1083. BENA: IMBWA NDAVILA PASI YE NYIDZI.

KISWAHILI: MBWA ANAYEANGALIA CHINI NDIYE MWIZI.

Methali hiyo, huangalia maisha ya mbwa aliyekuwa mwizi. Mbwa huyo, alikuwa akiiba nyama na kula mara kwa mara bila ya wamiliki wake kufahamu kuwa ni yeye kwa sababu ya kujificha kwake kwa kuangalia chini. Mbwa huyo alikuwa akiangalia chini ili kunesha hali ya kuficha kosa la kuiba nyama hizo.

Wamiliki wake walifanya utafiki uliowezesha kumtamgua aliyekuwa akiiba nyama zao. Utafiti huo, ulimkamata mbwa huyo baada ya kumuona akiziiba nyama hizo. Ndiyo maana walisema kwamba, “mbwa anayeangalia chini ndiye mwizi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huonekana kuwa ni mwema kwa nje lakini kwa ndani ni muovu, katika maisha yake. Mtu huyo, hutenda matendo yake kwa lengo la kujionesha kwa nje tu kuwa ni mwema kwa sababu ya kutaka kujificha ili uovu wake usijulikane kwa watu. Yeye hugundulika tabia yake hiyo mbaya baada ya kukaa naye, ndipo unafiti wake hujionesha wazi baada yeye kujisahau, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule mbwa aliyekuwa akiiba nyama na kujificha kwa kuangalia chini, kwa sababu naye huonekana kwa nje kuwa ni mtu mwema kumbe kwa ndani ni muovu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mbwa anayeangalia chini ndiye mwizi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya kujionesha kwa nje kuwa wema kwa kuacha kutenda maovu, na badala yake watende mema ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, katika familia zao.

Mathayo 23:28 “Vivyo hivyo, ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.”

Luka 6:44 “Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba wala zabibu kwenye michongoma.”

1samweli 16:7 “Lakini Bwana akamwambia Samweli usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake, kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama wanadamu waangaliavyo, bali Bwana huutazama moyo.”

ENGLISH: A DOG THAT LOOKS DOWN IS THE THIEF.

The overhead proverb looks at the life of a dog that was a thief. Such dog used to steal meat and eat it frequently without its owners realizing that it was him because of his hiding by looking down. Such dog was looking down in order to hide the crime of stealing the meat.

Its owners made a research that enabled them to identify the one who was stealing their meat. Such research, arrested the dog after seeing him stealing the meat. That is why they said that, “a dog that looks down is the thief.”

This proverb is compared to the person who appears to be good on the outside but is evil on the inside, in his life. Such person does his actions with the aim of showing himself to be good on the outside because he wants to hide himself so that his evil will not be known by people. People discover his bad behavior after staying with him, then his selfishness shows itself clearly after he forgets himself, in his life.

This person is like the dog that was stealing meat and hiding by looking down, because he also looks like a good person on the outside but is evil on the inside, in his life. That is why people tell him that, “a dog that looks down is the thief.”

This proverb instills in people an idea of abandoning a habit of showing themselves to be good by stopping doing evil, and instead they should do well so that they can live in peace with their nobles, in their families.

Matthew 23:28 “In the same way, you also, on the outside you appear to be righteous, but on the inside you are full of hypocrisy and rebellion.”

Luke 6:44 “Every tree is known by its fruit.” Because people don’t pick figs on thorns or grapes on brambles.”

1 Samuel 16:7 “But the Lord said to Samuel, don’t look at his face, nor at the height of his stature, because I have rejected him. The Lord does not look as men look, but the Lord looks at the heart.”

dog-1418330__480

puppy-4240180__480

german-shepherd-1970026__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.