1022. KALAGU – KIZE. GWA KAGAKULAGULAGA – KAGOKO.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kikalile ka ngoko. Ingoko yiniyo igigalaga yukulagula umugwicholela ijiliwa jayo, umukikalile kayo kenako. Iyoyi igajitagulaga hasi ijiliwa nulu jigikala jitulile mujisema, kunguno ya wigulambija bho gwicholela jagulya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “gwa kagakulagaulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga gwicholela sabho bho gutumama milimo yakwe bhuli lushigu, umukitakile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wigulambija gutumama milimo yakwe bho gwanguha uguyandya uguitumama bhuli lushigu, kunguno ya gutogwa guyibheja chiza ikaya yakwe yiniyo. Uweyi agapandikaga sabho ningi umumilimo yakwe kunguno ya wigulambija bhokwe bhunubho ubho gutumama milimo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nkogo iyo igikalaga yuchola jiliwa bhuli lushigu, kunguno nuweyi agigulambijaga kutumama milimo yakwe chiza, mpaga opandika sabho ningi, umubhutumami bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gwa kagakulagulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bhuli lushigu kugiki bhadule kupandima sabho jagijilanhanila chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

2Wathesalonike 3:10.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KILA SIKU HUPEKUAPEKUA – KUKU.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia maisha ya kuku. Kuku huyo, hupekuapekua kila siku katika kujitafutia chakula chake, katika maisha yake hayo. Yeye hukimwaga chini hata chakula kile kilichomo kwenye chombo kizuri kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kutafuta chakula. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kutafuta mali kwa kufanya kazi zake kila siku, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa akijibidisha kufanya kazi zake kwa kuwahi kwenda kazini kila wakati kwa sababu ya kutaka kuitunza vizuri familia yake. Yeye hufanikiwa kupata mali nyingi katika kazi zake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kuyatekeleza vizuri majukumu yake hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule kuku aliyejibisha kutafuta chakula kila siku, kwa sababu naye hujibidisha kufanya kazi vizuri, mpaka anafanikiwa kupata mali nyingi za kutosha kuitunza vizuri familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kila siku ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza vizuri familia zao, maishani mwao.

2Wathesalonike 3:10.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.