Sukuma Sayings

1037. OLINDA GWENHELWA ALUGUJA NANG’HO?

Alihoyi munhu umu chalo ja Sanjo uyo oliadaga ukumajisho ulu oluobhilingwa na bhiye. Umunhu ng’wunuyo olindilaga gwiza gubhabhuja duhu abho bhajaga ukujisho jinijo kugiki bhanomela imihayo iyo bhawilagwa na guigwa ukwenuko.

Nose abhanhu agabhanoja iki omanaga ubhabhugilija bhuli jigasho jene kunguno ya kugija guja bho gulindila gulomelwa nabhobhajaga koyi. Hunagwene abhanhu bhagamuja giki, “olinda gwenhelwa aliguja nang’ho?”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adinawiyambilija na nabhiye ijinagutumama imilimo aliyo ugwilombeleja ijiliwa ukubhiye bhenabho alinkamu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga wigashije duhu ulubhalija abhiye ugujutumama imilimo kunguno ya bhuyiyene na bhugokolo bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga wilombeleja jiliwa ukubhiye abho bhagiyambilijaga na bhichabho ugutumama ilimimo yabho, kunguno ya bhujidadilila bho milimo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oliadajaga ukumajigasho uyo alindilaga gubhabhuja abho bhagaja koyi kugiki bhanomele, kunguno nuweyi adiyambilija na bhiye ugutumama imilimo bho gulindalila gwiza gwilombeleja jiliwa ukubhanhu abho bhagatumama milimo yabho chiza. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagamujaga giki, “olinda gwenhelwa aliguja nang’ho?”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhumo bho guja kumajigasho na gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi na gujilanhana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 5:14.

Yakobo 5:19-20.

Tito 3:10-11.

KISWAHILI: UMESUBIRI KULETEWA NAKUENDA NAWE?

Alikuwepo mtu mmoja katika kijiji cha Sanjo ambaye hakuwa anahudhuria mikutano alipoalikwa na wenzake. Mtu huyo, alikuwa akisubiri kuja kuwauliza tu wale waliohudhuria ule mkutano ili wamwambia yale waliyoyasikia kwenye mkutano huo.

Mwishowe mtu huyo, alifikia hatua ya kuwachosha wale watu waliohudhuria mkutano aliokuwa akiwauliza mara kwa mara. Ndiyo maana walimuuliza kwamba, “umesubiri kuletewa na kuenda nawe?”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa hasaidiani na wenzake katika kufanya kazi, lakini ni mwenye bidii ya kuwaomba msaada wale wanaofanya kazi zao vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa amekaa tu wakati wenzake wanashirikiana kufanya kazi wakati huo wa kazi kwa sababu ya uvivu wake na kutokushirikiana na wenzake vizuri. Yeye huishi maisha ya kuombaomba kwa wale wanaoshirikiana kufanya kazi, kwa sababu ya kutokujali kwake kazi, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa hahudhurii mikutano ambaye alisubiri kuwauliza wale waliohudhuria kwenye mikutano hiyo, maishani mwake, kwa sababu naye huwa hashirikiani na wenzake katika kufanya kazi akisubiri kuwaomba msaada wale walioshirikiana vizuri kuyatekeleza majukumu yao. Ndiyo maana watu hao humuuliza kwamba, “umesubiri kuletewa na kuenda nawe?”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umoja wa kushirikiana vizuri katika kuhudhuria mikutano yao, na kusaidiana katika kufanya kazi, ili waweze kupata maendeleo ya kuwawezesha kulitunza vizuri familia zao, maishani mwao.

1Wakorintho 5:14.

Yakobo 5:19-20.

Tito 3:10-11.

market-280135__480

1036. ULIKUMILIJA MBULA OYINZA?

Imbuki ya kahayile kenako, yingilile kuli munhu uyo oikumilijaga mbula iyo yatulaga aliyo adinayinza. Uguyinza ilipona jiliwa mpaga ubhukabhanya ubhusiga na mitugo guti ng’ombe, mbuli nulu ng’holo na jingi kuti jinijo.

