Sukuma Proverbs

1185. NALIB’IMBILA MJISINZA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile bhubhimbi bho numba ubho bhudadulikanile. Alihoyi munhu uyo obhimbaga numba bho gutumila jisinza mpaga uduma ugubyedecha kunguno ya gutumila ginhu jidamu jinijo. Uweyi oliadatumilaga ingoye, maswa, na manti amadimu ubhutumami bhokwe. Hunagwene agayomba giki, “nalib’imbila mjisinza.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alindimu ugwelelwa wangu iyo agawilagwa nabhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga alemile ugwigwa imihayo ya bhiye kunguno ya nhinda jakwe jinijo. Uweyi agagayiyagwa abhanhu abha guhoya nanghwe aka haya yakwe, kunguno ya bhudamu bho gwelelwa wangu imihayo iyo agawilagwa na bhiye, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu mimbiji o mujisinza uyo adabyedechije, kunguno nuweyi alindamu ugugwelelwa wangu imihayo iyo agawilagwa na bhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene umunhu uyo agahoyaga nanghwe agayombaga giki, “nalib’imbila mujisinza.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigwa na gwelelwa wangu imihayo iyo bhagawilagwa na bhichabho, bho guleka gubhiza bhadamu guti jisinza, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Zaburi 95:7b-8.

Wagalatia 3:1-6.

Mathayo 16:21-23.

KISWAHILI: NAEZEKEA CHUMA.

Methali hiyo, huongelea uelezekaji wa nyumba usiowezekana. Alikuwepo mtu aliyekuwa akiezekea chuma nyumba yake kwa muda mrefu bila mafanikio kwa sababu ya kutumia kitu kigumu. Yeye hakutumia kamba, nyasi, na miti migumu inavyokiwa katika kazi yake hiyo. Ndiyo maana alisema kwamba, “naezekea chuma.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mgumu wa kuelewa maneno anayoambiwa na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, hukataa ushauri wa wenzake ambao ungeweza kumsaidia vizuri katika familia yake, kwa sababu ya kiburi chake hicho. Yeye huishi peke yake katika familia yake hiyo, kwa sababu ya ugumu wake huo wa kuelewa anachoambiwa na wenzake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule alieyezekea chuma nyumba yake mpaka akashindwa kufaulu, kwa sababu naye ni mgumu wa kuelewa kile anachoambiwa na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana yule anayeongea naye husema kwamba, “naezekea chuma.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa wepesi wa kusikia na kuelewa kwa haraka ushauri wanaopewa na wenzao, badala ya kuwa waguma kama chuma, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Zaburi 95:7b-8.

Wagalatia 3:1-6.

Mathayo 16:21-23.

ENGLISH: I HAVE AN IRON ROOFING.

The above proverb speaks of an impossible roofing of a house. There was a man who was roofing his house by using metal for a long time without being successful because of using something which is hard. He did not use ropes, grasses, and hardwoods in his work. That is why he said that, “I have an iron roofing.”

This proverb is related to a person who has difficult in understanding words which said to him by his colleagues, in his life. Such person rejects advises of his colleagues that could help him well in his family, because of his pride. He lives alone in his family, because of his difficulty in understanding what his peers say to him in his life.

This person resembles the one who roofed his house by using iron until he failed, because he has also difficult in understanding what his colleagues say in his life. That is why he says to the one who is talking to him that, “I have an iron roofing.”

This proverb imparts in people an idea of being quick to hear and quickly understand the advises which are given to them by their nobles, instead of being stubborn like iron, so that they can raise their families well, in their lives.

Psalm 95:7b-8.

Galatians 3:1-6.

Matthew 16:21-23.

roofing-nails-4631354__480

roof-1559803__480

iron-7391493__480

1184. NGIKULU NG’WAGALA, UNTWE MONDO.

Imbuki ya lusumo lunulo, imhoyelile munhu ngikulu uyo ali na miaka mingi. Ungikulu ng’wunuyo, adulile gugachala amiganiko gakwe kungi niyo kule ulu mulilomela mhayo nebhe nuweyi. Uweyi adulile nulu gudedebhala duhu, nulu gukamala bho nduhu nulu guyomba mhayo ulu alilomela mhayo na munhu. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ngikulu Ng’wagala, untwe Mondo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe ukunu amiganiko gakwe gali kungi niyo kule naho alitumamila unimo gokwe gunuyo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajaga gujulima kungunda, aliyo amiganiko gakwe gali ha kaya yakwe, kunguno ya gugayiwa witegeleja bho gutumama nimo gumo bhuli likanza. Uweyi agadumaga uguimala chiza imilimo yakwe kunguno ya gudilila mihayo mingi umubhutumami bho milimo yakwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ngikulu uyo wilomelaga mhayo na ng’wiye ukunu amiganiko gakwe gali kule na henaho, kunguno nuweyi agatumamaga nimo ukunu amiganiko gakwe gali kule na ha nimo gunuyo, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ngikulu Ng’wagala, untwe Mondo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo yabho bho gugatuula amiganiko gabho haho nimo uyo bhaligutumama, kugiki bhadule gupandika sabho ningi umubhutumami bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 13:10-15.

