780. NG’HOMBA YA NG’WISONZO UDIKOMBA WIMALE.

Ilisongo jiliseme ijo jigabhejiyagwa bho gutumila madala. Amadala genayo, gagalyenhelejaga gubhiza na tujishepo, umo idulie gwingila inhomga ulu yuditilwa moyi. Giko lulu, umunhu uyo aliyikomba imhomba yiniyo aduyimala. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “Ng’homba ya ng’wisonzo udikomba wimale.”

Usulumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo adagudebhile chiza, umukikalile  kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agadumaga uguimala chiza imilimo yakwe, kunguno ya gwandya guitumama bho nduhu uguitila bhukengeji. Uweyi agapandikaga makoye mara hingi ahakaya yakwe, kunguno ya guduma ugubisha ijiliwa, umukikalile  kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agakomba ng’homba ng’wisonzo uduma uguimala, kunguno nuweyi agadumaga uguimala chiza imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ng’homba ya ng’wisonzo udikomba wimale.”

Usulumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuidebha chiza tamu imilimo yabho, na bhandye uguitumama, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Marko 6:40-44.

KISWAHILI: UJI WA KWENYE KISONZO HUWEZI UKAUKOMBA UUMALIZE.

Kisonzo ni chombo ambacho hutengenezwa kwa majani fulani yaitwayo ‘madala.’ Madala hayo, husababisha kuwepo kwa vitundu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kuruhusu uji upenye ndani yake. Hivyo basi, mtu anayekomba uji ule hawezi kuumaliza. Ndiyo maana watu husema kwamba, “uji wa kwenye kisonzo huwezi ukaukomba uumalize.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi ambayo haielewi vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, hushindwa kuzimaliza vizuri kazi zake hizo, kwa sababu ya kuanza kuzitekeleza bila ya kuzifanyia utafiti. Yeye huwa anapata matatizo mara nyingi kwenye familia yake, kwa sababu ya kushindwa kuivisha chakula, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekomba uji wa kwenye kisonzo, akashindwa kuumaliza, kwa sababu naye hushindwa kuzimaliza kazi zake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “uji wa kwenye kisonzo huwezi ukaukomba uumalize.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzielewa vizuri kazi zao kwanza kabla ya kuanza kuzitekeleza, katika maisha yao, ili waweze kupata maendeleo mengi, maishani mwao.

Marko 6:40-44.

porridge uji1

porrdge uji2

porridge uji3

basket uji

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.