Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile bhukandi bho bhusu bho ngano. Olihoyi munhu uyo okandaga bhusu bho ngano ub’o bhugakandwa mpaga bhomonda na wigelelwa guzugwa mandazi, chapati na migate. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agayombaga giki “najikandandilile jumonda.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alindamu ugutumama milimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi na bhukamu bhutale kunguno ya bhutungilija bhokwe mpaga onamhala naonaga lulu uguitumama imilimo yiniyo. Uweyi agapandikaga matwajo mingi aha kaya yakwe kunguno ya bhukamu bhunubho ubho gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agakanda bhusu bho ngano mpaga bhumonda bho gwikoma guzugwa mandazi, chapati na migate, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe mpaga opandika matwajo mingi, umuwikaji bhokwe. “hunagwene agayombaga giki, “najikandile jumonda.”
Akahahile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gwigulambija gutumama milimo yabho bho nguvu ningi, kugiki bhadule kupandika matwajo gagubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Yahana 21:18.
KISWAHILI: NIMEUKANDA UKALAINIKA.
Chanzo cha msemo huo huongelea juu ya unga wa ngano. Alikuwepo mtu aliyekuwa akitengeneza unga huo wa ngano kwa kuukanda mpaka ukalainika kiasi cha kutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkakamavu wa kufanya kazi katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi na kwa bidii kubwa kwa sababu ya uaminifu wake huo, mpaga anazeeka ndipo anachoka kuzifanya kazi hizo. Yeye hupata mafanikio mengi katika familia yake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi, maishani mwake.
Mtu huyo hufanana na yule aliyekanda unga wa ngano mpaga ukalainika kiasi chakutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate, kwa sababu naye hufanya kazi zake kwa nguvu mpaka anapata mafanikio mengi maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao kwa nguvu nyingi, ili waweze kupata mafanikio mengi ya kuwasaidia katika kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Yahana 21:18.
ENGLISH: “I KNEADED IT UNTIL IT WAS SOFT.”
The origin of this saying is about wheat flour. There was a person who was making wheat flour by kneading it until it was soft enough to be used for baking buns, and bread. That is why he said that, “I kneaded it until it was soft.”
This saying is matched to a person who is hardworking in his life. This person, exerts himself to do his work with great strength and diligence because of his loyalty, when he gets old he gets tired of doing those jobs. He achieves a lot of success in his family because of his diligence in doing his works with great strength, in his life.
This person resembles the one who kneaded wheat flour until it was soft enough to be used for baking buns, and bread, because he also works hard until he achieves a lot of success in his life. That is why he says that, “I kneaded it until it was soft.”
This saying instills in people a clue of being honest and hard working enough to nicely fulfill their responsibilities, so that they can achieve countless successes which can help them in developing their family lives.
John 21:18.