KISWAHILI: BIBI KIZEE MWAGALA, KICHWA MONDO.

Chanzo cha methali hiyo, humuongelea bibi kizee mwenye miaka mingi. Bibi kizee huyo, aweza kuyapeleka mawazo yake kwingine wakati munaongea neno fulani naye. Yeye aweza hata kuduwaa tu kwa kukaa kimya wakati anaongea neno fulani na mwenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “bibi kizee Mwagala, kichwa Mondo.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi wakati mawazo yake yako kwingine ambako ni mbali na pale, katika maisha yake. Mtu huyo, huenda kulima shambani wakati mawazo yake yako nyumbani kwake, kwa sababu ya kukosa umakini wa kutekeleza jambo moja kwanza na kulimaliza. Yeye hushindwa kuzimaliza vizuri kazi zake, kwa sababu ya kufikiria kitu kingine wakati anafanya kazi  zake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule bibi kizee aliyeweka mawazo yake kwingine wakati anaongea na mwenzake, kwa sababu naye huyaweka mawazo yake mbali na kazi anayoifanya wakati huo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “bibi kizee Mwagala, kichwa Mondo.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi zao kwa kuweka mawazo yao kwenye kazi hizo wanazozifanya wakati huo, ili waweze kupata mali nyingi katika kazi zao hizo, maishani mwao.

Mathayo 13:10-15.

 

ENGLISH: OLD LADY MWAGALA, HEAD MONDO.

The cradle of the overhead proverb is talking about an old woman who had many years of old. Such old lady could take her thoughts elsewhere while talking to her. She could even become stunned just by staying silent when she is speaking about something to her partner. That is why people said about her that, “old lady Mwagala, head Mondo.”

This proverb is compared to a person who works when his thoughts are elsewhere, which is far from there, in his life. Such person goes to work to the field while his mind is at home, because of lack of focus enough to do one thing first and finish it. He fails to complete his tasks properly, because of thinking about something else while doing his tasks, in his life.

This person is similar to the old lady who put her thoughts elsewhere when she was talking to her partner, because he also keeps his thoughts away from the work which he is doing at that time. That is why people tell him that, “old lady Mwagala, head Mondo.”

This proverb teaches people about doing their works by putting their thoughts on the works which they are doing at that time, so that they can get a lot of wealth in their works in daily lives.

Matthew 13:10-15.

 

african-6261815__480

1180. ULINOGELA JIB’ELE.

Olihoyi munhu uyo agalima lishamba lya bhulubha bihi na nzila. Umunhu ng’wunuyo, ulimaga gwingila diyu mpaga mhindi kunguno ya bhukamu bhokwe bhunubho. Aliyo lulu, uweyi lyashigaga likanza uyulima hado hado kunguno ya bhunoge bho bhugugutumama likanza lilihu unimo gokwe gunuyo. Hunagwene abhanhu abho bhabhitaga aha nzila yiniyo, bhagang’wila giki, “ulinogela jib’ele.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyumilijaga gutumama nimo ndamu mpaga ogumala chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikomejaga kutumama milimo yakwe bho gwingila diyu mpaga mhindi kunguno aidebhile isolobho ya milimo yakwe yiniyo, aha shigu ijahabhutongi. Uweyi agapandikaga majikolo mingi noyi aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya wiyumilija bhokwe ubho gutumama nimo mpaga ogumala chiza, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nimi obhulubha uyo olimaga gwingila diyu mpaga mhindi, kunguno nuweyi agigulambijaga gutumama milimo yakwe bho gwingila diyu mpaga oimala chiza, umukikalile kakwe. Hunagwene bhanhu bhagang’wilaga giki, “ulinogela jib’ele.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gutumama milimo yabho bho gwiyumilija mpaga bhayimala chiza, kugiki bhadule gupandika majikolo mingi, umuwikaji bhobho.

Luka 13:22-24.

Mathayo 10:16-23.

Mathayo 19:27-29.

KISWAHILI: UNACHOKA KWA FAIDA.

