Songs

71. Ng’osha Ya Welelo Iliyiyene (Wiyene)

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Mhayo gwenuyo gugakumuchiwa (gukakumuchiwa) na bhagalu aho sabho bhuhemba, Gumha, wacha. Hang’wa Gumha, yaliho ng’hungulume ya Ngoko yalalaga kukisunzu sha numba, ulu bhalogi bhiza, nayo yahilaga.

Uluyahila abhalogi bhaluma nhambo bhajile (tukubhonwa), wangaluka ubhujiku. Nose abhagalu bhose bhali bhamana giki atiho wakumulaga Gumha. Aho Gumha wacha, abhagalu bhose bhuyuhaya giki, “Ng’wenuyu winjiwa kunu kunze na Liwelelo iti bhalogi”.

Niyo gashi, Ing’osha ya Welelo ili yiyene, nachene ikantwala na Ib’ambangulu na ng’wana Malundi, nu jinamhala wa ng’wa Wande ungika.

Kiswahili: Mwanamume Wa Ulimwengu Yuko Peke Yake

Neno hilo lilienezwa na kundi la ngoma lijulikanalo kama “Wagalu” walipoona baba yao wa madawa, aliyejulikana kama “Gumha” amekufa. Kwa Gumha, kulikuwa na Jogoo aliyekuwa akilala kwenye kilele cha nyumba, kama wachawi wakija, naye aliwika (walivyoamini wao).

Alipowika wachawi walitimua mbio wakienda (kwa kadiri ya wao walivyoamini), wakisema “tutaonwa” kumbe kunakucha. Mwishowe, Wagalu wote walifahamu kwamba, hayupo wa kumuua Gumha. Alipokufa Gumha, wagalu wote wakawa wanasema hivi, “Huyo ameondolewa huku nje na Mwenyewe, (Liulimwengu) sio wachawi.”

 Kumbe, Mwanamume wa Ulimwengu yuko peke yake. Ndiyo maana ilimchukua na Ibambangulu na Ng’wana Malundi, na mzee wa Wande Mgika (Kundi jingine pinzani na lile la wagalu).

people-

ENGLISH: THE MAN OF THE UNIVERSE IS ALONE

That word was spread by a group of “Drum dancers” known as “Wagalu” when they witnessed heir medicineman, known as “Gumha” to have died. With Gumha, there was a cock which used to be lying on the roof of the house.When witches came and it crowed (according to what they believed).

When it crowed, the witches ran away(according to what they believed).The witches could say,“We will be seen.It is already morning.” Finally, all the Wagalu knew that, there was no one who could kill Gumha. When Gumha died, all the Wagalu were saying, “He has been taken from here by Himself, (the man of the World) and not sorcerers.”

  After all, the Man of the World is alone. That is why he took even Ibhambangulu and Ng’wana Malundi, and an old Wande Mgika (another opposing group to that of the wagalu).

70. Jigano Ja Ng’hwimi – Jitegile

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Aho kale alaliho munhu umo uyo witangwa Jitegile. Witanagwa giko kunguno alatogilwe kutega ndimu, noni, na shingi shose isho jikomile gutegwa.

Lushiku lumo agaja gujutega ng’wipolu, aho watega lukangala lwa kwandya upuja kagi. Nako kagi guntayila gete akalekeje ajidugabhulaga. Jitegile nang’hwe uzunya ukalekela akagi.

Lushiku lwa kabhili upuja ganoni, nakene kung’wila nigiko, nanhwe ukalekela. Lushiku lwa gadatu upuja kalung’wando, nako kunomba gukalekeja, nang’hwe wita nichene. Na lushiku lwa kane upuja mhuli, nayo yunomba nigiko, nang’hwe wilekeja.

Aho jabhita shiku ningi, lushiku lumo jitegile ubhucha nhola na ukampandika ng’waniki wa kuntola. Aliyo mpaga tamu ashigilije malagilo ayo gali madamu gete.

