1042. UNKONO UGUMO GUDALELAGA NG’WANA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya bhuleji bho ngw’ana. Ubhuleji bhunubho bhuli bho bhabyaji pye abhose kunguno bhuli ng’wene alina solobho nhale ukubhukuji bho ng’wana.

Aho kale olihoyi nkima umo uyo oliangegelile ung’wana okwe bho nduhu ugwiyambilija na bhiye ugunhela chiza iki oliwiisanije weyi duhu. Ung’wana okwe ng’wunuyo agabhiza na nhungwa ja bhulambu bhoguyulema ugutung’wa na bhangi kunguno ya nhinda jakwe jinijo.

Ung’wana ng’wunuyo agayubeha njemu, guikenya na bhiye, na guhaya gumulag uninao okwe uyo mpaga nose agang’wenheleja kupandika mamihayo ga gulipa sabho ninghi kunguno ya bhugulu bho ng’wana okwe ng’wunuyo.

Lushugu lumo, abhanhu pye nu Ntemi bhagibhilinga ahakaya ya nina o ng’wana ng’wunuyo kugiki bhadule kumuja ijenheleja ja bhugulu bho ng’wana okwe ng’wunuyo.

Unina o ng’wana ng’wunuyo, agabhalomela umo onhelela bhung’wene chiniko niyo bho gungegela ung’wina ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wina umyaji ng’wunuyo giki, “unkono ugumo gudalelaga ng’wana.”

Unina o ng’wana ng’wunuyo agazunya ugwiyambilija na bhana nzengo ugunhela chiza ung’wana okwe ng’wunuyo mpaga nose ubhiza na nhung’wa ja wiza kunguno ya wiyambilija bho bhanhu bhingi ugunhela chiza chiniko.

KISWAHILI: MKONO MMOJA HAULEI MTOTO.

Methali hii inaongelea juu ya malezi ya mtoto yanayohitaji ushirikiano wa wazazi wote wawili. Wazazi hao hutakiwa kushirikiana pia na jumuiya ndogondogo za Kikristo katika kuwalea vizuri watoto wao.

Hapo zamani alikuwepo mama mmoja aliyekuwa akimdekeza mtoto wake kwa kutowaruhusu wengine kumsaidia katika kumlea, zaidi yake yeye mwenyewe. Mtoto yule alikuwa na tabia mbaya sana na mpaka akawa anavuta bangi, kupiga watu na kutaka kumuua mzazi wake huyo.

Mzazi huyo wa mtoto alipiga yowe watu wakaja pamoja na mfalme wa eneo hilo wakitaka kufahamu chanzo cha kuharibika kwa mtoto huyo. Mama yule alieleza jinsi alivyo mdekeza mtoto wake huyo. Ndipo watu wakamwambia kwamba, “mkono mmoja haulei mtoto.”

Mama wa mtoto huyo aliwaomba watu na jumuiya ndogo ndogo kikristo washirikiane kumlea mtoto huyo. Walipofanya hivyo, mtoto huyo aliacha tabia mbaya akawa na tabia njema ya kuwatendea mema wenzake.

Alibatizwa na akashirikiana na jumuiya ndogo ndogo katika kuwalea watoto wa familia zilizoko ndani ya Jumuiya zao hizo za kikristo. Ndiyo maana alianza kuwaambia watu kwamba, “mkono mmoja haulei mtoto.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa wazazi wale ambao huwa hawasaidiani vizuri kuwalea watoto wao mpaka wanapata matatizo ndipo wanaanza kushirikiana kuifanya kazi hiyo. Wazazi hao, hutegeana kwa kumwachia mmoja kati yao, mpaka watoto wao wanawaletea matatizo yatokanayo na tabia mbaya ndipo wanaungana kuwalea hao kwa pamoja, maishani mwao. Ushirikiano huo wa kuwalea watoto wao, huwajengea tabia njema ya kuishi kwa upendo wa kuwasaidia vizuri wenzao, katika maisha yao.

Wazazi hao, hufanana na yule mzazi aliyemdekeza mtoto wake, mpaga akawa na tabia mbaya iliyomletea matatizo ndipo akaanza kusaidiana na wenzake katika kumlea vizuri mtoto huyo, kwa sababu nao hutegeana katika kuwalea watoto wao, mpaga wanapata matatizo ndipo wanaanza kushirikiana na wenzao, katika kuwalea kwa pamoja watoto hao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “mkono mmoja haulei mtoto.”

Methali hiyo, hufundisha wazazi juu ya kuwa na ushirikiano wa kuwalea watoto wao kwa pamoja ndani ya jumuiya zao ndogo ndogo za Kikristo, ili waweze kukua wakiwa na maadili mema ya kusaidiana na wenzao, maishani mwao.

 

Mathayo 19:14

Luka 2:26-27

Luka 2:48.

ENGLISH: ONE HAND DOES NOT RAISE A CHILD.

This proverb talks about the upbringing of a child that requires the cooperation of both parents. Those parents are also required to cooperate with small Christian communities in raising their children well.

Once upon a time there was a mother who was admonishing her child for not allowing others to help her in raising her, other than herself. Such had a very bad behavior until he was smoking marijuana, hitting people and wanting to kill his mother.

The child’s parent screamed and people came with the king of that area wanting to know the cause of the child’s deformity. The mother explained how she raised alone by not warning her child. Then the people told her that, “one hand does not raise a child.”

The child’s mother asked people and small Christian communities to work together enough to raise the child. When they did that, the child gave up his bad behavior and started doing well to his peers.

He was baptized and collaborated nicely with small communities in raising the children of families in their Christian communities. That’s why he started telling people that, “one hand does not raise a child.”

This proverb is compared to those parents who do not help each other properly enough to raise their children until they have problems and then they start working together in doing such work. The parents do not participate together in raising their children by not collaborating well, until their children bring them problems due to bad behavior and then they unite to raise them together, in their lives. This partnership for raising their children, builds a good habit of living with the love of helping their peers well, in their lives.

Those parents are similar to the parent who scolded his child, until when he had a bad behavior that caused her problems and then she started to help another with her colleagues in raising the child well, because they also do not work together as a team in raising their children, until they get problems then they start cooperating with their peers, in raising them by working together enough to raise well their children. That is why people tell them that, “one hand does not raise a child.”

The proverb teaches parents on how to cooperate in raising their children together in their small Christian communities, so that they can grow up with good values enough ​​to help each other, in their lives.

Mt 19:14.

Luke 2:26-27.

Luke 2:48.

happy--

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.