Mwanza

1329. LUPA LUDI NANG’WINIKILI.

Ulupa lililintego ili ligategagwa aho igelelilwe gubhita ho ndimu nulu noni nhale. Ulupa lunulo lugapujaga ndimu iyo yupitila hoyi nulu nu munhu uyo ulutegaga ulu ubhitila hoyi lumpuja duhu kunguno ludakominije uo gupuja. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “lupa ludi nang’winikili.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhejaga jilagilo ijo jigampujaga nuweyi ng’winikili, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhejaga jilagilo jagulemeja bhanhu gwita ginhu jilebhe nulu ja gubhalemeja guja hanhu, ogisanga jilintunga nuweyi ng’winikili, kungulo ya gugaiwa witegeleja bho jujikalana chiza, umuwikaji bhokwe. Uweyi agitungaga ng’winikili ulu ojibhinza ijilagilo jinijo ijo ojibheja ng’winikili, kunguno ya gugaiwa wigetegeleja bhunubho ubho gujikalana chiza, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agatega lupa wisanga lulimpuja nuweyi ng’winikili, kunguno nuweyi agabhejaga jilagilo ogisanja jilintunga nuweyi ng’winikili, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “lupa ludi na ng’winikili.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gugikalana chiza amalagilo ayo bhagagabhejaga kugiki bhadule gwikala ni lange lya gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Isaya 1:17.

Mithali 4:2.

Yakobo 2:9.

KISWAHILI: MTEGO HAUNA MWENYEWE.

Mtego ni kitu kinachotegwa pale ambapo wanyama poli au ndege wakubwa hupita. Mtego huo, hukamata mnyama yoyote yule apitiaye hapo au hata mtu aliyeutega mtego huo akipitia hapo unamkamata tu kwa sababu haubagui wa kukamata. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtego hauna mwenyewe.”

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutunga amri au sheria ambazo humfunga yeye mwenyewe, katika maisha yake. Mtu huyo, gutunga sheria au amri za kuwakataza watu kwenda sehemu fulani, au za kuwakataza kufanya kitu fulani ambazo hujikuta zimemkamata yeye mwenyewe kwa sababu ya kukosa umakini wa kuziishi vizuri, maishani mwake. Yeye hujifunga mwenyewe kila anapozivunja amri hizo alizozitunga mwenyewe, kwa sababu ya kukosa umakini huo wa kuziishi, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyetega mtego akajikuta umemkamata yeye mwenyewe, kwa sababu naye hutunga amri au sheria ambazo hujikuta zimemfunga yeye mwenyewe, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtego hauna mwenyewe.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuyaishi maagizo yale wanayojitungia ili waweze kuishi kwenye malezi ya kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Isaya 1:17.

Mithali 4:2.

Yakobo 2:9.

gray-crowned-crane-5896928_1280

buffalo-840340_1280

dikdik-4281516_1280

ENGLISH: THE TRAP HAS NO OWNER.

A trap is something that is set where large animals or birds pass by. This trap catches any animal that passes by or even the person who set the trap when he/she passes by, it catches them only because it does not tell apart between the ones it catches. That is why people say that, “the trap has no owner.”

This proverb is equated to a person who makes orders or laws that bind him, in his life. Such person makes laws or orders to prohibit people from going to a certain place, or to prohibit them from doing something that he finds himself bound by because of his lack of thoughtfulness for putting them into practice well, in his life. He binds himself every time he breaks those orders that he made himself, because of his lack of responsiveness, in his life.

This person is like the one who set a trap and found himself bound by it, because he also makes orders or laws that he finds himself bound by in his life. That is why people say that, “the trap has no owner.”

This proverb imparts in people an idea of being so cautious enough to live by the instructions they create for themselves so that they can live in a way that will nicely nurture their families throughout their lives.

Isaiah 1:17.

Proverbs 4:2.

James 2:9.

1328. NANG’WIKIJA NKIMA NDOB’O KUNTWE.

Olihoyi munhu umuchalo ja Ng’watugu uyo agang’wikija nkima ndob’o kuntwe. Unkima ng’wunuyo oliabhuchije ndob’o iyo yalina minzi ayo oliogadahila kumongo go Mangu kunguno galinduhu aminzi umuchalo jabho jinijo.