Lilagilo lya kwandya ng’waniki uyo wali wantogwa agagulanyiwa mu bhaniki bhingi, abho ali ikolile nabho gete. Jitegile agawilwa anchagule uyo ali okwe.

Aho wali atali wilalangija ung’wiganda lyenilo, Kagi kagiza mpaga ha matu gakwe, kung’wila giki, “Uyo nalagandane nang’hwe, ulu uginga na nkono hu ng’wene nsolege, nako akagi kulala mpaga kugagwila hagutu gwa ng’waniki uyo Jitegile akantogwa kwandya. Nang’hwe akipuga ha gutu, haho na haho Jitegile ubhiza wahebha ilagilo lyenilo na upila kubhulagwa.

Lushiku lungi lo kabhili agawilwa kukong’onha bhusiga ubho bhugitwa igunila igima. Haho na haho, aho wandya duhu kusong’onha kanoni kagiza na bhiye bhugombagula bhusiga pye ubhose, na kubhuswila ng’wigunila nyenilo makanza maguhi duhu.

Jitegile uhebya ilagilo lyenilo, hangi upila ugubhulagwa. Lushiku lungi lwa kadatu uwilwa kuditila lyochi mjisabo, aha wafuma hanze kujuyela ng’wipolu, akamanhya na kasayayi, nako kumuja, “Bhageshi Jitegile, ulikobha Ki?” Nang’hwe ushosha, “Nalikobha isala lya kuditila lyochi mjisabho.” Nako kasayayi kung’wila Jitegile giki, “Nukulanja isala.

Kiswahili: Hadithi Ya Mwindaji – Vilivyotegwa

Hapo  zamani kulikuwa na mwindaji mmoja ambaye alikuwa anatega wanyama. Mawindo hayo yalisaidia sana maisha yake. Siku moja mwindaji huyo alimunasa mnyama Mhanga.

Lakini mnyama huyo alimsihi na kumbembeleza sana akisema, “Bwana unihurumie nami nitakusaidia wakati wa shida zako.” Mwindaji  huyo akafikiri na akajiinamia, baadaye mnyama huyo akamwachilia. Akatega tena mtego wake, akakuta amenasa mdudu (Inzi).

Mwindaji huyo akawa na mawazo mengi sana akafikiri moyoni na kusema, “Balaa gani  mtego wa mnyama anaswe Inzi?” Hapo Inzi hakujua ni kitu gani anafikiri. Mwindaji akaamua kumwua tu huyo Inzi.

Inzi akamsihi asimuue akamwambia, “Unihurumie nami nitakusaidia baadaye.” Inzi huyo akaachiliwa akaenda. Naye mwindaji hakukata tamaa akaendelea na uwindaji tu.

Baba yake na yule mwindaji akamwambia atafute mwanamke wa kuoa. Akaenda  hata akafika katika familia ya Mtemi na akamwona hapo mwanamke wa kuoa, akampenda, hivyo akamposa na wakakubaliana. Mwindaji huyo akarudi nyumbani kutoa taarifa yake. Akamwambia babaye, “Nimeposa kwenye familia ya Mtemi fulani.”  Baba yake akaenda kwa Mtemi kupangiana mahari. Nao pia wakaelewana, Mtemi akachukua mahari.

Baada ya siku chache mwindaji huyo akaenda kwa wakwe zake kumfuata mke wake. Alipofika alitoa hoja kuwa, “nimekuja kumchukua mke wangu twende nyumbani.”  Mtemi akamshukuru na kumpa mashariti  magumu kama ilivyokuwa desturi yao.

Akamwambia basi kesho utashinda hapa na nitakuruhusu tu. Mtemi akachinja ng’ombe mmoja na kuwaamuru watu wampike ng’ombe huyo bila kubakiza aina yoyote ya nyama, na ilipoiva akapelekewa nyama yote huyo mkwe (mkwilima mwindaji) ili asipoimaliza auawe, tena asiweze kumchukua mke wake. Basi akiwa ndani ya chumba kizuri pamoja na mshenga wake akaanza kulia tu, huku akijifikiria ni jinsi gani atapona.