Giko lulu, uyo adinapandika jikolo guti jinijo, adazunilijiwe uguikumilija imbula, kunguno atali ndo. Uweyi uluikumilija ulu yiza iguntema ucha. Hunagwene umunhu uyo agaikumilija imbula yiniyo bhagamuja abhiye giki, “ulikumilija mbula oyinza?”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitulatulaga mkajile ka nyatale ahikanza atali ndo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’unuyo, adinabhukalalwa bho kuchola jikolo guti gutumama milimo yake bho bhukamu bhutale, kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga nhabhi bhuli makanza ahakaya yakwe, kunguno ya gwiyitya bhutale bhunubho, aliyo alimunhu ndo umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agaikumilija imbula aliyo atali uguyinza, kunguno nuweyi agiyityaga bhutale aliyo atali ndo bho kuguleka kutumama milimo guti giki osabha sabho, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagamujaga giki, “ulikumilija mbula oyinza?”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka gwitula bhutale bho gwigulambija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule kupandika sabho ja gutumamila chiza, umuwikaji bhobho.

Zaburi 34:13-14.

Zaburi 15:4-5.

Zaburi 16:1-3.

 

KISWAHILLI: UNAISIFIA MVUA UMENUNUA NINI?

Chanzo cha msemo huo, chatokea kwa mtu aliyekuwa akisifia mvua iliyokuwa ikinyesha wakati hajanunua chochote kupitia mazao yake. Kununua kitu  ni kupata mazao mengi na kuuza chakula au kubadilisha mazao hayo na mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika.

Hivyo basi, mtu yule ambaye hajanunua chochote haluhusiwi kuisifia mvua hiyo inayonyesha, kwa sababu bado ni mdogo. Mtu huyo, akiisifia mvua hiyo ikija itamkata afe. Ndiyo maana watu walimuuliza mtu huyo kwamba, “unaisifia mvua umenunua nini?”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujifanya kuwa ni mkubwa wakati yeye ni mdogo, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hapendi kufanya kazi ya kumwezesha kupata mali kwa bidii kubwa, kwa sababu ya uvivu wake huo. Yeye huwa maskini kila wakati kwenye familia yake, kwa sababu ya kujifanya kwake kuwa mkubwa, wakati yeye ni mdogo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeisifia mvua wakati bado hajanunua chochote, katika maisha yake, kwa sababu naye hujifanya kuwa mkubwa kwa kuacha kufanya kazi zake kwa bidii wakati yeye ni mtu mdogo tu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuuliza kwamba, “unaisifia mvua umenunua nini?”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kujifanya wakubwa wakati wao ni wa kawaida, kwa kujibidisha kufanya kazi zao vizuri, ili waweze kupata mali za kutumia vizuri, maishani mwao.

Zaburi 34:13-14.

Zaburi 15:4-5.

Zaburi 16:1-3.

 

ENGLISH: YOU PRAISE THE RAIN WHAT DID YOU BUY?

The source of this saying can be traced back to a person who was praising the rain that was falling while he had not bought anything through his crops. To buy something is to get a lot of crops and sell food or exchange those crops with: cows, goats, sheep and so on.

Therefore, the person who has not bought anything is not allowed to praise the rain while it is raining, because he is still young. If such person praises the rain when it comes will cut him to death. That is why people asked such man that, “You praise the rain, what have you bought?”

This saying is compared to the person who pretends to be a big one while he is a small one, in his life. Such person does not like to work enough to enable him get wealth with great effort, because of his laziness. He is always poor in his family, because of his pretending to be big, while he is small, in his life.

This person is similar to the one who praised the rain when he has not yet bought anything in his life, because he also pretends to be big by stopping to do his work diligently while he is just a small person in his life. That is why people ask him that, “you praise the rain, what have you bought?”

This saying, imparts in people an idea of stopping pretending to be great while they are normal ones, by forcing themselves to do their jobs well, so that they can get many assets enough to run well in their lives.

Psalm 34:13-14.

Psalm 15:4-5.

Psalm 16:1-3.

 

 

umbrella-3219621__480

 

 

 

1035. BHUSAB’I BHO BHANGI DUHU ALAYISE NDUHU.

Imbuki ya kahayile kenako ingilile kubhanhu abho bhilolelaga mbina muchalo ja Idisa. Imbina yiniyo yali ya bhagika na bhagalu. Bhuli ningi ng’wene oli na bhanyalali bhakwe.