Umunhu ng’wunuyo aho otung’wana nanghwe agang’wimbilija bho gung’wikija indob’o yiniyo gwingila kuntwe gokwe kunguno ya aganchila jigongo. Hunagwene agayomba giki, “nang’wikija nkima ndob’o kuntwe.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinisungu lya gubhambilija bhakima abho bhali na makoye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhambilija abhamayu abho bhali nikoye lya kugayiwa minzi bho gubhasimbila lyunzi lo minzi umuchalo jabho kugiki bhadule gulimala ilikoyi lya gubhunwa ndob’o ja minzi kumitwe yabho linilo gwingila kumongo, kunguno ya lisungu lyakwe linilo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhambilija bhamayu bhingi abho bhali na makoye kunguno ya lisungu lya nholo yakwe linilo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agang’wambilija nkima uyo oliabhuchije ndob’o ya minzi, guyicha indob’o yiniyo, gwingila kuntwe gokwe, kunguno nuweyi agabhambilija bhakima bhingi abho bhali na makoye ga gugayiwa minzi bho gubhasimbila lyinzi umuchalo jabho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “nang’wikija nkima ndob’o kuntwe.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza nisungu lya gubhambilija abhakima abho bhali na makoye kugiki bhadule gugamala wangu amakoye genabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 11:28-30.

Wafilipi 2:4.

Zaburi 72:12-14.

Zaburi 103:13.

NIMEMTUA MWANAMKE NDOO KICHWANI.

Alikuwepo mtu katika kijiji cha Mwatuju aliyemtua mwanamke ndoo kichwani. Mwanamke huyo alikuwa amebeba ndoo ya maji kichwani aliyoyachotea kwenye mto wa Mangu, kwa sababu hayakuwepo maji katika kijiji chake hicho.

Mtu huyo alikutana naye njiani akamsaidia kuitua ndoo hiyo kutoka kichwani kwa sababu alimuonea huruma. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimemtua mwanamke ndoo kichwani.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana huruma ya kuwasaidia wanawake wanakumbwa na matatizo mbalimbali, katika maisha yake. Mtu huyo, huwasaidia wakina mama katika kutatua tatizo la kukosa maji kwa kuwachimbia kisima cha maji kijijini mwao, kwa sababu ya huruma yake hiyo, maishani mwake. Yeye huwasaidia wakina mama wengi wenye matatizo mbalimbali katika kuyatatua matatizo yao, kwa sababu ya huruma yake hiyo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mtu aliyemuonea huruma mwanamke aliyekuwa amebeba ndoo ya maji kichwani mpaga akamsaidia kuitua ndoo hiyo kichwani, kwa sababu naye huwasaidia wanawake wengi wenye matatizo ya kukosa maji kwa kuwachimbika kisima cha maji kijijini mwao, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimemtua mwanamke ndoo kichwani.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na huruma ya kuwasaidia wanawake wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali ili waweze kuyatatua haraka, maishani mwao.

Mathayo 11:28-30.

Wafilipi 2:4.

Zaburi 72:12-14.

Zaburi 103:13.

outdoors-3378794_1280

ethiopia-4117617_1280

people-6556791_1280

ENGLISH: I HAVE DROPPED A BUCKET FROM A WOMAN’S HEAD.

There was a man who lived in the village of Mwatuju who met a woman carrying a bucket on her head. The woman was carrying a bucket of water on her head that she had drawn from Mangu River, because there was no water in her village.

This man met her on the way and helped her put the bucket off her head because he felt sorry for her. That is why he said, “I have dropped a bucket from a woman’s head.”

This saying is matched to a man who has compassion for helping women who face various problems in their lives. Such person helps mothers in solving problem of lack of water by digging a well for them in their village, because of his compassion for them in his life. He helps various mothers who had several problems in solving their hitches, because of his compassion, in his life.

This man resembles the one who felt sad for a woman carrying a bucket of water on her head and helped her put it down from her head, because he also helps a lot of women who face water problems by digging a well for them in their village. That is why he says that, “I have dropped a bucket from a woman’s head.”

This saying teaches people about having compassion for helping women who suffer from various difficulty so that they can solve them quickly, in their lives.

Matthew 11:28-30.

Philippians 2:4.

Psalm 72:12-14.

Psalm 103:13.

1327. NAGULEKA MUMANGAILA.

Aho kale olihoyi munhu uyo ohayaga na bhiye bho gutumila mihayo ya mbisila iyo bhadumaga abhiye bhenabho uguyelelwa chiza kunguno ya gubhisa ginhu jilebhe ukubhoyi. Umunhu ng’wunuyo, obhalekaga abhiye bhadadebhile ubhulingisilo bho mihayo iyo abhalomelaga yiniyo, kunguno ya gutumila mihayo ya mbisila yiniyo, umuwikaji bhokwe bhonubho. Hunagwene agayomba giki, “aguleka mumangaila.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wimi nholo umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhabhisaga abhiye ijikolo jakwe bho gutumila bhushirimu kugiki akije ugubhinha abho bhalinomba kunguno ya wiminholo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agagayiyagwa ulubhango ulo gwikala na bhuyeji aha kaya yakwe kunguno ya wiminholo bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agabhabhisa abhiye kinhu jilebhe bho guyomba mihayo ya mbisila mpaga bhuduma uguyelelwa chiza imihayo yakwe yiniyo, kunguno nuweyi agabhimaga abhiye ijikolo jakwe bho gutumila bhushirimu bho gung’wambilija gukija ugubhinha abhiye abho bhalinomba, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “naguleka mumangaila.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka wiminholo bho gubhambilija chiza abhichabho abho bhali na makoye, kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala na bhuyeji umu kaya jabho.