Mara Mhanga akajitokeza bila kujua ametokea wapi na kuambiwa, “Usisumbuke na hali hii tu, nitakusaidia.” Mhanga  akachimba shimo ndani ya nyumba na kumwambia,  “Haya mwaga nyama yote ndani ya shimo hili.” A kafanya kama alivyoambiwa.

Mhanga  akalifukia shimo hilo, mwindaji akawa na furaha sana na Mhanga akatoweka hapo hapo. Watumishi wa Mtemi walifuata vyombo walikuta nyama yote imekwisha wakasitaajabia. Na Mtemi (mfalme) alipoona hivyo akastaajabu sana na kujisemea moyoni, lipi basi atalishindwa, ng’ombe mzima amemalizwa na watu wawili tu. Ajabu zipo.

Mtemi akamwita mkwe (mkwilima) wake akamwambia, “basi mwanangu kesho utakwenda nyumbani baada ya chakula cha mchana.”  Kulipokucha  chakula kiliandaliwa mapema wakala.

Baada ya kula Mtemi akamwambia mkwe (mkwilima) wake, “Mchague mkeo kati ya wanawake hawa watatu.” Mmoja alikuwa mama mkwe wake ambaye alifanana sana na binti yake. Na wadogo zake na mke wake wawili waliofanana pia. Hilo ni jaribio la pili nala mwisho. Mtemi akawaambia wajipange na mkwe (mkwilima) achague mke wake.

Jinsi walivyokuwa wanafanana na jinsi nguo zao walivyovaa, akasema moyoni,  “Leo ni mwisho wangu tu.” Hapo katika kufikiri mara Inzi akaja akamwuliza, “Mbona una mawazo na unasikitika kiasi hicho?” Mwindaji akasema, “Nataka nimchague mke wangu, lakini wanafanana na mama mkwe na wadogo zake, nisipompata nitauawa.”

Inzi akasema, “Nitakayemwangukia jichoni na kunipunga kwa mkono huyo ndiye.”  Inzi akaruka mpaka kwa wanawake hao, naye akaangalia kwa makini.

Akatua kwa mke wake kama alivyosema na akapunga mkono. Mkwilima huyo akamchagua mara, na watu wakapiga vigelegele na kumsindikiza kwa furaha nyumbani.

africa-2

ENGLISH: THE STORY OF THE HUNTER – CACHED.

In the past, there was one hunter who used to trap animals. Those hunting activities were very useful in his life. One day, the hunter caught the wild animal.

But the animal begged and pleaded with him, saying, “Lord have mercy on me and I will help you in your time of trouble.” The hunter thought and released him. He rebuilt his trap and found the insect (the fly).

The hunter had so much thought and thought in his heart and said, “What is the curse? In the trap of an animal, you catch the fly?” Then the fly did not know what the hunter was thinking. The hunter decided to kill such fly.

The fly begged him not to kill him and said, “Have mercy on me and I will help you later.” The fly was let free.It went. And the hunter did not despair and went on hunting.

His father told him to find a woman to marry. He went to the family of the Chief and saw a woman to marry. He loved her, and so he engaged her and she agreed to marry him. The hunter returned home to inform his relatives. He said to his father, “I have passed over to the family of a certan Chief.” They went to arrange dowry.They agreed and the Chief took the dowry.

After a few days, the hunter went to his father-in-law to fetch his wife. When he arrived he said, “I have come to take my wife and go home with her.” The Chief thanked him and gave him the difficult conditions as was the custom.

