila muofisi. Wangu wangu agakungula amajitambalala na ngofila yenuyo, na heneho, wimanyicha kubhoi igiki ali nani, bho nduhu guyomba mhayo gosegose. Pye bhuding´wa na bhujinjimazu, bho gukumya!

Aho Ntale osi Nyerere oshoka Dar es salama, igatangajiwa giki, umeneja ng´wenuyo na bhambilija bhakwe, bhapejiwagwa imilimo ya gubhatumamila abhanhu kulwa nguno ya juhuma iyo bhagiyita.

Tukio La Rais Nyerere Na Njaa
Mwaka 1974 Tanzania iliandamwa na janga la njaa. Wananchi waliilalamikia serikali kwa vile walikosa kupewa chakula. Kwani kile chakula cha njaa kilihujumiwa kwa maslahi ya watu binafsi.

Hivyo, wananchi walipata usumbufu mkubwa. Kilio cha wanyonge kilimfikia Rais Mwalimu Julius Nyerere. Baada ya kuyasikia malalamiko yao, akaamua kuyatembelea maghala yote yaliyotumika kuhifadhia chakula cha kugawa bure kwenye shirika la Taifa la Usagishaji (NMC).

Siku moja akiwa mjini Shinyanga, Mwalimu Nyerere alifanya vioja kwa kuvaa matambara na kofia kuukuu kama omba omba. Alipowasili kwenye lango la NMC, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kumtambua. Akajipenyeza moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya meneja, bila ya kupata kibali kwanza.

Alipiga hodi mlangoni na kupaza sauti akisema, “Enyi watu ndani humo!” Nisaidieni, sina chembe ya chakula nyumbani kwangu!” meneja akamjibu, “Acha kutubughudhi mzee wewe! Ondoka hapa! Nenda zako huko sokoni ukajinunulie chakula. Hata hivyo, Nyerere aliendelea kuwasihi, “Jamani, nisaidieni! Nitakufa kwa njaa.

Lakini kwamwe hawakumsikiliza, badala yake, meneja na wasaidizi wake wakaendelea kulangua na wafanyabiashara waliofika kununua kile chakula cha njaa ambacho kingepaswa kugawiwa bure kwa wananchi wahitaji.

Kumbe ni kweli kwamba:
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Mwishoni, Nyerere aliufungua mlango na kuingia ofisini. Ghafla akavua yale matambara na ile kofia, na hapo hapo akajidhihirisha kwao kuwa ni nani, bila ya kusema neno lolote. Wote walishikwa na butwaa!

Baada ya Rais Nyenye kurejea Dar es Salaam, ilitangazwa kwamba yule meneja na wasaidizi wake waliwajibishwa kwa kufukuzwa kazi kwa hujuma.

Kiswahili: Tukio La Rais Nyerere Na Njaa

Mwaka 1974 Tanzania ilikumbwa na janga la njaa. Wananchi waliilalamikia Serikali kwa vile walikosa kupewa chakula. Kwani  kile chakula cha njaa kilihujumiwa kwa maslahi ya watu binafsi.

Hivyo, wananchi walipata usumbufu mkubwa. Kilio cha wanyonge kilimfikia Rais Mwalimu Julius Nyerere. Baada ya kuyasikia malalamiko yao, akaamua kuyatembelea maghala yote yaliyotumika kuhifadhia chakula cha kugawa bure kwenye shirika la Taifa la Usagishaji (NMC).

Siku moja akiwa mjini Shinyanga, Mwalimu Nyerere alifanya vioja kwa kuvaa matambara na kofia kuukuu (iliyochakaa) kama omba omba. Alipowasili kwenye lango la NMC, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kumtambua. Akajipenyeza moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya meneja, bila ya kupata kibali kwanza.

Alipiga hodi mlangoni na kupaza sauti akisema, “Enyi watu ndani humo!” Nisaidieni, sina chembe ya chakula nyumbani kwangu!” meneja akamjibu, “Acha kutubughudhi mzee wewe! Ondoka hapa! Nenda zako huko sokoni ukajinunulie chakula. Hata hivyo, Nyerere aliendelea kuwasihi, “Jamani, nisaidieni! Nitakufa kwa njaa.

Lakini kamwe hawakumsikiliza, badala yake, meneja na wasaidizi wake wakaendelea kulangua na wafanya biashara waliofika kununua kile chakula cha janga la njaa, ambacho kilipaswa kugawiwa bure kwa wananchi wahitaji.

Kumbe ni kweli kwamba:

Mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Mwishoni, Nyerere aliufungua mlango na kuingia ofisini. Ghafla akavua yale matambara na ile kofia, na hapo hapo akajidhihirisha kwao kuwa ni nani, bila ya kusema neno lolote. Wote walishikwa na butwaa!

Baada ya Rais Nyerere kurejea Dar es Salaam, ilitangaza kwamba yule meneja na wasaidizi wake waliwajibishwa kwa kufukuzwa kazi kwa hujuma.

begging-

English: President Nyerere Disguises Himself as a Beggar

In 1974 Tanzania had a serious famine. The government provided famine relief, but the food was not getting to the people who complained to the authorities. The President of Tanzania, Julius Nyerere, heard about the complaints and decided to visit all the storehouses of the National Milling Company (NMC) where the food was being kept.
One day Nyerere visited the NMC in Shinyanga. He disguised himself as a beggar wearing worn out clothes and an old hat. When he arrived at the gate of the NMC no one recognized him. He passed through the gate without permission and went straight to the office of the manager. He knocked on the door and yelled out, “Hey, you people in there. Help me. I don’t have any food.” The manager answered, “Stop bothering us, old man. We don’t have any food here. Go to the market and buy some for yourself.” As the African proverb says: A satisfied person does not know the hungry person.
Nyerere continued to cry out, but no one paid any attention. The manager and his assistants were busy with some local business men who were buying the famine relief food that was supposed to go to the Tanzanian people. Finally Nyerere opened the door and walked into the office. He immediately took off his hat and made himself known. Needless to say, the manager was speechless.
After President Nyerere returned to Dar es Salaam, it was announced that the manager of the NMC in Shinyanga had been fired together with some of his assistants.

child

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.