Mathayo 13:24-30.

Mathayo 25: 36-43.

Zaburi 119:130.

KISWAHILI: NIMEKUACHA BILA UFAFANUZI.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyeongea na wenzake kwa kutumia maneno ya mafumbo. Maneno hayo yalisababisha kwa wenzake hao kushindwa kuuelewa vizuri ujumbe wake kwa sababu alikuwa na lengo la kuwaficha kitu fulani wenzake hao. Mtu huyo aliwaacha wenzake hao katika hali ya kukosa ufafanuzi wa maneno yake hayo yenye mafumbo. Ndiyo maana yeye alisema kwamba, “nimekuacha bila ufafanuzi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mchoyo wa kutowashirikisha wenzake mali zake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwaficha wenzake mali zake hizo kwa kutumia ujanja wa kumwezesha kuacha kuwapatia wenzake hao wanaomuomba mali zake hizo, kwa sababu ya uchoyo wake huo, maishani mwake. Yeye hukosa Baraka za kumwezesha kuishi kwa furaha katika familia yake, kwa sababu ya uchoyo wake huo wa kutowashirikisha wenzake mali zake hizo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewaficha wenzake kitu fulani kwa kutumia maneno yenye mafumbo mpaga akawacha bila ufafanuzi, kwa sababu naye huwanyima wenzake mali zake kwa kutumia ujanja wa kumwezesha kutowapa mali zake hizo, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimekuacha bila ufafanuzi.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha uchoyo kwa kuwasaidia wenzao walioko kwenye matatizo ili waweze kupata Baraka za kuishi kwa furaha katika familia zao.

Mathayo 13:24-30.

Mathayo 25: 36-43.

Zaburi 119:130.

ENGLISH: I HAVE LEFT YOU WITHOUT EXPLANATION.

Once upon a time, there was a man who spoke to his companions by using cryptic words. These words prevented his companions from understanding his message properly because he intended to hide something from them. Such man left his acquaintances in a state of lacking explanation for his cryptic words. That is why he said, “I have left you without explanation.”

This saying is equaled to a person who is greedy in not sharing his possessions with his companions, in his life. Such person hides his possessions from his companions by using cunning deeds which can enable him to stop giving his companions who ask for his possessions, because of his greed in his life. He lacks blessings that can enable him to live happily in his family, because of his greed of not sharing his possessions with his companions in life.

This person is like someone who hid something from his friends by using cryptic words which left them without explanation, because he also deprives his friends of his possessions by using cunning deeds which enables him not to give them his possessions in his life. That is why he says, “I have left you without explanation.”

This saying imparts in people a clue of giving up greed by helping their friends who are in trouble so that they can receive blessings of living happily in their families.

Matthew 13:24-30.

Matthew 25: 36-43.

Psalm 119:130.

portrait-3157821_1280

girl-429380_1280

man-792821_1280

1326. IZUGA LYA MANYANYA NULU HALIMI DUHU JUPYA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile bhuzugi bho manyanya. A manyanya genayo gadi nizuga lidamu kunguno unzugi ogo adulile nulu gugachembagula duhu ugaleka mulimi gupya. Umunhu ng’wunuyo, agagutumamaga unimo gunuyo bho nduhu nulu gunoga. Hunagwene agayombaga giki “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adebhile gutumama milimo yakwe chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga na milimo mingi iyo aidebhile uguitumama mpaga oyimala chiza kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi noyi aha kaya yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho gudebha guitumama mingi chiza chiniko, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo oliadebhile guzuga nyanya chiza, kunguno nuweyi adebhile gutumama milimo yakwe chiza chiniko, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “izuga lya manyanya nulu halimi duhu jupya.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gudebha kutumama milimo yabho chiza chiniko, kugiki bhadule gupandika matwajo  mingi, umuwikaji bhobho.

Ezra 5:8.

KISWAHILI: UPISHI WA NYANYA HATA JUANI TU ZINAIVA.

Chanzo cha msemo huo huangalia upishi wa nyanya. Nyanya hizo hazina mapishi magumu kwa sababu mpikaji wake aweza hata kuzikatakata tu akaziacha juani zikaiva. Mtu huyo huifanya kazi hiyo bila hata ya kumchosha. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anaelewa kufanya kazi zake vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo hufanya kazi nyingi anazizoelewa kuzitekeleza mpaga anazimaliza vizuri, kwa sababu ya  umakini wake huo, maishani mwake. Yeye hupata mali nyingi sana kwenye familia yake kwa sababu ya umakini wake huo wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zake hizo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeelewa kupika nyanya vizuri, kwa sababu naye anaelewa kuzitekeleza kazi zake vizuri, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “upishi wa nyanya hata juani tu zinaiva.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzielewa na kuzitekeleza vizuri kazi zao zote, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Ezra 5:8.