He said to him,“Tomorrow,you will spend the whole day here and I am the one who will let you go.” The Chief slaughtered one cow and ordered the people to boil the bull without retaining any meat.When it was cooked, it was given to the son-in-law, as an attempt to kill him. He was told that he would die if he didnot finish the meat and he would not take his wife. So, the hunter remained in a nice room with his companion. He simply cried, while thinking about how he would solve the riddle.

Once Mhanga appeared without knowing where he came from and told the hunter, “Don’t worry about this situation, I will help you.” Mhanga dug a hole in the house and told him, “Take all the meat into this hole.” He did as he was told.

Then Mhanga ran out of the hole by covering it, and the hunter was very happy and Mhanga was gone. The crew’s staff followed the containers and found all the meat finished.They were very surprised. When the chief saw this, he was so astonished and spoke in his heart.Then he thought he would fail as the whole herd was finished by only two people. Wonders exist.

The chief then called his son-in-law and said, “Then my son tomorrow you will go home after dinner. The next day food was prepared.They ate.

After eating the Chief said to his son-in-law, “Choose your wife amongst these three women.” One was his mother-in-law who resembled her daughter very much. His two sister-in-laws also looked alike. That is the second and last trial. The Chief told them to arrange themselves and his son-in-law should choose his wife.

How they looked like the clothes they were wearing, he said in his heart, “Today is my end.” Then Inzi (the fly) came and asked, “Why are you thinking hard and you look sorry?” The hunter said,“I want to choose my wife but she looks likemy mother-in-law and her young ones. If I don’t identify her, I will be killed.”

The fly said, “The one into whose eye I’ll fall   that the one who will wave a hand is the one.” The fly flew down to the women, and she looked closely.

She stayed on the hunter’s wife as it had said. The son–in-law chose her without delaying, and the people shouted loudly and happily.They escorted him home.

69. NGOSHA UYO AKANGEMA NKE AMANE ULU ATOGILWE NG’HANA.

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Bhagosha bhabhili bhidimile bhusumba bhandya kwibhuja, gete abhake bhise bhatutogilwe? Ungi uhaya giki, nke wane, anitogilwe ng’hana.

Ng’wiye uhaya, “Hene witogwa wenubho bhuli wa ng’hana?” nsumba ng’wiye unshokeja, “Nakungema nahene ulu ng’hana anitogilwe, uhaya giki nache nandegeleke.”

Lushiku lumo bhali mu numba kihamo, ngoshi na nke. Ngoshi wali ha bhulili, nu nke nang’hwe waliwigashije hihi. Huna lulu ngosha ung’wila unke, “Nke wane nacha!” Nu ngoshi wichijisha (kwiyitya kiti uchile- kujifanya).

Nkima wahayubhona ngoshi wacha uhaya, “Nite kinehe lulu? Natubhaga no, ulu nandya kulila bhakwiza bhanhu bhanizwanje nikale na nzala gete nalye nigute tame, na nize nalile.

Huna lulu wandya kuzugija, aliyo ikubhi lyalilitiho, bhuki walibhusungile ha lusungo haho na bhulili. Nkima wihamba kusungula uduma iki wali nguhi, nose umpanda ungoshi wakwe mu ng’humbi na usola bhuki.

Aho wamala kulya na kwiguta wandya lulu ugulila bhiza bhanhu. Bhingila mu numba bhumuja, “Kinehe mayu?” Nang’hwe, “Ngoshi wane wachaga.”

Nsumba ng’wiye wa ngoshi ubhawila bhanhu giki, “Fumagi mo pye, nene nanagule, namanile bhugota wa kumpija. Bhusaga ho bhabhili umu numba, wandya kumuja ng’wiye, wabhona kinehe?

Iyo nabhona ya gukamaja, aho nkima wane wanibhona nacha, uhaya, “Umo natubhilaga umu ulu nandye kulila bhakwiza bhanhu bhanizwanje nikale na nzala, hambu hambu nazuge nalye nigute tame, huna lulu wandya kuzuga bhugali, aliyo ikubhi lyalilitiho. Bhuki wali bhusungile haho na bhulili, aho wihamba kwinja ulebha, nose wandya kunipanda mu ng’humbi.