Aho yashila imbina yiniyo, abhiloleji bhabhugika na bhabhugalu, bhagayuhaya giki bhuli bhene bhakindaga mpaga nose bhuhaya gwiduma aliyo bhiloleji duhu abho bhadapandikaga isabho. Abhalingi bhabho habho bhagasolaga isabho ijahambina yiniyo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “bhusab’i bho bhangi duhu alayise nduhu.”

Akahahile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalijimijaga sagala ilikanzwa lwakwe ilya milimo bho gwikala mumaligusha ayo gadina solobho ukuli weyi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, aligatumilaga ilikanzwa lwakwe bho gwikala mumaligusha ga gwingila diyu mpaga mhindi, bho nduhu ugupandika solobho yoseyose, kunguno ya gukija gwiganika gokwe chiza. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa aha ng’wakwe kunguno ya gulijimija sagala ilikanza lwakwe linilo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhihalalikila bhukindi bho mbina aliyo isabho jalijabhalingi bhabho, kunguno nuweyi agalijimejaga sagala ilikanza lwakwe bho nduhu gupandika josejose umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “bhusabhi bho bhangi duhu alayise nduhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanzwa lyabho bho gutumama milimo iyo idulile gubhenhela solobho yoseyose, kugiki bhadule gupandika sabho ja gubhambilija chiza umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 9:24-27.

Yakobho 1:12-14.

KISWAHILI: UTAJIRI WA WENGINE TU LAKINI SISI HAKUNA.

Chanzo cha msemo huo, ulianzia kwa watu waliokuwa wakiangalia ngoma kwenye kijiji cha Idisa. Ngoma hiyo, ilikuwa ya wagika na wagalu. Kila manju alikuwa na mashabiki wake.

 Ilipoisha ngoma hiyo, wale mashabiki wa pande zote mbili wakaanza kudai kwamba kila kundi limeshinda mpaka mwishowe wakataka kugombanga wakati wao ni watazamaji tu wa ngoma hiyo. Mamanju wa ngoma hiyo ndiyo waliochukua mali za hapo. Ndiyo maana mashabiki hao walisema kwamba, “utajiri wa wengine tu lakini sisi hakuna.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huutumia ovyo muda wake wa kufanya kazi, kwa kujali mambo yasiyo na faida kwake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia muda wake kwenye michezo ya kuanzia asubuhi hadi jioni, bila kupata faida yoyote, kwa sababu ya kutokufikiri vizuri kwakwe. Yeye hukosa mali za kumsaidia katika kutunza familia yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na wale mashabiki wa ngoma waliokuwa wakibishania ushindi wa ngoma mpaka wakataka kukosana bure, kwa sababu naye huupoteza muda wake wa kazi kwenye michezo ambayo haimletei faida yoyote, maishani mwake. Ndiyo maana yeye alisema kwamba, “utajiri wa wengine tu lakini sisi hakuna.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao kwa kufanya kazi ziwezazo kuwaletea faida yoyote, ili waweze kupata mali za kutosha kuwasaidia vizuri maishani mwao.

1Wakorintho 9:24-27.

Yakobho 1:12-14.

ENGLISH: ONLY OTHER PEOPLE’S WEALTH, BUT WE DO NOT HAVE ANY.

The foundation of the above saying started from the people who were watching a game in Idisa village. Such dance was of Wagika and Wagalu group. Each leader of above groups had followers.

When the game ended, the followers of both sides started to claim that each group had won until finally they wanted to fight when they were just viewers of such game. The leaders of each group are the ones who took the properties there. That is why the followers said that, “only other people’s wealth, but we do not have any.”

This saying is compared to the person who wastes his working time by caring about things that are not beneficial to him in life. Such person, spends his time in watching games from morning to evening, without getting any benefit, because of his lack of good discerning. He lacks assets for helping him in taking care of his family life.

This person is similar to those game followers who were arguing about the victory of such game until they wanted to hurt one other for nothing, because he also wastes his working time by watching games that do not bring him any benefit in his life. That is why he said that, “only other people’s wealth, but we do not have any.”

This saying, teaches people about spending their time by doing jobs that can bring them profits, so that they can get enough assets to nicely run their lives.

1 Corinthians 9:24-27.

James 1:12-14.

drums-5935804__480

dance-5935800__480

african-traditional-dance-2934852__480

1032. ILINO ILYA HA NHELO ITI B’UGOTA B’O B’UYU.

Akahayile kenako, kingilile kuli munhu uyo uli na b’uyu uyo wikalaga Ng’wagala. Umunhu ng’wunuyo olemaga uguwilwa igiki alina b’uyu kunguno oli omala amino usaja lino lyaha mhelo tuhu.

