789. WAJAGA NA NDA YAKWE.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya nda ya ng’wa munhu uyo ozumalikaga. Umunhu ng’wunuyo, agoyaga ugutubha kunguno ya goya ugwiigwa. Abhanhu abho bhagampinihalilaga mpaga bhaduma ugutumama imilimo yabho, bhagakomelejiywagwa gwendelea na milimo kunguno abhoyi bhatali bhulya ijiliwa, alu njimiji ung’wene, ojaga na nda yakwe. Huangwene abhanhu bhayombaga ulu munhu ozumalikaga giki, “wajaga na nda yakwe.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapandikaga makoye apinihala mpaka oduma ugutumama imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agazongaga noyi mpaga ogayiwa inguzu ja gwendelea uguitumama chiza imilimo yakwe kunguno ya gwendelea gugizuka amakoye ayo gampandikaga. Uweyi agiyenhelejaga nose kupandika makoye gangi ayo gali kihamo na gugayiwa ijiliwa aha kaya yakwe, kunguno ya gwikala makanza malihu bho nduhu ugutumama imilimo yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nabho bhagachilwa na ng’wichabho bhumpinihalila mpaga bhoya uguitumama imilimo yabho, kunguno nuweyi, agadumama ugutumama imilimo yakwe, ulu opandikaga makoye, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki amakoye ayo gabhita gikolile nu munhu uyo, “wajaga na nda yakwe.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na wiyumilija bho gugamala wangu amakoye ayo bhali nago, umukikalile kabho, kugiki bhadule guitumama chiza imilimo yabho, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 3:19.

KISWAHILI: AMEENDA NA TUMBO LAKE.

Msemo huo, huongelea juu ya tumbo la mtu aliyefariki dunia. Mtu huyo, hukoma kujisikia njaa kwa sababu ya kukoma kujihisi. Hivyo, watu wanaomhudhunikia mpaka kufikia hali ya kushindwa kuyatekeleza majukumu yao, huhimizwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwa sababu wao wanahitaji kula, lakini aliyefariki ameenda na tumbo lake. Ndiyo maana watu hao huambiwa kwamba aliyefariki, “ameenda na tumbo lake.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huhudhunika kwa muda mrefu kila anapopata matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hufikia hali ya kushindwa kuyatekeleza majukumu yake ya kila siku kwa sababu ya kuendelea kulifikiria tatizo lililopita katika maisha yake. Yeye hujikuta mwishowe amepata matatizo mengine, yakiwemo yale ya kukosa chakula katika familia yake, kutokana na kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi.

Mtu huyo, hufanana na wale waliacha kufanya kazi zao kwa sababu ya kufiwa na mwenzao, kwa sababu naye hushindwa kuyatekeleza majukumu yake kwa sababu ya kuyafikiria matatizo yaliyopita, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, matatizo hayo ni sawa na mtu aliyefariki ambaye, “ameenda na tumbo lake.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuyamaliza mapema matatizo wanayokumbana nayo, katika maisha yao, ili waweze kuendelea kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Mwanzo 3:19.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.