Bhandya lulu guseka, aho bhanhu bhigwa bhaliseka bhuhaya, ng’wichiswe wapilaga lulu. Huna lulu ngosha ung’wila nke, “Gashinaga witogwa wako bhuli bhudo ng’hana, nkima aho wizuka isho witaga usunduhala no.

Kiswahili: Mwanamume aliyemjaribu mke wake afahamu kama kweli anampenda.

Wanaume wawili walikuwa marafiki sana. Siku moja wakaanza kuulizana. “Wake zetu wanatupenda kweli?”  Mmoja akasema kwamba, “Mke wangu ananipenda kweli.”

Mwenzake akasema, “Upendo wenu ni wa kweli kabisa?” Mwenzake akamjibu, “Nimwangalie mke wangu kama kweli ananipenda, akasema kwamba nife nimsikilize.”

Siku moja walikuwa ndani ya nyumba pamoja mume na mwanamke. Mme alikuwa kitandani, na mkewe alikuwa amekaa karibu. Kwa hiyo mme akamwambia mkewe, “Mke wangu nimekufa.” Na mme akajifanya amekufa.

Mwanamke alipoona mmewe amekufa akasema, “Nifanye nini sasa?” Muhimu nile kwanza nishibe ndo nilie.”  Kwa hiyo akaanza kupika. Lakini hakuwa na mboga, alikumbuka kuwa kuna asali ipo juu ya dali usawa wa kitanda.

Mwanamke alijaribu kuchukua ile asali, alishindwa maana alikuwa mfupi. Mwisho akapanda kitandani, akamkanyaga mmewe tumboni, na akachukua asali. Alipomaliza kula na kushiba akatoka nje kulia.

 Wakaja majirani, wakaingia ndani, wakmuuliza vipi mama? Kuna nini? Naye akajibu mme wangu amekufa.

Rafiki yake aliwaambia tokeni ndani nimponye maana najua dawa ya kumponya. Walibaki wawili ndani, akaanza kumuuliza mwenzake umeonaje sasa? Rafiki yake alimwambia aliyoyaona, mke wangu aliponiona nimekufa aksema, nilivyo na njaa hivi nianze kulia watakuja watu wanijaze mawazo nishinde njaa, afadhali nipike nile nishibe kwanza, ndio akaanza kupika ugali, ila mboga haikuwepo. Asali ilikuwa juu ya dali karibu na kitanda, alipotaka kutoa hakufikia, sasa akaona anikanyage tumboni.

Wakaanza kucheka sasa, watu waliposikia kicheko wakasema mwenzetu amepona. Mme ndo akamwambia mkewe kwamba, “Kumbe upendo wako ni mdogo kabisa.”  Mwanamke akakumbuka kile alichokifanya na kusikitika.

passed-out

vintage-

ENGLISH: LET ME TEST IF MY WIFE LOVES ME

Two men were very great friends. One day they began to ask each other. “Do our wives really love us?” One of them said, “My wife loves me.”

His companion said, “Is her love  true?” His colleague replied, “I will find out if my wife really loves me. I will pretend to be deadcand listen to her.”

One day,one of the men was in the house with  his wife. A husband was in bed, and his wife was sitting next to him. The husband said to his wife, “My wife I am dead.” And he pretended to be dead.

When the woman saw that her husband is dead, she said, “What am I going to do now?” The first thing I must do is eat enough food.Then I will start crying.”So she started cooking. But she discovered that she did not have vegetables.Then she remembered that there was honey on the roof just above the bed.

The woman tried to take the honey but she failed because she was short. Finally,she went up to the bed, stood her legs on the stomach of her husband, and took honey. When she had finished eating and satisfied,she went out and started crying.

 And the neighbours came in, and asked her, “What is the matter,woman? What is there?” And she answered my husband is dead.

