981. OZUB’ANGAGA.

Olihoyi nkima umo uyo ozugaga jiliwa. Unkima ng’wunuyo, ogazuga jiliwa jib’isi kunguno ya bhuzuki bhokwe ubho sagala bhunubho. Uweyi agenheleja bhanhu gwikala na nzala kunguno ya guduma ugujilya ijiliwa jakwe ijib’isi jinijo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “ozub’angaga.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adatumamaga chiza imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga sagala sagala imilimo, iyo ilikihamo na bhulimi, na bhusuluja, kunguno ya gugayiwa bhudiliji bho milimo yakwe yiniyo. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa jagulya aha kaya yakwe, kunguno ya gugayiwa bhudiliji bho milimo yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nkima uyo agazuga jiliwa jib’isi, kunguno nu weyi agatumamaga sagala sagala bho nduhu uguidilila chiza imilimo yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ozub’angaga.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija guitumama imilimo yabho bho guidilila chiza, kugiki bhadule gupandika jiliwa na sabho ja gubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Warumi 12:11.

Mathayo 24:13.

KISWAHILI: UMEHARIBU.

Alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa akipika chakula. Mwanzake huyo, alipika hovyo chakula hicho kikawa kibichi kwa sababu ya kukosa umakini wa kujali vizuri kazi yake. Yeye alisababisha watu kushinda na njaa kwa sababu ya kushindwa kukila chakula chake hicho kibichi. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umeharibu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule asiyeyatekeleza vizuri majukumu yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi zake hovyo hovyo, ambazo ni pamoja na zile za kilimo na biashara, kwa sababu ya kutokujali kwake kazi zake hizo. Yeye hukosa chakula nyumbani kwake kwa sababu ya kukosa umakini wake huo, katika utekelezaji wa majukumu yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mwanamke aliyepika hovyo chakula chake kikawa kibichi, kwa sababu naye hufanya kazi zake hovyo, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “umeharibu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao kwa kuyajali vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi, maishani mwao.

Warumi 12:11.

Mathayo 24:13.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.