Alikuwepo mtu aliyelima shamba la pamba karibu na njia. Mtu huyo, alikuwa akilima shambani mwake humo kuanzia asubuhi hadi jioni. Lakini ulifika wakati, akawa analima pole pole kwa sababu ya uchovu wa kufanya kazi yake hiyo kwa muda mrefu. Ndiyo maana watu waliokuwa wakipita kwenye njia hiyo, walimwambia kwamba, “unachoka kwa faida.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia kufanya kazi ngumu mpaka anaimaliza, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu anazielewa faida za kazi hizo, katika siku za mbeleni. Yeye hupata mali yenye thamani ya kuwa na vitu vingi sana kwenye familia yake, kwa sababu ya uvumilivu wake huo wa kufanya kazi mpaka anaimaliza vizuri, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mkulima wa pamba aliyelima kuanzia asubuhi hadi jioni, kwa sababu naye hujibidisha kufanya kazi zake kwa uvumilivu kuanzia asubuhi hadi anazimaliza vizuri, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “unachoka kwa faida.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi zao kwa uvumilivu mpaga wanazimaliza vizuri, ili waweze kupata mafanikio ya kuwa na mali nyingi, maishani mwao.

Luka 13:22-24.

Mathayo 10:16-23.

Mathayo 19:27-29.

ENGLISH: YOU ARE GETTING TIRED FOR PROFITS

There was a man who cultivated a cotton field near a pathway. Such man was farming in his field from morning to evening. But when the time came, he was slowly plowing because of the fatigue of doing his work for a long time. That is why the people who were passing by that way, told him that, “you are getting tired for profits.”

This proverb is compared to the person who endures doing hard work until he finishes it, in his life. Such person tries to do his work from morning to evening because he understands the benefits of such work in the future. He gets a valuable asset enough to have many things in his family, because of his patience of working until he finishes it well, in his life.

This person is similar to the cotton farmer who cultivated from morning to evening, because he also has to do his work patiently from morning until he finishes it well, in his life. That is why people tell him that, “you are getting tired for profits.”

This proverb, teaches people about doing their works with patience until they finish them well, so that they can get the success of having a lot of wealth in their lives.

Luke 13:22-24.

Matthew 10:16-23.

Matthew 19:27-29.

farmer-5353778__480

1179. BHUSOGA WIKOB’A, MUNDA B’UB’OLE.

Ulusumo lunulo, lulolile wiza bho hanze ya ginhu na bhubhi bho mugati yajo. Olihoyi munhu uyo agagubhona nyembe gusoga gete mpaka wiyangula gugutona kugiki agulye kunguno ya wiza bho hanze yago bhunubho. Aho ugukubhula igiki wandye ugugulya ugubhona giki gubholile gashinaga umugati yago. Hunagwene agayomba giki, “bhusoga wikob’a, munda b’ub’ole.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ni hanga lya wiza aliyo amiito gakwe gali gabhub’i, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyolechaga guti owiza ubho gunhola aliyo agiganikaga miganiko mab’i umunholo yakwe, kunguno ya miito gakwe aga bhub’i genabho. Uweyi agenhelejaga bhanhu gwikenya aha kaya yakwe, kunguno ya miito gakwe aga bhub’i genayo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nyembe uyo goli gusoga ihanze aliyo gubholile umugati yago, kunguno nuweyi ali ni hanga lya wiza aliyo amiito gakwe gali ga bhub’i, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “bhusoga wikob’a, munda b’ub’ole.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guleka kajile kagwita yabhub’i bho gwita miito gawiza bhuli makanza, kugiki bhadule gwikala bho mholele, umukaya jabho.

Mathayo 7:15-17.

Luka 6:43-45.

Mathayo 23:27-28.

KISWAHILI: UZURI WA NGOZI, TUMBONI UOZO.

Methali hiyo, huangalia uzuri wa nje ya kitu fulani na ubaya uliyopo ndani yake. Alikuwepo mtu ambaye aliliona embe zuri sana mpaka akaamua kulichuma ili alile kwa sababu ya uzuri wake huo wa nje. Alipolimenya embe hilo, aligundua kwamba, kumbe lilikuwa limeoza ndani yake. Ndiyo maana alisema kwamba, “uzuri wa ngozi, tumboni uozo.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana sura nzuri lakini matendo yake ni maovu, katika maisha yake. Mtu huyo, hujionesha kwa nje kuwa ni mzuri, lakini hufikiria mawazo mabaya katika moyo wake, kwa sababu ya matendo yake hayo maovu. Yeye hugombanisha watu walioko kwenye familia yake, kwa sababu ya matendo yake hayo maovu, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na lile embe lililoonekana zuri kwa nje, lakini ndani yake lilikuwa limeoza, kwa sababu naye ana sura nzuri, lakini matendo yake ni maovu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “uzuri wa ngozi, tumboni uozo.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha mwenendo wa kutenda maovu, kwa kutenda mema, ili waweze kuishi kwa amani, maishani mwao.