Lushugu lumo agenhelwa maguha kugiki alye, huna uduma ugugalya kunguno ya guyagaiya Mino. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “ilino ilya ha nhelo iti b’ugota b’o b’uyu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ozumalikilwa na myaji okwe uyo oli ang’wisanije gete, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, opandikaga sabho na jikolo ja mbika ningi ija gufumila kuli myaji okwe ng’winuyo. Kiyiniyo lulu, ubhuzumaliki bho myaji okwe ng’winuyo, bhugang’wenheleja kugayiwa umunhu uogung’wambilija, kunguno oliang’wisanijia weyi duhu umukikalile kakwe. Uweyi agikalaga na makoye ga gugayiwa isabho ja gungunana aha kaya yakwe yiniyo.

Umunhu ung’wunuyo, agikolaga nuyo ali na lino lya ha mhelo ilolidang’wambilijije ugulya amaguha ayo agenhelwa, kunguno nuweyi ogaiwa umunhu uogung’wingija amakoye aha kaya yakwe gwingila haho ozumalikilwa nu myaji okwe uyo ong’wambilija, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “ilino ilya ha mhelo iti b’ugota b’o b’uyu.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gujilabhila chiza isabho ni jitumamilo jabho, umukikalile kabho, kugiki didule gubhambilija chiza ihikanza bhalinajo, umubhulamu bhobho bhunubho.

1Wakorintho 12:14-26.

1Wakorintho 13:11-12.

KISWAHILI: JINO LA PEMBENI SIYO DAWA YA MAPENGO.

Msemo huo, ulianzia kwa mtu mwenye mapengo aliyekuwa anaishi Ng’wagala. Mtu huyo, alikuwa akikataa kuambiwa kuwa ana mapendo kwa sababu ya kubakiwa na jino moja la pembeni baada ya yale mengine kung’oka.

Siku moja aliletewa miwa ili ale, ndiyo akashindwa kuila kwa sababu ya kukosa meno. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “jino la pembeni siyo dawa ya mapengo.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule aliyefiwa na mzazi wake aliyekuwa akimtegemea sana katika maisha yake. Mtu huyo, alikuwa akipokea mali na vitu vya aina mbalimbali kutoka kwa mzazi wake huyo. Kwa hiyo, kufariki kwa mzazi wake huyo, kumemsababishia kukosa mtu wa kumsaidia kwa sababu alikuwa akimtegemea yeye tu katika maisha yake. Yeye huishi katika hali ya kukumbwa na matatizo ya kukosa mali za kumsaidia katika familia yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa na jino la pembeni ambalo halikumsaidia kuweza kula miwa aliyoletewa, kwa sababu naye alikosa wa kumsaidia katika familia yake baada ya mzazi wake kufariki. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “jino la pembeni siyo dawa ya mapengo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutumia vizuri mali walizozipata katika utekelezaji wa majukumu yao, ili ziweze kuwasaidia vizuri wakati wakiwa nazo, maishani mwao.

1Wakorintho 12:14-26.

1Wakorintho 13:11-12.

ENGLISH: A SIDE TOOTH IS NOT A MEDICINE FOR GAPS.

The above saying started with a man that has gaps who lived in Ng’wagala. This man was refusing to be told that he has gaps in his mouth because he had one front tooth that was left after the others had fallen out.

One day sugarcane was brought for him to eat, but he couldn’t eat it because of missing teeth. That is why people told him that, “a side tooth is not a medicine for gaps.”

This saying is compared to the person who lost his parent to whom he depended on in his life. Such person used to receive wealth and various things from his parent. Therefore, the death of his parent has caused him to have no one who can help him because he was only relying on him in his life. He lives in a situation where he faced many problems of not having assets to support him in his family.

This person is similar to the one who had a side tooth that did not help him to be able to eat the cane that was brought to him, because he also lacked someone to help him in his family after his parent died. That is why he says that, “a side tooth is not a cure for gaps.”

This saying, teaches people about using the assets they got in performing of their duties, so that they can help them well when they have them, in their lives.

