Folklore

942. NENE NG’WENUYU NALYA WIYAB’I.

Olihoyi munhu uyo wigalulaga bho gutumila wiyab’i bhutale. Nzenganwa okwe agamuja, “nibhuli ugusiminzaga ugambalile chiniko?” Uweyi agashosha, “nagutumilaga wiyabhi bhone.” Unzenganwa okwe agashosha, “ulu ubhutumila shib’i uwiyabhi bhoko bhunubho ugupandika makoye, umukikalile kako.” Uweyi agashosha, “nene ng’wenuyu nalya wiyab’i.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhutumilaga shib’i uwiyab’i bhokwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyagalulaga bho gubhaluhya abhiye kunguno ya libhengwe lyakwe ubhuyi. Uweyi agidumaga na bhiye kunguno ya wiyagaluji bhokwe bhunubho, ubho bhugenhaga makoye ukubhanhu bhakwe, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo olyaga wiyabhi bho gusiminza agimbalile, umukikalile kakwe, kunguno nu weyi agiyagalulaga mpaga obhenhela makoye obhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “nene ng’wenuyu nalya wiyab’i.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza ni kujo lya gubhutumia chiza uwiyab’i bhobho, kugiki bhadule gwikala bho mholele na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 3:1-16.

Yohana 8:31-36.

KISWAHILI: MIMI HUYU NIMEKULA UHURU.

Alikuwepo mtu mmoja aliyeishi kwa kutumia uhuru mkubwa. Jirani yake alimuuliza, “kwa nini unatembea kwa kujipanga hivyo?” Yeye alijibu, “nautumia uhuru wangu.” Jirani yake akajibu, “ukiutumia vibaya uhuru wako utapata matatizo katika maisha yako.” Yeye alijibu, “mimi huyu nimekula uhuru.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huutumia vibaya uhuru wake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufurahia kwa kuwatesa wenzake kwa sababu ya dharau yake kwao. Yeye hukosana na wenzake kwa sababu ya kuutumia vibaya huo uhuru wake, unaoleta matatizo kwa watu wake hao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekula uhuru wake kwa kutembea kwa majigambo, katika maisha yake, kwa sababu naye huutumia vibaya uhuru wake mpaka unaleta matatizo kwa wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “mimi huyu nimekula uhuru.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na busara ya kuutumia vizuri uhuru wao, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Mwanzo 3:1-16.

Yohana 8:31-36.

african-woman1

underground-

 

boy-1

 

ENGLISH: I HAVE EATEN FREEDOM.

There was one man who lived by enjoying great freedom. His neighbor asked him, “Why are you walking all the way?” He replied, “I exercise my freedom.” His neighbor replied, “If you abuse your freedom you will have problems in your life.” He replied, “I have eaten freedom.”

This saying is compared to a person who abuses his freedom, in his life. This man, however, rejoices in torturing his fellow men because of his contempt for them. He quarrels with his colleagues because he abuses his freedom, which causes him problems to his people, in his life.

This person is like the one who ate his freedom by walking proudly, in his life, because he also abuses his freedom by causing problems to his fellows, in his life. That is why he says that, “I have eaten freedom.”

This saying teaches people on how to be wise enough to make the best use of their freedom, so that they can live in peace with each other, in their lives.

Genesis 3: 1-16.

John 8: 31-36.