Mathayo 7:15-17.

Luka 6:43-45.

Mathayo 23:27-28.

ENGLISH: BEAUTY OF THE SKIN, ROT IN THE STOMACH.

This proverb looks at the beauty which is outside of something and an ugliness of an inside of it. There was a man who saw a mango that was so beautiful that he decided to pick it to eat because of its external beauty. When he peeled it, he realized that it was rotten inside. That is why he said that, “beauty of the skin, rot in the stomach.”

This proverb is related to a person who has a good appearance but his actions are evil in his life. Such person shows himself to be good on the outside, but thinks evil thoughts in his heart, because of his wicked deeds. He quarrels the people in his family, because of his evil deeds, in his life.

This person is like a mango that looked good on the outside, but inside it was rotten, because he also shows a good face, but his actions are evil, in his life. That is why people tell him that, “beauty of the skin, rot in the stomach.”

This proverb imparts in people an idea of stopping doing evil by doing good, so that they can peacefully live with their societal members in lives.

Matthew 7:15-17.

Luke 6:43-45.

Matthew 23:27-28.

mango-1218147__480

1178. NULU UGADIMA UGUTYUJA.

Ulusumo lunulo, lunhoyelile munhu uyo ugatyuja umulinti ugugwa hasi. Umunhu ng’wunuyo, aliolinha umulinti lya minyembe kugiki atone minyembe ya gulya. Ohayimanile otyuja ugwa hasi aliyo oliodima chiza. Hunagwene agayonmba giki, “nulu ugadima ugutyuja.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ohubhaga bho gwenhelejiwa na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, alintungilija aliyo lulu agahubhiyagwa na bhiye abho bhali na nhungwa ja bhubhi kunguno agayelaga nabho, umubhutumami milimo yakwe yiniyo. Uweyi agapandikaga mamihayo gagwenhelejiwa na bhiye bhenabho abha miito gabhubhi, kunguno ya gwikala nabho, umubhutumami bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agatyuja ugwa hasi aliyo oliodima, kunguno nuweyi alintungilija aliyo agahubhaga bho gwenhelejiwa na bhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “nulu ugadima ugutyuja.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gwilalanhana na bhanhu abho, bhagatumamaga milimo yabho kugiki bhadizuhubhibhiwa nabho, umuwikaji bho bhutungilija bhobho bhunubho.

Mwanzo 3:1-7.

KISWAHILI: HATA UKISHIKA UTATELEZA.

Methali hiyo, humuongelea mtu aliyekuwa ameshikilia kwenye mti akateleza na kuanguka chini. Mtu huyo, alipanda kwenye mti wa miembe ili achume maembe ya kula. Kwa bahati mbaya aliteleza akaanguka chini, pamoja na kwamba alikuwa ameshikilia vizuri. Ndiyo maana alisema kwamba, “hata ukishika utateleza.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukosea kwa kusababishwa na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, ni mwanamifu ambaye hukosea kwa kusababishwa na wenzake wenye mtendo maovu kwa sababu ya kutembea nao, katika kazi zake. Yeye hupata matatizo ya kusababishwa na wenzake hao wenye matendo maovu, kwa sababu ya kufanya kazi pamoja nao, katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa ameshika kwenye mti akateleza na kuanguka chini, kwa sababu naye ni mwaminifu, ambaye hukosea kwa kusababishwa na wenzake ambao wana matendo maovu, katika utekelezaji wa majukumu yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “hata ukishika utateleza.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kujilinda na watu wanaofanya kazi pamoja nao, ili wasikoseswe na wao, katika maisha yao hao ya uaminifu.

Mwanzo 3:1-7.

ENGLISH: EVEN IF YOU HOLD ON YOU WILL SLIP.

The overhead proverb speaks of a man who was holding on to a tree who slipped and fell down. This man climbed a mango tree in order to pick mangoes to eat. Unfortunately he slipped and fell to the ground, even though he was holding on well. That is why he said that, “even if you hold on, you will slip.”

This proverb is equated to a person who makes a mistake because of his nobles, in his life. Such person is a miscreant who errs because of his colleagues who do evil because of being with them, in his work. He gets problems which are caused by those colleagues who have evil deeds, because of working with them, in carrying out of his duties.

This person is similar to the one who was holding on to a tree who slipped and fell down, because he is also honest, who errs because of his colleagues who have wicked deeds, in the enactment of his duties. That is why he says that, “even if you hold on, you will slip.”

This proverb teaches people on how to be careful enough to protect themselves and the people who work with them, so that they are not wronged by them, in their honest lives.

Genesis 3:1-7.

mango-5326504__480