1024. KALAGU –  KIZE. BHANA BHA NG’WISE B’ISHIGANYA UGUSIMINZA – MAZWI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kasiminzile ka ng’wa munhu. Umunhu ulu alisiminza, amagulu gadajilanijaga lihamo kunguno gagishiganyaga bho gumo gumo. Kuyiniyo lulu, amazwi galikihamo na magulu umo gagishiganijaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu bha hakaya iyo bhagishib’ilaga uguyomba, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagilekelaga uguyomba bho gundegeleka bhuli ng’wene mpaga omala uguyomba kunguno bhali nilange lya gwikuja bhuli ng’wene. Abhoyi bhagikalaga bhitogilwe bho gwiyambilija chiza bhuli ng’wene ulubhitana abhiye, kunguno ya wiyigwi bhobho bhunubho, umuwikaji bhobo.

Abhanhu bhanebho, bhagikolaga na mazwi ayo gagishib’ilaga ugusiminza, kunguno nabhoyi bhagishib’ilaga uguyomba, mpaga omala ung’wene na oyomba nu ungi, aha kaya yabho yiniyo. Hunagwene bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gub’iza nikujo lya gwidegeleka chiza umumahoya gabho bho gwilekela oyomba uumo mpaga omala, na oyomba nuungi lulu, kugiki bhadule gwikala bho mholele chiza, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

WATOTO WA KWETU HUBISHANA KUTEMBEA – MAGOTI.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia utembeaji wa mtu. Mtu anapotembea miguu yake huwa haiendi kwa pamoja kwa sababu hupishana mmoja mmoja. Kwa hiyo basi, magoti nayo yako pamoja na miguu inavyotembea. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wa kwenye familia ile ambayo watu wake huwa wanasikilizana katika maongezi yao kwa kupeana zamu, katika maisha yao. Watu hao, huachiana zamu ya kuongea kwa kumsikiliza kila mmoja wao mpaka anamaliza vizuri kuongea ndipo na mwingine anaanza, kwa sababu ya heshima walionayo kwa kila mmoja wao. Wao huishi katika upendo wa kusaidiana vizuri kila mmoja anapowahitaji wenzake, kwa sababu ya uelewano wao huo mzuri, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na yale magoti ambayo hupeana zamu katika kutembea, kwa sababu nao huachiana zamu ya kuongea mpaka mmoja wao anamaliza ndipo na mwingine anaanza kuongea, kwenye familia yao hiyo. Ndiyo maana watu hao huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na heshima ya kusikilizana vizuri katika maongezi yao kwa kuachiana kila mmoja anaongea mpaka anamaliza ndipo anaanza na mwingine kuongea, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani, maishani mwao.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.