1018. NG’WENUYU JIITA MAKUB’I.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya ng’ombe iyo ili mbisuji. Abhasugi bha ng’ombe yiniyo, bhagashemaga mab’ele mingi noyi kunguno ya bhub’isuji bhoyo bhunubho. Abhoyi bhagagalilaga na bhugali amab’ele genayo mpaga bhiguta bho nduhu nulu gulila makub’i gangi kunguno agoyi ha makub’i gabho lulu. Hunagwene bhagaitanaga ing’ombe yiniyo giki, “ng’wenuyo jiita makub’i.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayilanhanaga chiza ikaya yake bho guipandikila jiliwa ja julya pye amakanza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga kutumama milimo yakwe bho bhukamu bhutale, mpaga opandika sabho ningi kunguno ya b’utungilija bhokwe ukubhanhu bhakwe, umukikalile kakwe kenako. Uweyi agaponaga pye ijo agalimaga kunguno agadebhile chiza amakanza ga gulima bhuli jene ijo agalimaga, umubhutumami bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ng’ombe iyo yafunyaga mab’ele mingi, kunguno nuweyi agigulambijaga kutumama milimo chiza mpaga apandikaga sabho ningi ja gudula gubhagunana chiza abhanhu bhakwe bho pye amakanza. Hunagwene abhanhu bhakwe bhenabho bhagang’witanaga giki, “ng’wenuyo jiita makub’i.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho chiza na gusuga mitugo mingi, kugiki bhadule gupandika sabho ningi ija gubhambilija bho pye amakanza, umuwikaji bhobho.

Isaya 55:1.

Mwanzo 18:6-8.

KISWAHILI: HUYU KIMWAGA MBOGA.

Msemo huo, huongelea juu ya ng’ombe aliyetoa mazima mengi. Wafugaji wa ng’ombe huyo, humkamua mazima mengi sana kutoka kwake kwa sababu ya utajiri wake huo. Wao huyatumia maziwa hayo kwa kuliia ugali, kwa sababu hayo ndiyo mboga yenyewe. Hata kama wapishi watawapelekea mboza ja majani, zitarudi bila kutumiwa na wafugaji hao. Ndiyo maana wafugaji hao humuita ng’ombe huyo kwamba, “huyu kimwaga mboga.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huitunza vizuri familia yake kwa kuipatia chakula cha kutumia kwa muda wote, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake kwa bidii kubwa mpaka anafanikiwa kupata mali nyingi kwa sababu ya uaminifu wake huo kwa watu wake, maishani mwake. Yeye hufanikiwa kupata mavuno mengi kila mwaka kwenye mazao anayolima, kwa sababu anafahamu vizuri muda wa kuanza kulima kila zao, katika kazi yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na yule ng’ombe aliyetoa mazima mengi ya kuwatosha wafugaji wake, kwa sababu naye hufanya kazi kwa bidii na kupata mali za kutosha kuitunza familia yake kwa muda wote. Ndiyo maana wanafamilia wake hao, humuita kwamba, “huyu kimwaga mboga.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao vizuri na kufuga mifugo mingi, ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuwasaidia kwa muda wote, maishani mwao.

Isaya 55:1.

Mwanzo 18:6-8.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.