1 Corinthians 12:14-26.

1 Corinthians 13:11-12.

man-tongues

africa-2002838__480

africa--=

1029. OGWILAGA NINDO.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya ng’wa munhu uyo ogwilaga ningo. Olihoyi munhu uyo oliolinha mlinti lya minyembo kugiki ayobhe minyembe ya gulwa. Umunhu ng’wunuyo oliadina witegeleja bhutale umukalinhile kakwe kenako kunguno agatyuja gwiza hasi uyigwila inindo yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “ogwilaga nindo.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ajaga ng’wichola ugashoga adapandikile josejose, umubhuchoji bhokwe bhunubho. Umunhu ng’wunuyo agacholaga sabho bho nduhu gubhiza na uwitegeleja bhutale, kunguno ya gukija ugwiganika chiza umumasala gakwe. Uweyi agashoga kaya bho nduhu nulu ginhu josejose umumakono gakwe, kunguno ya gubhugayiwa uwitegeleja bhunubho, umukacholele kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agalinha mulinti lya minyembe bho nduhu gubhiza na witegeleja bhutale mpaga nose ugwila nindo, kunguno nuweyi agacholaga sabho bho nduhu gubhiza na witegeleje bhutale umubhuchoji bhokwe bhunubho mpaga nose ojigayiwa isabho jinijo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ogwilaga nindo.” Imaana ya gwila nindo ili gugayiwa ijo olujicholaga, unchoji o sabho ng’wunuyo, ushoga makono duhu ugukaya yakwe.

Akahayile kenako kalanga bhachoji bha sabho higulya ya gubhiza na witegeleja bhutale umukacholele kabho, kugiki bhadule gujipandika isabho ijo bhalijichola, umuwikaji bhobho.

Luka 15:13-14.

Luka 16:3-9.

KISWAHILI: AMEANGUKIA PUA.

Msemo huo, huongelea juu ya mtu aliyeangukia pua. Alikuwepo mtu mmoja aliyekwea kwenye mtu wa maembe ili achume maembe ya kula. Mtu huo, aliukwea mtu huo wa muembe bila kuwa na umakini mkubwa katika ukweaji wake, kwa sababu aliteleja akaangukia pua. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “ameangukia pua.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huenda kutafuta mali na kurudi bila kupata chochote, katika utafutaji wake. Mtu huyo, hutafuta mali hizo bila kuwa na umakini mkubwa kwa sababu kutokufikiri vizuri katika akili zake. Yeye hurudi nyumbani kwake bila kuwa kitu chochote katika mikono yake, kwa sababu ya kuukosa umakini huo katika utafutaji wake huo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekwea kwenye mti wa maembe bila kuwa na umakini mkubwa, mpaka mwishowe akaangukia pua, kwa sababu naye hutafuta mali bila kuwa na huo umakini katika utafutaji, mpaka anashindwa kupata chochote. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “ameangukia pua.” Maana ya kuangukia pua ni kukosa au kushindwa kupata mali na kurudi nyumbani mikono mitupu kwa mtafutaji huyo.

Msemo huo, hufundisha watafutaji wa mali juu ya kuwa na umakini mkubwa katika utafutaji wao, ili waweze kufanikiwa kupata mali wanayoitafuta, katika maisha yao.

Luka 15:13-14.

Luka 16:3-9.

ENGLISH: HE HAS FALLEN ON HIS/HER NOSE.

This saying speaks of a person who fell on his nose from a Mango tree. There was one man climbed on a mango tree carelessly to pick mangoes for eating. He fell on his nose to the point of hurting it. That is why people said to him that, “He has fallen on his nose.”

This saying is compared to a man who goes about seeking wealth but returns without getting anything, in his search. He did not look for those treasures with much caution because of not thinking well in his mind. He returns home with nothing in his hands.

This man is like the one who climbed on a mango tree without much attention, until he finally fell on his nose, because he too seeks wealth without having that focus in searching, until he fails to get anything. That is why people say to him that, “he has fallen on his nose.” The meaning of falling on one’s nose is to miss or fail to acquire property and return home empty-handed to his family.

This saying teaches property seekers to be very careful in their  ways of searching, so that they can successfully find the property which they are looking for, in their lifetime.

Luke 15: 13-14.

Luke 16: 3-9.

male-4948672__480

girl-6274742__480

black-man-7154113__480