Author: Sukuma legacy

1025. ULU UJILE BULU ULU USHOKILE SELE.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile higulya ya bhudahi bho minzi bho bhakima. Abhakima ulu bhajile kumongo gujudaha minzi, b’agatuulaga jiseme ja gudahila aminzi genayo umundobho jabho. Ijiseme jinijo jigajaga jitulanya ni ndob’o jalila ‘gudulu gudula’ aliyo ulu bhashokile jigabhiza sele, kunguno jigab’izaga muminzi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ulu ujile bulu ulu ushokile sele.”

Akahayile kenako, kagalenijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga gutumama milimo yakwe, mpaga opandika sabho ja gutumila bho molele, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agazunyaga guleka tulo jakwe bho gwipuna diyu gete kunguno ya bhukamu bho gutumama milimo mpaga opandika sabho ya guyulya apolile, umukaya yakwe yiniyo. Uweyi agasab’aga majikolo mingi noyi, kunguno ya gulitumila chiza ilikanza lwakwe lya milimo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhadayi bha minzi abho bhagaja kumongo na jisema jilidulanya umundobho, ijo jigikala sele aho bhashokile, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe bho bhukamu bhutale na nguzu ningi, mpaka opandika sabho ningi ja gutumamila, umukikajile kakwe.  Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ulu ujile bulu ulu ushokile sele.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho chiza mpaga bhandike sabho ningi, kugiki bhadule gujilanhana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mithali 20:5.

Yohana 4:7.

Yohana 4:10-15.

Mithali 14:23.

Mithali 21:5.

Mithali 24:27.

KISWAHLI: UNAPOENDA KELELE UNAPORUDI KIMYA.

Chanzo cha msemo huo cha husu uchotaji wa maji wa wanawake. Wanawake wanapoenda kuchota maji mtoni, huweka vyombo vya kuchotea maji ndani ya ndoo zao. Vyombo hivyo, hupiga kelele ndani ya ndoo hizo na kulia ‘gudulu gudulu’ kwa sababu ya kugongana na ndoo wakati wa kwenda. Lakini wakati wa kurudi huwa viko kimya kwa sababu ya vyombo hivyo kuwa ndani ya maji. Ndiyo maana watu husema kwamba, “unapoenda kelele unaporudi kimya.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kufanya kazi zake mpaka anafanikiwa kupata mavuno mengi ambayo huyatumia kwa amani, katika maisha yake. Mtu huyo, hukubali kuacha usingizi wake kwa kuamuka asubuhi na mapema kwa sababu ya bidii yake hiyo, ya kufanya kazi mpaka anafakiwa kupata mali za kutumia akiwa ametulia, nyumbani kwake. Yeye hutajirika kwa kupata mali nyingi sana, kwa sababu ya kuutumia vizuri muda wake huo wa kazi, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na wachotaji wa maji walioenda mtoni na vyombo vyao vikipiga kelele wakarudi vikiwa kimya, kwa sababu naye hujibidisha kufanya kazi kwa nguvu, na bidii kubwa, mpaga anafanikiwa kupata mali nyingi za kutumia katika familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “unapoenda kelele unaporudi kimya.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa nguvu, ili waweze kupata mali nyingi za kutumia katika familia zao, maishani mwao.

Mithali 20:5.

Yohana 4:7.

Yohana 4:10-15.

Mithali 14:23.

Mithali 21:5.

Mithali 24:27.

ENGLISH: WHEN YOU GO YOU MAKE NOISE BUT YOU RETURN SILENTLY.

The cradle of the above saying is about women’s water fetching. When the women go to fetch water from the river, they put water fetching vessels in their buckets. These vessels, in turn, scream into the buckets and make noise ‘gudulu gudulu’ because of colliding with the bucket on the way. But when they return, they are silent because these bowls are in the water. That is why people say, “when you go you make noise but you return silently.”

This saying is likened to a man who works hard enough to earn a living until he is able to reap a bountiful harvest that he peacefully uses in his lifetime. This man, agrees to give up his sleep by waking up early in the morning because of his diligence, to work until he has to get the property for using while he is calm, at his home. He becomes rich because of the good use of his time in his daily life.

This man resembles the water fetchers who went to the river with their vessels shouting and came back in silence, because he also strives to work hard, with great diligence to the point of managing to get a lot of resources for using in his family. That is why people say to him that, “when you go you make noise but you return silently.”

This saying imparts in people a clue on how to work hard, so that they can earn a lot of money for spending in their family lives.

Proverbs 20: 5

John 4: 7.

John 4: 10-15.

Proverbs 14:23.

Proverbs 21: 5.

