1032. ILINO ILYA HA NHELO ITI B’UGOTA B’O B’UYU.

Akahayile kenako, kingilile kuli munhu uyo uli na b’uyu uyo wikalaga Ng’wagala. Umunhu ng’wunuyo olemaga uguwilwa igiki alina b’uyu kunguno oli omala amino usaja lino lyaha mhelo tuhu.

Lushugu lumo agenhelwa maguha kugiki alye, huna uduma ugugalya kunguno ya guyagaiya Mino. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “ilino ilya ha nhelo iti b’ugota b’o b’uyu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ozumalikilwa na myaji okwe uyo oli ang’wisanije gete, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, opandikaga sabho na jikolo ja mbika ningi ija gufumila kuli myaji okwe ng’winuyo. Kiyiniyo lulu, ubhuzumaliki bho myaji okwe ng’winuyo, bhugang’wenheleja kugayiwa umunhu uogung’wambilija, kunguno oliang’wisanijia weyi duhu umukikalile kakwe. Uweyi agikalaga na makoye ga gugayiwa isabho ja gungunana aha kaya yakwe yiniyo.

Umunhu ung’wunuyo, agikolaga nuyo ali na lino lya ha mhelo ilolidang’wambilijije ugulya amaguha ayo agenhelwa, kunguno nuweyi ogaiwa umunhu uogung’wingija amakoye aha kaya yakwe gwingila haho ozumalikilwa nu myaji okwe uyo ong’wambilija, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “ilino ilya ha mhelo iti b’ugota b’o b’uyu.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gujilabhila chiza isabho ni jitumamilo jabho, umukikalile kabho, kugiki didule gubhambilija chiza ihikanza bhalinajo, umubhulamu bhobho bhunubho.

1Wakorintho 12:14-26.

1Wakorintho 13:11-12.

KISWAHILI: JINO LA PEMBENI SIYO DAWA YA MAPENGO.

Msemo huo, ulianzia kwa mtu mwenye mapengo aliyekuwa anaishi Ng’wagala. Mtu huyo, alikuwa akikataa kuambiwa kuwa ana mapendo kwa sababu ya kubakiwa na jino moja la pembeni baada ya yale mengine kung’oka.

Siku moja aliletewa miwa ili ale, ndiyo akashindwa kuila kwa sababu ya kukosa meno. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “jino la pembeni siyo dawa ya mapengo.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule aliyefiwa na mzazi wake aliyekuwa akimtegemea sana katika maisha yake. Mtu huyo, alikuwa akipokea mali na vitu vya aina mbalimbali kutoka kwa mzazi wake huyo. Kwa hiyo, kufariki kwa mzazi wake huyo, kumemsababishia kukosa mtu wa kumsaidia kwa sababu alikuwa akimtegemea yeye tu katika maisha yake. Yeye huishi katika hali ya kukumbwa na matatizo ya kukosa mali za kumsaidia katika familia yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa na jino la pembeni ambalo halikumsaidia kuweza kula miwa aliyoletewa, kwa sababu naye alikosa wa kumsaidia katika familia yake baada ya mzazi wake kufariki. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “jino la pembeni siyo dawa ya mapengo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutumia vizuri mali walizozipata katika utekelezaji wa majukumu yao, ili ziweze kuwasaidia vizuri wakati wakiwa nazo, maishani mwao.

1Wakorintho 12:14-26.

1Wakorintho 13:11-12.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.