940. KALAGU – KIZE. NG’WISHIGU ALIYO ADIOGUSEJIWA – LIJIGANGA.

Ikalagu yiniyo ihoyelile lijipanga. Ilijiganga liniyo, lili liwe litale ilo lidasegejiyagwa na mhunhu oseose kunguno lyasumva chene. Ilyoyi lili lidito ilo lidilyagushingisha nulu hado nu nshindiki olyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “ng’wishigu aliyo adiogusegejiwa – lijiganga.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agadimilaga nhungwa ja wiza bho nduhu ugutinginyiwa na munhu ose ose, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alemile ugugaleka amiito gakwe agawiza mumo bhagang’witila abhanishi bhakwe, kunguno agapandikaga mbango ja gufumila kuli Mulungu uyo ang’wisanije, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’winuyo, agikolaga ni liwe ilo lidasegejiyagwa na oseose, kunguno nuweyi alemile uguyileka imihayo iya nhana, umukikalile kakwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhakwe guyidimila imihayo ya ng’wa Mulungu bho kikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ng’wishigu aliyo adiogusegejiwa – lijiganga.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gudimilaga chiza inhungwa ja wiza bho gunzunya na gung’wisanya Mulungu shigu jose, kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala chiza na bhichabho, umuwikaji bhokwe.

Waefeso 6:10 – 17.

Wagalatia 5:1.

Tito 2:1-2.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

YU IMARA LAKINI HASOGEZWI – MWAMBA.

Kitendawi hicho huongelea Mwamba. Mwamba huyo, ni jiwe kubwa ambalo halisogezwi na mtu kwa sababu limeumbwa hivyo. Lenyewe ni zito lisilo tigiswa hata kidogo na msukumaji wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “yu imara lakini hasogezwi – mwamba.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huishikiria tabia njema bila kutikishwa na mtu, katika maisha yake. Mtu huyo, hataki kuyacha matendo yake mema hata maadui zake wamtigise kiasi gani, kwa sababu hupata Baraka kutoka kwa Mungu amwaminiye ambazo humsaidia kuyashikiria mema hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na lile jiwe lisilosogezwa na yeyote, kwa sababu naye hataki kuiacha tabia yake hiyo njema yimwezeshayo kuishi maisha mema, maishani mwake. Yeye huwafundisha watu wake namna ya kuyaishi maneno ya Mungu kwa njia a maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “yu imara lakini hasogezwi – mwamba.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuyaishi maadili mema kwa kumwamini Mungu siku zote, ili waweze kupata Baraka za kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao.

Waefeso 6:10 – 17.

Wagalatia 5:1.

Tito 2:1-2.

 

stone-11

stone-12

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

HE IS STRONG BUT NOT MOVED – A ROCK.

This riddle speaks of the Rock. This rock is a huge stone that cannot be moved by any one because it was created in that way. It is heavy to the point of not being moved by its pushers. That is why people say that, “He is strong but not moved – a rock.”

This riddle is compared to a person who adheres to good manners without being shaken by anyone in life. Such person does not want to give up his/her good works no matter how much his/her enemies may scare him/her, because he/she receives blessings from a God who helps him/her enough to hold on to live that good life.

This person is like a stone that no one can move, because he also does not want to give up his good character that enables him to live a good life with others. He teaches his people on how to live the word of God through his life. That is why people say to him that, “He is strong but not moved – a rock.”

This riddle imparts in people an idea on how to live morally by trusting in God at all times, so that they may receive blessings of living well with one another in their lives.

Ephesians 6:10 – 17.

Galatians 5: 1.

Titus 2: 1-2.

coast-rock

762. JANDUGUYO JANUKULAGE NA BHUYEGI: ULIHAYA JIGABU WALIMA NANGHWE?

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile kuli munhu uyo aginhiwa jikolo na ng’wiye uyo olinduguye. Aho winhiwa ijikolo jinijo, agakija ugulumba kunguno uliojidalahija. Uweyi wigongejaga gwinhiwa jikolo ijo jidulile gokala mujigabu guti giki bhajilima nanghwe umunhu ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “janduguyo janukulage na bhuyegi: ulihaya jigabu walima nanghwe?”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina bhulumbi ukubhiye abho bhagangunanaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhadalahijaga abhiye abho bhagangunanaga bho gujibyedeleja ijikolo ijo bhagang’winhaga. Uweyi agajibhonaga jidololo bhuli jene ijo bhaling’winha abhiye, kunguno agigongejaga winhiwe jikolo jitale gukila ijo bhang’winhaga jinijo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo aginhiwa jikolo na nduguye, ujidalahija, bho gwigongeja winhiwe ijo jokalile mujigabu, kunguno nuweyi adalumbaga ulu bhang’wambilija abhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene bhagang’wilaga giki, “janduguyo janukulage na bhuyegi: ulihaya jigabu walima nanghwe?”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhulumbilija ulu bhinhiwagwa jikolo nulu jigabhiza jigehu na ginehe, kugiki bhadule gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho. Idichiza ugujidalahija ijikolo ija gwinhiwa na bhichabho.