Proverbs 24:27.

madagascar-1

1024. KALAGU –  KIZE. BHANA BHA NG’WISE B’ISHIGANYA UGUSIMINZA – MAZWI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kasiminzile ka ng’wa munhu. Umunhu ulu alisiminza, amagulu gadajilanijaga lihamo kunguno gagishiganyaga bho gumo gumo. Kuyiniyo lulu, amazwi galikihamo na magulu umo gagishiganijaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu bha hakaya iyo bhagishib’ilaga uguyomba, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagilekelaga uguyomba bho gundegeleka bhuli ng’wene mpaga omala uguyomba kunguno bhali nilange lya gwikuja bhuli ng’wene. Abhoyi bhagikalaga bhitogilwe bho gwiyambilija chiza bhuli ng’wene ulubhitana abhiye, kunguno ya wiyigwi bhobho bhunubho, umuwikaji bhobo.

Abhanhu bhanebho, bhagikolaga na mazwi ayo gagishib’ilaga ugusiminza, kunguno nabhoyi bhagishib’ilaga uguyomba, mpaga omala ung’wene na oyomba nu ungi, aha kaya yabho yiniyo. Hunagwene bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gub’iza nikujo lya gwidegeleka chiza umumahoya gabho bho gwilekela oyomba uumo mpaga omala, na oyomba nuungi lulu, kugiki bhadule gwikala bho mholele chiza, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

WATOTO WA KWETU HUBISHANA KUTEMBEA – MAGOTI.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia utembeaji wa mtu. Mtu anapotembea miguu yake huwa haiendi kwa pamoja kwa sababu hupishana mmoja mmoja. Kwa hiyo basi, magoti nayo yako pamoja na miguu inavyotembea. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wa kwenye familia ile ambayo watu wake huwa wanasikilizana katika maongezi yao kwa kupeana zamu, katika maisha yao. Watu hao, huachiana zamu ya kuongea kwa kumsikiliza kila mmoja wao mpaka anamaliza vizuri kuongea ndipo na mwingine anaanza, kwa sababu ya heshima walionayo kwa kila mmoja wao. Wao huishi katika upendo wa kusaidiana vizuri kila mmoja anapowahitaji wenzake, kwa sababu ya uelewano wao huo mzuri, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na yale magoti ambayo hupeana zamu katika kutembea, kwa sababu nao huachiana zamu ya kuongea mpaka mmoja wao anamaliza ndipo na mwingine anaanza kuongea, kwenye familia yao hiyo. Ndiyo maana watu hao huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na heshima ya kusikilizana vizuri katika maongezi yao kwa kuachiana kila mmoja anaongea mpaka anamaliza ndipo anaanza na mwingine kuongea, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani, maishani mwao.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

OUR RELATIVES CHILDREN ARGUE ABOUT WALKING – KNEES.

The source of the above riddle looks at a person’s walking. When a person walks his legs do not move together because they overlap one by one. Therefore, the knees are also with the legs as they move. That is why people say to one another that, “Our relatives children argue about walking – knees.”

This riddle is compared to the members of a family whose people listen to each other in their conversations in their lives. These people take turns talking to each other until they have finished talking and then the other can start doing so, because of the respect they have for each other. They live in love of helping each other well when they are in need, because of their good understanding in their lives.

These people are like the knees that take turns walking, because they also take turns talking until one of them finishes and the other can start talking to their family members. That is why these people tell each other that, “Our relatives children argue about walking – knees.”

This paradox teaches people on how to have a good sense of respect on one another in their conversations by letting each other talk until one finishes and then they can start talking to each other, so that they can live well and peacefully in their lives.

Acts 17:25.

1 Peter 2: 4.

1023. KALAGU – KIZE. IKAYA YISE ILELO BHO GUNUNG’HYA – MHANDE.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ihoyelile higulya ya bhuli bho mhande. Imhande indoto ulu juzugwa abhanhu bhadatondolaga akagula gajo kunguno bhagazigaza bhegeleja haho nomo bhakanza yafuma imhande balya giti balinung’hya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “ikaya yise ilelo bho gunung’hya – mhande.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na ng’wigwano go wiza aha kaya yabho. Abhanhu bhanebho, bhagilomelaga mihayo ya gwiyambilija gutumama milimo yabho bhizunilija chiza, kunguno ya ng’wigwano gobho gunuyo, umukikalile kabho. Abhoyi bhagaponaga jiliwa noyi umubhutumami bho milimo yabho yiniyo, kunguno ya gujilanija chiza, umuwikaji bhobho bhunubho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga ni mhande ijo bhajilyaga abhanhu bho gwegeleja hanomo bhakanda yafuma guti bhalinunghya, kunguno bhagatumamaga milimo yabho bho gujilanija na ng’wigwano chiza, mpaga bhapandika sabho ningi a hakaya yabho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayombaga giki, “ikaya yise ilelo bho gunung’hya – mhande.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gujilanija chiza umuwigulambija bho gutumama milimo yabho, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila chiza umu kaya jabho.

