1019. NTEMI OGWA MU MAGULU.

Imbuki ya kahayile kenako yingilile kubhanhu abho bhali bhapona majiliwa mingi gete. Abhanhu bhenabho, bhagalima na gupandika jiliwa jingi gete ijo bhagayujipandikagila nose umumagulu gabho kunguno ya wingi bhojo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayuyomba giki, “Ntemi ogwa mumagulu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalimaga migunda mitale iyo agampandikilaga majiliwa mingi gete, umukikalile kakwe.  Umunhu ng’wunuyo, agikomejaga kulima bho gwipuna diyu bhuli lushigu ogalima migunda mitale ya jiliwa ja bhuli mbika, kunguno ya bhukamu bhokwe ubho gutumama milimo bhunubho. Uweyi agajikwijaga noyi isabho umubhulimi bhokwe bhunubho, kunguno ya witegeleja bhokwe, umukikalile kakwe kenako.

Isabho jakwe umunhu ng’wunuyo, jigikolaga nijiliwa ijo bhagajipandika abhalimu abho mpaga bhuyujipandagila bho magulu gabho, kunguno nijoyi jakwila mpaga uduma ugujimala ugujilwa umunhu ng’wunuyo kihamo ni kaya yakwe. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “Ntemi ogwa mumagulu.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bho bhukamu bhutale mpaga bhapandike sabho ningi, ja gudula gugamala makoye ga nzala, umukaya jabho.

Waroma 12:11.

Luka 9:62.

Ufunuo 2:10.

Wagalatia 6:7-9.

Mithali 16:26.

Mithali 14:23.

Mithali 12:4.

KISWAHILI: MFALME AMEANGUKA MIGUUNI.

Chanzo cha msemo huo, kilianzia kwa watu waliolima mashamba wakapata chakula kingi sana. Watu hao, walilima mashamba ya mazao mbalimbali ambayo yaliwapatia chakula kingi mpaga wakaanza kukikanyaga kwa miguu yao, kwa sababu ya wingi wake uliowazidi hivyo. Ndiyo maana watu hao walianza kusema kwamba, “mfalme ameanguka miguuni.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hulima mashamba makubwa ya mazao mbalimbali, na kupata chakula kingi, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kulima mazao ya aina mbalimbali kwenye mashamba yake hayo makubwa, ambayo humpatia chakula kingi cha kula na kusaza kwenye familia yake, kwa sababu ya bidii yake hiyo kufanya kazi. Yeye hukusanya mali nyingi sana katika kilimo chake hicho, kwa sababu ya umakini wake mkubwa katika kuyatekeleza vizuri majukumu yake, maishani mwake.

Mali ya mtu huyo, hufanana na chakula kingi walichokipata wale wakulima ambacho walishindwa kukimalima kukila mpaka wakaanza kukikanyaga kwa miguu yao, kwa sababu nazo zimekuwa nyingi sana, mpaka mtu huyo na familia yake, wakashindwa kuzimalima. Ndiyo maana watu hao walisema kwamba, “mfalme ameanguka miguuni.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa bidii kubwa mpaka wafanikiwe kupata mali nyingi, cha kuweza kuyamaliza matatizo ya njaa, katika familia zao.

Waroma 12:11.

Luka 9:62.

Ufunuo 2:10.

Wagalatia 6:7-9.

Mithali 16:26.

Mithali 14:23.

Mithali 12:4.

ENGLISH: THE KING HAS FALLEN ON HIS FEET.

The origin of the above saying started from the people who farmed enough to get a lot of food. They cultivated a variety of crops that provided them with plenty of food to point of starting to trample it underfoot, because of its excessive quantity. That is why the people began to say that, “the king has fallen on his feet.”

This saying is related to a man who cultivates a large farm of crops, and obtains plenty of food, throughout his life. This man, in turn, strives to cultivate a wide variety of crops on his large farm, which provides him with plenty of food to eat for his family, because of his hard working. He accumulates a great deal of wealth in his field, because of his great care in carrying out his duties, in his lifetime.

This man’s property is like the food that the farmers got which they could not finish to use it until they began to trample it with their feet, because he also got so abundant food that his his family could not finish to use it. That is why the people said that, “The king has fallen on his feet.”

This saying teaches people on how to work hard enough to succeed in acquiring more wealth for using in their families, so that they can end hunger problems in their families.

Romans 12:11

Luke 9:62

Revelation 2:10.

Galatians 6: 7-9

Proverbs 16:26

Proverbs 14:23

Proverbs 12: 4.

fruit-3247447__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.