Bhaebrania 12:28.

KISWAHILI: CHA NDUGUYO KIPOKEE KWA FURAHA (KATIKA TUNGA):  WATAKA KAPU ULILIMA NAYE?

Chanzo cha methali hiyo, kilianzia kwa mtu aliyepewa kitu na ndugu yake. Alipopewa kitu kicho hakushukuru kwa sababu alikidharau, kuwa ni kidogo. Alitaka apewe kitu kikubwa cha kuweza kujaa kwenye kapu kana kwamba, walilima naye ndugu yake huyo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “cha nduguyo kipokee kwa furaha (katika tunga): wataka kapu ulilima naye?”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hana shukrani kwa wenzake wanaomsaidia, katika maisha yake. Mtu huyo, hukidharau kitu anachosaidiwa kwa kupewa na wenzake. Yeye huviona kuwa ni kidogo kila kitu anachopewa na wenzake, kwa sababu ya kutaka apewe kikubwa zaidi kupita kile alichopewa.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyepewa kitu na ndugu yake, akakidharau, kwa kutaka apewe kikubwa cha kujaa kapu, kwa sababu naye hashukuru anapopewa vitu na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “cha nduguyo kipokee kwa furaha (katika tunga): wataka kapu ulilima naye?”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo wa shukrani kwa wale wanaowasaidia kwa kuwapatia vitu mbalimbali, hata kama vikiwa vidogo kiasi gani, ili waweze kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao. Siyo vizuri kukidharau kitu cha kupewa na wenzao.

Waebrania 12:28.

farmer2

farmer african-girl

african-women-walking-along-road

ENGLISH: BE  CONTENT  TO  RECEIVE  WHATEVER  THE  AMOUNT  OF  SOMETHING  YOU  ARE  GIVEN.  THIS IS BECAUSE  YOU  DID NOT WORK   FOR  IT (RECEIVE THOSE OF YOUR RELATIVES WITH JOY: YOU WANT THE BASKET DID YOU CULTIVATE WITH THEM?)

The overhead proverb originated from a man who was given a gift by his brother. He was was not grateful because he despised such gift by considering it as a small thing. He wanted to be given a big one enough to fill the basket as if he cultivated together with his brother. That is why people said to him that, “be  content  to  receive  whatever  the  amount  of  something  you  are  given.  This is because  you  did not work   for  it.”

The proverb is likened to a man who has no appreciation to his fellow human beings who help him, in his life. Such person, in turn, despises the gifts that are given to him by his peers. He considers them as small things, because he wants to be given more than what he received.

This person resembles the one who despised what his brother gave to him, by remanding something bigger than that, because he also did not appreciate the gifts which were given to him by his fellows. That is why people tell him, “be  content  to  receive  whatever  the  amount  of  something  you  are  given.  This is because you did not work   for  it.”

This proverb instills in people an idea on how to be grateful to those who help them in various ways, no matter how small their helps can be, so that they can live well with each other, in their lives. It is not good to look down on others.

Hebrews 12:28.