Matendo ya mitume 10:34-36.

Luka 16:9-10.

Matendo ya mitume 2:42-46.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

FAMILIA YETU LEO WA KUNUSA – NJUKU MAWE.

Chanzo cha kitendawili hicho huongelea juu ya ulaji wa njugu mawe. Njugu mawe hizo, zikipikwa wakati zikiwa mbichi, watu huwa hawamenyi maganda yake, kwa sababu huwa wanasogeza kwenye mdomo na kuminya ambapo njugu mawe hutoka yenyewe kwa kurukia mdomoni na kuila kama wananusa hivi. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “familia yetu leo wa kunusa – njugu mawe.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale walio na uelewano kwenye familia zao. Watu hao, hupanga mipango yao ya kusaidiana katika kufanya kazi kwa kuelewana vizuri, kwa sababu ya uelewano wao huo, katika maisha yao. Wao hupata mavuno mengi katika kazi zao hizo, kwa sababu ya kuendana kwao huko vizuri, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na zile njuku mawe walizokuwa wakizila wale watu kwa kusogeza mdomoni na kuminya halafu inarudia mdomoni wanakula kama wananusa hivi, kwa sababu nao huyatekeleza majukumu yao kwa uelewano mzuri, mpaka wanafanikiwa kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza familia zao. Ndiyo maana wao huwaambia watu kwamba, “familia yetu leo wa kunusa – njugu mawe.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uelewano wa kuendana vizuri katika juhudi zao za kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza vizuri familia zao.

Matendo ya mitume 10:34-36.

Luka 16:9-10.

Matendo ya mitume 2:42-46.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

AT OUR HOME TODAY WE WILL EAT SOMETHING SMELLY – BAMBARA NUTS.

The foundation of the overhead riddle talks about eating of Bambara nuts. If these Bambara nuts are cooked when they are raw, people do not peel their pods, because they tend to bring near to their mouth and squeeze where the Bambara nuts come out by themselves by jumping in the mouth and eating them as if they smell like this. That is why people say to one another that, “at our home today we will eat something smelly – Bambara nuts.”

This riddle is compared to people who have harmony in their families. These people, in turn, make plans to help each other enough to work in harmony with each other, because of their mutual understanding, in their lives. They reap a bountiful harvest in their labors, because of their good arrangement in their lifetime.

These people resemble the Bambara nuts that the people used to eat by bringing them near to their mouths and squeezing enough to let them jump into their mouths, because they also carry out their duties in a good way, until they manage to get enough wealth to take care of their families. That is why they tell people that, “at our home today we will eat something smelly – Bambara nuts.”

This riddle imparts in people an idea on how to have a good sense of belonging in their efforts to fulfill their responsibilities, so that they can have enough wealth to take good care of their families.

Acts 10: 34-36.

Luke 16: 9-10.

Acts 2: 42-46.

hazelnut-2284654__480

nuts-762803__480

peanut-6757556__480

1022. KALAGU – KIZE. GWA KAGAKULAGULAGA – KAGOKO.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kikalile ka ngoko. Ingoko yiniyo igigalaga yukulagula umugwicholela ijiliwa jayo, umukikalile kayo kenako. Iyoyi igajitagulaga hasi ijiliwa nulu jigikala jitulile mujisema, kunguno ya wigulambija bho gwicholela jagulya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “gwa kagakulagaulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga gwicholela sabho bho gutumama milimo yakwe bhuli lushigu, umukitakile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wigulambija gutumama milimo yakwe bho gwanguha uguyandya uguitumama bhuli lushigu, kunguno ya gutogwa guyibheja chiza ikaya yakwe yiniyo. Uweyi agapandikaga sabho ningi umumilimo yakwe kunguno ya wigulambija bhokwe bhunubho ubho gutumama milimo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nkogo iyo igikalaga yuchola jiliwa bhuli lushigu, kunguno nuweyi agigulambijaga kutumama milimo yakwe chiza, mpaga opandika sabho ningi, umubhutumami bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gwa kagakulagulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bhuli lushigu kugiki bhadule kupandima sabho jagijilanhanila chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

2Wathesalonike 3:10.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KILA SIKU HUPEKUAPEKUA – KUKU.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia maisha ya kuku. Kuku huyo, hupekuapekua kila siku katika kujitafutia chakula chake, katika maisha yake hayo. Yeye hukimwaga chini hata chakula kile kilichomo kwenye chombo kizuri kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kutafuta chakula. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kutafuta mali kwa kufanya kazi zake kila siku, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa akijibidisha kufanya kazi zake kwa kuwahi kwenda kazini kila wakati kwa sababu ya kutaka kuitunza vizuri familia yake. Yeye hufanikiwa kupata mali nyingi katika kazi zake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kuyatekeleza vizuri majukumu yake hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule kuku aliyejibisha kutafuta chakula kila siku, kwa sababu naye hujibidisha kufanya kazi vizuri, mpaka anafanikiwa kupata mali nyingi za kutosha kuitunza vizuri familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kila siku ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza vizuri familia zao, maishani mwao.

