1035. BHUSAB’I BHO BHANGI DUHU ALAYISE NDUHU.

Imbuki ya kahayile kenako ingilile kubhanhu abho bhilolelaga mbina muchalo ja Idisa. Imbina yiniyo yali ya bhagika na bhagalu. Bhuli ningi ng’wene oli na bhanyalali bhakwe.

Aho yashila imbina yiniyo, abhiloleji bhabhugika na bhabhugalu, bhagayuhaya giki bhuli bhene bhakindaga mpaga nose bhuhaya gwiduma aliyo bhiloleji duhu abho bhadapandikaga isabho. Abhalingi bhabho habho bhagasolaga isabho ijahambina yiniyo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “bhusab’i bho bhangi duhu alayise nduhu.”

Akahahile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalijimijaga sagala ilikanzwa lwakwe ilya milimo bho gwikala mumaligusha ayo gadina solobho ukuli weyi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, aligatumilaga ilikanzwa lwakwe bho gwikala mumaligusha ga gwingila diyu mpaga mhindi, bho nduhu ugupandika solobho yoseyose, kunguno ya gukija gwiganika gokwe chiza. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa aha ng’wakwe kunguno ya gulijimija sagala ilikanza lwakwe linilo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhihalalikila bhukindi bho mbina aliyo isabho jalijabhalingi bhabho, kunguno nuweyi agalijimejaga sagala ilikanza lwakwe bho nduhu gupandika josejose umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “bhusabhi bho bhangi duhu alayise nduhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gulitumila ilikanzwa lyabho bho gutumama milimo iyo idulile gubhenhela solobho yoseyose, kugiki bhadule gupandika sabho ja gubhambilija chiza umuwikaji bhobho.

1Wakorintho 9:24-27.

Yakobho 1:12-14.

KISWAHILI: UTAJIRI WA WENGINE TU LAKINI SISI HAKUNA.

Chanzo cha msemo huo, ulianzia kwa watu waliokuwa wakiangalia ngoma kwenye kijiji cha Idisa. Ngoma hiyo, ilikuwa ya wagika na wagalu. Kila manju alikuwa na mashabiki wake.

 Ilipoisha ngoma hiyo, wale mashabiki wa pande zote mbili wakaanza kudai kwamba kila kundi limeshinda mpaka mwishowe wakataka kugombanga wakati wao ni watazamaji tu wa ngoma hiyo. Mamanju wa ngoma hiyo ndiyo waliochukua mali za hapo. Ndiyo maana mashabiki hao walisema kwamba, “utajiri wa wengine tu lakini sisi hakuna.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huutumia ovyo muda wake wa kufanya kazi, kwa kujali mambo yasiyo na faida kwake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia muda wake kwenye michezo ya kuanzia asubuhi hadi jioni, bila kupata faida yoyote, kwa sababu ya kutokufikiri vizuri kwakwe. Yeye hukosa mali za kumsaidia katika kutunza familia yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na wale mashabiki wa ngoma waliokuwa wakibishania ushindi wa ngoma mpaka wakataka kukosana bure, kwa sababu naye huupoteza muda wake wa kazi kwenye michezo ambayo haimletei faida yoyote, maishani mwake. Ndiyo maana yeye alisema kwamba, “utajiri wa wengine tu lakini sisi hakuna.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia muda wao kwa kufanya kazi ziwezazo kuwaletea faida yoyote, ili waweze kupata mali za kutosha kuwasaidia vizuri maishani mwao.

1Wakorintho 9:24-27.

Yakobho 1:12-14.

ENGLISH: ONLY OTHER PEOPLE’S WEALTH, BUT WE DO NOT HAVE ANY.

The foundation of the above saying started from the people who were watching a game in Idisa village. Such dance was of Wagika and Wagalu group. Each leader of above groups had followers.

When the game ended, the followers of both sides started to claim that each group had won until finally they wanted to fight when they were just viewers of such game. The leaders of each group are the ones who took the properties there. That is why the followers said that, “only other people’s wealth, but we do not have any.”

This saying is compared to the person who wastes his working time by caring about things that are not beneficial to him in life. Such person, spends his time in watching games from morning to evening, without getting any benefit, because of his lack of good discerning. He lacks assets for helping him in taking care of his family life.

This person is similar to those game followers who were arguing about the victory of such game until they wanted to hurt one other for nothing, because he also wastes his working time by watching games that do not bring him any benefit in his life. That is why he said that, “only other people’s wealth, but we do not have any.”

This saying, teaches people about spending their time by doing jobs that can bring them profits, so that they can get enough assets to nicely run their lives.

1 Corinthians 9:24-27.

James 1:12-14.

drums-5935804__480

dance-5935800__480

african-traditional-dance-2934852__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.