 

761. UNINDI O SHILI HUNI O SHILI.

Imbuki ya lusumo lunulo, ingilile kuli munhu uyo olindaga shili mungunda. Unindi ng’wunuyo ojilindaga ishili jinijo bhuli lushigu, aliyo lulu, ishili jinijo jamanaga jushila duhu.
Nose bhuyibhuja giki, ‘nibhuli jigumanaga juliwa ishili jiniji?” Umo obho uyomba, “ditagi bhukengeji kugiki dudule gudebha chiza.” Aho bhakengela chiza bhubhona giki, gashinaga umunhu uyo olijindaga ishili jinijo, huyo ojilyaga. Hunagwene bhagayomba giki, “unindi o Shili huni o shili.”
Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajikenagulaga sagala ijikolo jakwe bho weyi ng’winikili, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajimalaga isabho jakwe bho gujitumamila sagala na gujilekanija. Uweyi agajimalaga isabho jinijo aliyo unindi ojo nu weyi ng’winikili.
Umunhu ng’wunuyo, agikilolaga nu nindi o shili uyo ojikamala ishili ijo ojilindaga, kunguno nu weyi agajikenagulaga sagala isabho jakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “unindi o shili huni o shili.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kudebha gujilanghana chiza isabho jabho bho guleka gujikenagula sagala, umukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.
Yohana 18:2-5.

KISWAHILI: MLINZI WA KUNDE NDIYE MLAJI WA KUNDE.

Chanzo cha methali hiyo kilitokea kwa mtu aliyekuwa akilinda kunde shambani. Mlinzi huyo wa kunde alikuwa akilinda kila siku, lakini kunde hizo zilikuwa zikiendelea kuisha tu.
Mwishowe walijiuliza kwamba, “kwa nini kunde hizi zinaendelea kuisha?” Mmoja wao alisema, “tufanye utafiti vizuri ili tuweze kufahamu.” Walipofanya utafiki huo, waligundua kwamba, kumbe mtu aliyekuwa akizilinda kunde hizo ndiye aliyekuwa akizila. Ndiyo maana walisema kwamba, “mlinzi wa kunde ndiye mlaji wa kunde.”
Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huiharibu mali yake mwenyewe kwa kuitumia vibaya, katika maisha yake. Mtu huyo, huzimaliza mali zake mwenyewe kwa kuzitumia hovyo. Yeye badala ya kuzitunza mali hizo huziharibu kwa kuzitelekeza na kupangia matumizi mabaya.
Mtu huyo, hufanana na mlinzi wa kunde aliyekuwa akizimaliza kunde hizo kwa kuzila mwenyewe, kwa sababu naye huiharibu mwenyewe mali yake hiyo kwa kuitumia vibaya. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mlinzi wa kunde ndiye mlaji wa kunde.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuelewa namna ya kuzitunza vizuri mali zao, kwa kuacha kuzitumia kwenye matumizi ya hovyo, ili waweze kupata maendeleo mengi zaidi maishani mwao.
Yohana 18:2-5.

kunde string-beans

peas-

munhu o bhuganda

ENGLISH:  THE GUARD OF THE COW-PEAS IS THE ONE WHO EATS THEM.

The origin of the above proverb came from a man who was guarding a field of legumes. He was guarding it daily, but the legumes were still running out.

Finally they wondered, “Why do these legumes continue to run out?” One of them said, “Let us do a good research so that we can understand what is going on.” When they did such research, they discovered that the person who was guarding the legumes was actually eating them. That is why they said, “the guard of the cow-peas is the one who eats them.”

The proverb is likened to a man who destroys his own properties by abusing them, in his life. He, in effect, squanders his resources on wasteful usage. Instead of safeguarding them, he destroys them by abandoning and plundering them.

Such man is like the caretaker of the legumes who was eating them himself, because he was also destroying his own properties by abusing them. That is why people say to him that, “the guard of the cow-peas is the one who eats them.”

This proverb teaches people on how to have good care of their possessions, by stopping not misusing them, so that they can make more progress in their lives.

John 18: 2-5.