 

ENGLISH: COOKING TOMATOES EVEN IN THE SUN WILL RIPEN.

The origin of this saying looks at cooking tomatoes. These tomatoes do not have difficult recipes because their cook can even just chop them and leave them in the sun to ripen. This person does this work without even being tired. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying is matched to a man who understands how to do his work well, in his life. Such person does several tasks that he understands how to do, and he finishes them well, because of his responsiveness, in his life. He earns a lot of wealth in his family because of his thoughtfulness of understanding and carrying out his tasks well, in his life.

This person resembles the one who understood how to cook tomatoes well, because he also understands how to carry out his tasks well, in his life. That is why he says, “Cooking tomatoes even in the sun will ripen.”

This saying teaches people to be careful enough to understand and carry out all their tasks well, so that they can achieve great success in their lives.

Ezra 5:8.

 

 

woman-5935805__480

1325. UMUNHU UYO ADIMANILE ING’HANA UDIZUNG’WILA ING’HANA.

Akahayile kenako kandija kuli munhu uyo oyombaga mihayo ya bhulomolomo umukikalile kakwe. Abhanhu abho wikalaga nabho umunhu ng’wunuyo, bhang’wilaga giki  aileke imihayo yiniyo iyabhulongo bho guyomba bhunhana, olema kunguno ya bhuhalali bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “umunhu uyo adimanile ing’hana udizung’wila ing’hana.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitaga mihayo ya bhubhi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alinsembo uyo adigwaga  mihayo ya guwilwa na bhiye kunguno ya nhungwa jakwe ija bhuhalali jinijo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguilela chiza ikaya yakwe kunguno ya bhusembo bhokwe ubho gwita mihayo ya bhubhi bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo owilagwa giki aleke guyomba mihayo ya bhulomolomo olema, kunguno nuweyi agawilagwa na bhiye giki, aleke gwita mihayo ya bhubhi, olema, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu abho agabhahalalikaga bhagiwilaga giki, “umunhu uyo adimanile ing’hana udizung’wila ing’hana.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja gwita mihayo ya bhubhi bho gwita mihayo ya wiza kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

2Wakonritho 7:14.

Yohane 14:17.

KISWAHILI: MTU ASIYEUJUA UKWELI USIMWAMBIE UKWELI.

Msemo huo, ulianzia kwa mtu yule aliyekuwa alisema maneno ya uongo katika maisha yake. Watu waliokuwa wakiishi naye, walimwambia kwamba aache kusema uongo kwa kusema ukweli, akakataa kwa sababu ya ubishi wake huo. Ndiyo maana watu hao, walisema kwamba, “mtu asiyeujua ukweli usimwambie ukweli.”                                 

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutenda maovu katika maisha yake. Mtu huyo hutenda maovu kwa wenzake na kukataa kuyaacha pale wenzake hao wanapomshauri kuayaacha, kwa sababu ya tabia yake hiyo mbaya ya ubishi, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake hiyo kwa sagabu ya kutenda maovu hayo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekataa kuacha kusema uongo aliposhauriwa na wenzake, kwa sababu naye hukataa kuacha kutenda maovu anaposhauriwa na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana wenzake hao, huambiana kwamba, “mtu asiyeujua ukweli usimwambie ukweli.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kutenda maovu kwa kufuata ushauri wa kutenda mema kwa wenzao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

2Wakonritho 7:14.

Yohane 14:17.

ENGLISH: DO NOT TELL THE TRUTH TO A PERSON WHO DOES NOT KNOW IT.

This saying is originated from a person who had told lies in his life. The people who lived with him told him to stop lying by telling the truth, but he refused because of his argumentativeness. That is why those people said, “Do not tell the truth to a person who does not know it.”

This saying is equated to a person who commits evil deeds in his life. Such person commits evil deeds against his nobles and refuses to stop when those nobles advise him to stop, because of his wicked argumentative behavior in his life. He fails to nurture his family well because of committing those evil deeds in his life.

This person is similar to the one who refused to stop lying when advised by his fellows, because he also refuses to stop committing evil deeds when advised by his fellows in his life. That is why those fellows say to each other, “Do not tell the truth to a person who does not know it.”

This saying imparts in people an idea of stopping habits of doing evil deeds by following advice of doing good deeds to their fellows, so that they can nurture their families well, in their lives.

2 Corinthians 7:14.

John 14:17.