2Wathesalonike 3:10.

ENGLISH: I HAVE RIDDLE – LET IT COME.

IT PECKS EVERY DAY – CHICKEN.

The basis of the above riddle looks at the life of the chicken. The chicken search every day for their food in their lives. They even pour out the food that is in the fine container because of their zeal for the food. That is why people say that, “It pecks every day – chicken.”

This riddle is compared to a man who strives to seek wealth by doing his daily work, in his life. This person, in turn, strives to do his job by going to work all the time because he wants to take good care of his family. He succeeds in gaining wealth in his work because of his diligence in fulfilling his responsibilities in his life.

This man is like the hen that had to work hard to get food every day, because he also strives to work hard, until he manages to get enough wealth to take good care of his family. That is why people say to him that, “It pecks every day – chicken.”

This riddle teaches people on how to work hard every day so that they can earn enough money to take good care of their families in their lives.

2 Thessalonians 3:10.

chicken--

1021. IGUNILA IDUHU LIDIMILAGA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya bhudamu bho ligunila ugwimila ilo lidina ginhu umugati yalyo. Iligunila linilo lidadulile ugwimila kunguno lina jikolo ijagulyimilicha umugati yalyo. Ilyoyi ligagwaga hasi duhu ulu munhu ulyimilicha. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “igunila iduhu lidimilaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina masala magehu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga wambilijiwa bhuli makanza na bhanhu abho agikalaga nabho kunguno adidulile ugwimilila bho gwilanhana ng’winikili, umuwikaji bhokwe. Uweyi agakoyaga noyi agwigala chiza ulu ugayiwa uogung’wambilija, aho agikilaga.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga niligunila ilo lidina ginhu umo ligadumilaga ugwimila, kunguno nuweyi adadulile ugwimila ubho ing’wene, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “igunila iduhu lidimilaga.”

Ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kubhambilija abhanhu abho bhali na masala magehu, kugiki bhadule gubhalanhana chiza, umuwikaji bhobho.

1Petro 1:4:7-11.

1Wakorintho 13:1-5.

KISWAHILI: GUNIA TUPU HALISIMAMI.

Methali hiyo, huongelea juu ya ugumu wa junia kusimama lililotupu. Gunia hilo haliwezi kusimama kwa sababu halina kitu cha kuliwezesha kufanya hivyo ndani yake. Lenyewe huanguka chini tu endapa mtu atajaribu kulisimamisha kwa sababu ya ulaini wake huo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “gunia tupu halisimami.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana akili pungufu, katika maisha yake. Mtu huyo, hutegemea kupata msaada kila wakati kutoka kwa wale anaoishi nao, kwa sababu hajiwezi kujitegemea mwenyewe kwa kusimama peke yakwe, maishani mwake. Yeye huhangaika mno akikosa mtu wa kumsaidia, pale anapoishi.

Mtu huyo, hufanana na lile gunia lisilokuwa na kitu lisivyoweza kusimama, kwa sababu naye hawezi kusimama pele yake bila kuwa na mtu wa kumsaidia, katika maisha yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, “gunia tupu halisimami.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na moyo wa kuwasaidia watu wao waliopungukia akili au wale waliojiweza, ili waweze kuwatunza vizuri, maisha ni mwao.

1Petro 1:4:7-11.

1Wakorintho 13:1-5.

ENGLISH: “AN EMPTY SACK CANNOT STAND.”

The overhead proverb speaks about a difficulty of an empty sack to stand. Such sack cannot stand because it has nothing in it which can hold it enough to do so. It just falls to the ground if one tries to make it stand because of its softness. That is why people say that, “An empty sack cannot stand.”

This proverb is compared to a man who has a limited mind, in his life. He relies on constant support from those who live around him, because he is not able to stand alone on his own two feet. He is very worried about not having anyone to help him, where he lives.

This man is like the empty sack that has nothing in it that can make it stand, because he also not enable to live alone without anyone to help him, in his life. That is why people say that, “An empty sack cannot stand.”

This proverb teaches people about having a temperament of helping their mentally retarded people or the able-bodied, so that they can take good care of them, life is theirs.

1 Peter 1: 4: 7-11.

1 Corinthians 13: 1-5.

bag-1693897__480