1020. OB’ITYAGA NKOB’A.

Akahayile kenako, kahoyelile hugulya ya wisendeja bho kulinkima umo bho ng’wa munhu uyo oliatolile mhali. Umunhu ng’wunuyo oli na bhakima bhabhili abho agaduma uguigabhanya ukubhoyi kunguno agisendeja kuli nkima umo duhu, uungi unekanija. Hunagwene abhanhu bhagayuyomba giki “ob’ityaga nkob’a.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumama milimo mingi kuli kanza limo, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agandyaga gutumama milimo mingi iyo adayimalaga, kunguno ya gubhucha milimo mingi kuli kanza limo linilo, niyo alibhung’wene ubhuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga na makoye ga gugayiwa sabho aha ng’wakwe kunguno ya kuduma uguimala imilimo yakwe iyo agayaandyaga yiniyo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu ntoji o mhali uyo agisendeja kuli nkima umo duhu, uungi unekanija, kunguno nuweyi agandyaga kutumama milimo mingi mpaga oduma uguimala, umubhutumami bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ob’ityaga nkob’a.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kutola nkima umo duhu, na gutumama nimo gumo umubhutumami bhobho, kugiki bhadule gwikala chiza na kupandika sabho ningi, umuwikaji bhobho.

Mathayo 6:24.

Marko 10:11-12.

1Wakorintho 7:1-3.

KISWAHILI: AMEPITISHA MKANDA WA NGOZI.

Msemo huo, huongelea juu ya uegemeaji wa upande mmoja wa mtu aliyekuwa na mitala. Mtu huyo, alikuwa na wake wawili ambao alishindwa kujigawa katika kuwahudumia kwa sababu aliegemea kwa mke mmoja tu na kumtelekeza yule mwingine. Ndiyo maana watu walisema kwamba, “amepitisha mkanda wa ngozi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huanzisha kazi nyingi kwa wakati mmoja, katika kazi zake. Mtu huyo, huanzisha miradi mingi ambayo huwa hana uwezo wa kuitekeleza yote kwa wakati huyo mmoja na yuko peke yake, katika maisha yake. Yeye huishi katika matatizo ya kukosa mali kwenye familia yake, kwa sababu ya kushindwa kuimaliza miradi yake hiyo aliyoyianzisha, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeoa mitala akaegemea kwa mke mmoja na kumtelekeza yule mwingine, kwa sababu naye huanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja na kushindwa kuimaliza, katika utendaji wake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amepitisha mkanza wa ngozi.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na mke mmoja, na kutekeleza kwa umakini kazi moja kwa wakati mmoja, ili waweze kuishi vizuri na kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Mathayo 6:24.

Marko 10:11-12.

1Wakorintho 7:1-3.

ENGLISH: HE HAS PASSED THE LEATHER BELT.

The above saying refers to the one-sided dependence of a polygamist. Such man, however, had two wives whom he could not afford in order to take care for them because he depended on only one wife and abandoned the other. That is why people said that, “He has passed the leather belt.”

This saying is applied to the person who initiates many tasks at once, in his works. This person, in turn, initiates many projects that he or she is not able to accomplish all at once and is alone, in his or her life. He/she lives in the midst of a lack of property in his family, because of his inability to complete the projects that he started, in life.

This resembles the man who married a polygamist and leaned on one wife and abandoned the other, because he also initiates many projects at the same time and fails to complete them, in his enactment. That is why people said to him that, “He has passed the leather belt.”

This saying imparts in people an idea on having one wife, and seriously implementing one task at a time, so that they can live well enough to achieve more success in their lives.

Matthew 6:24.

Mark 10: 11-12.

1Corinthians 7: 1-3.

masai-warrior-474731__480

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.