Her husbad’s friend told them “Come out so that I can heal him because I know the cure.”The two remained in the house, and began to ask their partner,“What did you see now?” His friend told him what he saw, “When my wife saw me dead she said, I am hungry I will start crying after eating.” She started cooking, but the was no vegetables there. Honey was on the roof on top of the bed near it.When she wanted to take the honey, she did not reach it, and she walked on my stomach.”

They started laughing now, when the people heard the laughter they realized that our colleague was healed. And he said to his wife, “That your love is very little.” The woman remembered what she had done and was sorry.

 

 

68. Nkima Uyo Waladantogagwa (Antogilwe) Ngoshi

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Ng’waka gumo waliho ngosha na nke wakwe na bhana. Huna iza nzala nhale gete, bhusumilo wali kule. Nkima ung’wila ngoshi, “Jaga ugadukobhele ishiliwa.”

Huna ungosha uja lugendo, lwa kushimiza ji akagwisha. Intondo akifula, ntondo bhungi ushoka wenha shiliwa bhulya.
Lushiku lumo kwike kuhaya akakima, “Jashilaga ishiliwa ng’wana Kweji, shokaga hangi ukubhusumilo.” Aluwe alisiminza na nzala kwike mlugendo. Ulu washoka hakaya kang’wila, “Wenhaga shigehu.” Ntondo shokelaga, nose ungosha ucha. Ubhulagwa nzala na lugendo.

Kiswahili: Mwanamke Ambaye Alikuwa Hampendi (Anampenda) Mme Wake.

Mwaka mmoja alikuwepo mwanamume na mke wake na watoto wao. Basi ilitokea njaa kubwa kabisa, chakula kilipatikana mbali. Mwanamke akamwambia mme wake, “Nenda ukatutafutie chakula.”

Basi mme wake akaanza safari ya kutembea, jua likachwea. Kesho yake akapumzika.  Siku iliyofuata  alirudi akaleta chakula wakala. Siku moja tena  mke wake alisema, “Chakula kimekwisha mwana Kweji rudia tena.

Lakini mwanamume alikuwa anatembea na njaa tu safarini. Akirudi nyumbani anaambiwa umeleta kidogo, kesho rudia tena. Mwishowe mwanamume akafa kwa ajili ya njaa na safari.

african-family-

african

ENGLISH: A WOMAN WHO DID NOT LOVE HER HUSBAND

Once upon a time, there was a man and his wife and their children. Then there came a great famine. Food could befound  very far away. The woman said to her husband, “Go and get us food.”

So her husband began to walk. He walked until the sun went down. The following day, he rested. Then he went back home and brought food.They ate it. Another day, his wife said, “The food has been finished, Ng’wana Kweji, go an dbring some more.”

But the man was walking while hungry all the way. Whenever he came home, he was told he had brought little. So, he had to go back and bring some more the following day. Finally, the man died of hunger and travel fatigue.

67. Nashosha Ichimu Kuli Ngabhuji

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Kale bhanhu bhagabhulilagwa nyama na bhanamhala, kiti habhukombe na habhuyobhe na ha lufu na mumalibhilingo.

Kali kajile, uluwagabhulilagwa nyama na namhala (ngabhuji) kushosha nkono kuli ngabhuji. Kwene kuhaya kung’winha ngabhuji ipande lya nyama iyo winhwa. Ili nzila ya kufunya bhulumbi kuli ngabhuji, lumeng’ho lwa giki alinabhulumbi kuli ngabhuji.

Aliyo ulubhatagabhulililwe nyama abhajimbagwa na bhangi bhagabhulilagwa, bhabyaji bhasayaga kibhi no. Gwali mhayo gwa wisu huna lulu, bhubhatuma bhana bhado bhayanda kujung’wisha sumu ngabhuji.