760. LISO TALA YA MILI.

Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile nimo go liso ugo gugutimila imili. Iliso linilo, ligagutimilaga umili bhogubhona ginhu jose jose ijo jilihabhutongi bholyo. Ulu munhu ulitumila chiza iliso lwakwe umili gokwe gugwikala mhola.

Aliyo lulu, umunhu uyo ulitumila bho gubhola mihayo mib’i, umili gokwe gugupandika makoye kunguno imihayo yiniyo yigagutulaga mugiti umili. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “liso tala ya mili.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagatumililaga chiza amiso gakwe bho gubhona mihayo misoga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayegaga ulu oyibhona imihayo iyo ili miza, kunguno igang’wenhelala matwajo gagujibheja chiza ikaya ja bhanhu bhakwe. Uweyi agagalemejaga amiso gakwe ugubhona imihayo imib’i, kunguno igenhaga makoye umukikalile ka bhanhu.

Umunhu ng’wunuyo, agabhalangaga abhiye inzila ja gugatumila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza iyo igenhaga matwajo miza, umukikalile kabho kugiki nabho bhikali mulisana. Hunagwene uweyi agabhabhilaga abhanhu giki, “liso tala ya mili.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugatumamila chiza amiso gabho bho gubhona mihayo miza na guyileka imib’i, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 20:15.

Luka 2:30.

Luka 11:34.

2 Wakorintho 3:7.

KISWAHILI: JICHO NI TAA YA MWILI.

Chanzo cha methali hiyo, chaangalia kazi ya jicho katika kuumulikia mwili. Jicho hilo, huumulikia mwili kwa kuangalia kitu chochote ambacho kiko mbele yake. Mtu atayelitumia jicho lake vizuri mwili wake utakuwa salama.

Lakini basi, mtu huyo akilitumia vibaya jicho lake kwa kuona vitu vibaya, mwili wake utapata matatizo, kwa sababu vitu hivyo huuweka mwili gizani. Ndiyo maana watu husema kwamba, “jicho ni taa ya mwili.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyatumia vizuri macho yake kwa kuona vitu vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, hufurahi akiona kitu kizuri kwa sababu kitu hicho huleta maendeleo kwenye familia za watu wake. Yeye huyazuia macho yake kuona vitu vibaya kwa sababu vinaleta matatizo kwenye maisha ya watu kwa kuiweka miili yao gizani.

Mtu huyo, huwafundisha wenzake namna ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuona vitu vinavyowaletea maendeleo katika maisha yao, ili miili yao isiishi gizani. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “jicho ni taa ya mwili.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyatumia vizuri macho yao kwa kuangalia vitu vizuri na kuyazuia kuangalia vitu vibaya, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao kwa kuishi katika mwanga, maishani mwao.

Mathayo 20:15. “Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’”

Luka 2:30. “Kwa maana macho yangu yameuona wokovu Wako,…”

Luka 11:34. “Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote umejaa giza.”

2 Wakorintho 3:7. “Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia,…”

eyes girl

Eyes child-

eyes african-child

ENGLISH: THE EYE IS THE LIGHT OF THE BODY.

The essence of the above proverb looks at the function of the eye which is to illuminate the body. The eye illuminates the body by looking at anything that is in front of it. A person who uses his eye well, his body will be safe.

But if a person misuses his eye by looking at evil things, his body will suffer, because those things keep the body in the darkness. That is why people say that, “the eye is the light of the body.”

Such proverb is likened with a person who makes good use of his or her eyes to make them see good things in his life. Such person is happy to see something good because it brings development to the families of his people. He keeps his eyes away from seeing evils because they bring trouble to people’s lives as they keep their bodies in darkness.

This person teaches his colleagues on how to make good use of their eyes by seeing the things that can bring them progress in their lives, so that their bodies do not live in darkness. That is why he tells people that, “the eye is the lamp of the body.”

This proverb teaches people on how to use their eyes properly by looking at good things and preventing them from watching evil things.

Matthew 20:15.