Bhagabhuji bhagwashiwagwa bhingi no, na bhayanda bhakamalwa na bhujimbani wabho kulogwa. Kulishiwa sumu no, ishangilingili (kando kando) hihi hihi mung’hilimbwa na nyanza na Magu, na Nasa, na Masanza, niyo likaluma lya bhudumi.

Ubhebhe wangabhulila nyama ung’wana wakushokejaga bhulogo nulu ichimu. Mu ng’wanya gwa kushosha nkono, kufunya bhulumbi bhashoshaga ichimu bhubhamala abhagabhuji bhingi no umugubhalisha sumu, ichene mapande gakumanyanza bhatalyaga kungi kulwa widumi. Hangi ha walwa ulu ng’wenikili walwa atatogilwe kung’wa bhangi bhatuzunya iki bhogoha kulishiwa.

Kiswahili: Kurudisha Mkono Kwa Mgawaji

Hapo kale walikuwa wanagawiwa nyama na wazee kwa mfano, kwenye harusi, kwenye mkusanyiko wa kazi, kwenye kilio na kwenye mikutano mbali mbali.

Zamani ilikuwa kawaida yao kugawiwa nyama na wazee (mgawaji) kurudisha mkono kwa mgawaji ndiyo kusema kumpa mgawaji kipande cha nyama. Ambayo umepewa, ilikuwa njia mojawapo ya kutoa shukrani kwa mgawaji. Ni alama ya kujulisha kuwa ana furaha kwa mgawaji.

Kama hawatagawiwa nyama, wengine hawatazipata na wengine watapata kidogo. Wazazi walikuwa wanaudhika mno, lilikuwa neno la wivu. Kwa hiyo waliwatuma vijana wa kiume kuwanywesha sumu wagawaji.

Wagawaji walikuwa wananaswa wengi mno na vijana.  Walimalizwa wachoyo kwa kulogwa (kwa wanaoamini hivyo) na kulishwa sumu. Sana sana waliokuwa kando kando ya Ziwa kwa mfano, Bulima, Kwimba, Mwanza, Magu, Nassa na Masanza.

 Ndiyo kusema kuwa kulivuma hali ya kutokuwa na uwezo. Wewe uliyegawiwa nyama yeye amekurudishia sumu, au mkuki  kwenye kazi ya kurudisha mkono yaani kutoa shukrani, walikuwa wanarudisha mkuki, waliwamaliza wagawaji wengi mno kwa kuwalisha sumu.

Ndiyo maana pande za Nyaza (Ziwani) hawali kwingine kwa shida ya kukosana. Na tena kwenye pombe kama mwenye pombe hapendelei kunywa, wengine hawatakubali kwa vile wameogopa kulishwa sumu.

lance man with spear

ENGLISH: TO RETURN A HAND TO THE DISTRIBUTOR

In the past, meat was distributed by the elders. For example, during weddings, gatherings, funerals and in various meetings.

In the past, it was common for the recipients to share the meat they had been given with the distributor as a way of saying thank you.That means,the recipient had to give the distibutor a piece of meat. It was a sign that the recipient was happy with the distributor.

The practice was deemed good because if they didnot distribute the meat, some would not get it and others would get less. Some parents were very angry with the practice. It was a matter of jealousy. So, they conspired with the young men to poison the distributors.

Many distributors were trapped by young people. They were fed poison but they thought that they had beenbewitched (for those whobelieved in witchcraft). It was common in the Lake Zone. For example, it was observed in Bulima, Kwimba, Mwanza, Magu, Nassa and Masanza.

What was obvious is that there came a state of misunderstanding and mistrust. Imagine! Somebody gives you meat and return poison as thanks. In other words,you come with a spear in your hand to give back thanks. In this way of thanks giving, they poisoned so many distributors.

That is why the Nyaza (Lake Victoria) sides, people do not eat in other people’s homes because of being afraid to be poisoned through food. In the same is true for alcohol. If the owner does not drink, some will not accept their alcohol because they are afraid of being poisoned.